Political asylum: Walioshiriki kutaka kumuua Dr Ulimboka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Political asylum: Walioshiriki kutaka kumuua Dr Ulimboka

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ng`wanakidiku, Jun 30, 2012.

 1. Ng`wanakidiku

  Ng`wanakidiku JF-Expert Member

  #1
  Jun 30, 2012
  Joined: Apr 18, 2009
  Messages: 1,196
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Great Thinkers,
  Naamini JF ni kisima cha busara na darasa kwa watanzania wote. Ni imani yangu wale wote waliohusika na jaribio la kutaka kumuua Dr Ulimboka wanapita JF na kusoma update ya nini kinaendelea. Asilimia 99.9% ya watanzania mpaka sasa tunaamini serikali ndiyo imehusika kwa huu unyamana na ni vigumu kutushawishi. Ningeshauri wahusika waliohusika na hili tukio watueleze kilichopo nyuma ya pazia, ila kwa kulinda usalama wao nashauri wafanye hivyo kwa kuzingatia yafuatayo.
  1. Watafute ukimbizi wa kisiasa kwa kwenda kwenye balozi za nchi za nje, haswa zinazoaminika kwa kulinda haki za binaadamu, na wakiwa huko waeleze kilichotokea kwa kutumia vyombo vya habari.
  2. Kama wewe ni polisi/usalama wa taifa unayo haki ya kwenda balozi yeyote (Mfano Ubalozi wa Norway, UK, Canada, USA, Danmmark, etc).
  3. Fanyeni hivyo bila kuongopa. Mtatusaidia sana watanzania, wakati wa ukombozi ni sasa.
  4. Nawasilisha
   
 2. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #2
  Jun 30, 2012
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Ama kweli kuna watu hamnazo. Hivi unatarajia waje waeleze upuuzi wao hapa!!!! Wangeeleza hata kabla hawatekeleza mpango huo hapa JF kama wangekuwa na nia njema sembuse kuja kueleza upuuzi wao.
   
 3. m

  mr.dominick JF-Expert Member

  #3
  Jun 30, 2012
  Joined: Jun 21, 2012
  Messages: 244
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  waende wapi??? kuwatetea uamsho ???? hao wanaotumwa na waarabu kuweka fujo ili kurudisha utumwa . Yeyiote atayefanya upuuzi kama huo wa kisultani atakula kisago aende kwa mabwana zake waarabu
   
 4. Ng`wanakidiku

  Ng`wanakidiku JF-Expert Member

  #4
  Jul 1, 2012
  Joined: Apr 18, 2009
  Messages: 1,196
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Naona wewe umesoma huku unakimbia. Mi sijasema waje waeleze JF, Pointi yangu ni kuwa:
  1. Kuna uwezekano baada ya mission kushindwa wanaweza wakauawa na serikali,
  2. Njia pekee ya wao kujiokoa ni kukimbilia balozi za nje, na hiyo huwa ni kawaida kabisa, ila sema kwa watanzania wengi wetu ni mbumbu wa sheria nyingi zinazolinda haki za binaadamu, ndiyo maana hata wewe umekurupuka kujibu
  3. Kwa kufanya hivyo watakuwa wametusaidia kufahamu ukweli na wao wataenda kushi maisha ya raha huko waendako badala ya kuwa marehemu bongo
  4. Hizi ni njia zinatumika na wanaharakati wengi haswa ambao hawafahamiki ambao wanaweza kuuawa na dunia isitambue.
  5. Nimetoa haya maoni kwa kuzingatia kuwa wao kama walishinikizwa na serikali na hawakutumiza maana yake inaonekana hawakuridhia kumuua Dr
   
 5. Ng`wanakidiku

  Ng`wanakidiku JF-Expert Member

  #5
  Jul 1, 2012
  Joined: Apr 18, 2009
  Messages: 1,196
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  E bwana na wewe naona hujaelewa ujumbe. Mi sijataja uamusho. Mi nimeongelea maisha ya hao waliohusika, kama kweli ni watu wa usalama (including police) uwezekano mkubwa wa kuuawa na wao ili kuficha siri inawezekana, kwa hiyo njia pekee ya wao kuepuka na kifo na maisha ya wasiwasi ni kuondoka nchini huku wakiweka bayana yaliyojili. Inabidi uombe msamaha kwa kutokuelewa maandiko yangu.
   
 6. m

  mr.dominick JF-Expert Member

  #6
  Jul 1, 2012
  Joined: Jun 21, 2012
  Messages: 244
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Niombe msamaha kwani hao askari na wanausalama wamefanya lipi baya , yaani wewe unawapenda hao madaktari vibaraka wanaotumiwa na waarabu na masultani kuleta fujo nchini . Hivi hao si waafrika wazalendo ??? kwa nini hawana moyo wa kulisaidia taifa wakati huu ambao taifa linajitahidi kuinua uchumi wake??? Hao wametumwa na mabwana zao waarabu na uamsho waache waonje joto ya jiwe
   
 7. Ng`wanakidiku

  Ng`wanakidiku JF-Expert Member

  #7
  Jul 1, 2012
  Joined: Apr 18, 2009
  Messages: 1,196
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  No no no no, Mr. dominick hapa umekosea. Hakuna vikundi/kikundi (uamusho n.k) wanaohusika ktk hili sakata. Mimi nilipata kuwa mazingira ya muhimbili kwa kipindi fulani kwa kazi maalumu, wale jamaa mazingira yao ni mabovu.

  Mtu unakuta anatumia masaa kama 14 anafanya kazi, wakati huohuo baadhi ya vifaa havipatikani, na kupelekea baadhi ya wagonjwa kufariki kwa kukosa vifaa. Kazi ya U Dr ni ngumu sana (hasawa Tanzania) kwani unaweza shuhudia mgojwa anakufa kisa imekosekana huduma ya kifaa fulani.

  Na Dr ni mtu pekee anayebaki na hilo donda moyoni mwake. Na pia kwenye suala la mishahara nadhani wanayo haki ya kulipwa zaidi kwani shule yao ni ngumu sana na afya ni msingi na nguzo ya maendeleo ya taifa lolote.
   
 8. Gavana

  Gavana JF-Expert Member

  #8
  Jul 1, 2012
  Joined: Jul 19, 2008
  Messages: 17,986
  Likes Received: 1,557
  Trophy Points: 280
  kwani wanalipwa kiasi gani hivi sasa hata waamue kuuwa binadamu wenzao ???

  Wamshukuru Kikwete kwa ubinaadamu wake , Unaijua hali ya hospitali wakati wa Nyerere ??? kuna mtu alithubutu kulalamika ???
   
 9. z

  zanzibar huru Senior Member

  #9
  Jul 1, 2012
  Joined: May 28, 2012
  Messages: 184
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  kwa nini asiombe political asylum ubalozi wa Malawi Tanzania?

  Kwa nini aingie gharama za kwenda denmark na kwingineko?
   
 10. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #10
  Jul 1, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  unakurupuka sana,,,,jitahidi sana kutuletea ushahidi nasi tuwe informed
   
 11. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #11
  Jul 1, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  wa kuendelea kuwavumilia wabadhilifu,,,ni vizuri akawa mkali kotekote,,,(kwa madaktrar,mafisad,mawaziri wake vihiyo)si kwa watu wa aina moja tu,,,,,
   
 12. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #12
  Jul 1, 2012
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Mkuu swali hilo unapaswa uwaulize waliotumwa kumuua Ulimboka, unatakiwa uwaulize walilipwa kiasi gani.

  Hali ya Hospitali wakati wa Nyerere ilikuwa nzuri mara 100 kuliko sasa, watu walikuwa wanakwenda kutibiwa bila kulipa, na dawa, vifaa vya kazi na mazingira ya kazi ya madakatari kwa wakati ule yalikuwa si mabaya. Nilikwenda kutibiwa mara kadhaa hospitali zile mpaka leo nakumbuka. Hata majengo mengo unayoyaona sasa ni yaliyojengwa na serikali ya Nyerere.
   
 13. m

  mr.dominick JF-Expert Member

  #13
  Jul 1, 2012
  Joined: Jun 21, 2012
  Messages: 244
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  unataka ushahidi kwani mnaposema uamsho wamechoma makanisa mnaleta na ushahidi ???
  kwanini wasiwe ndio hawa madaktari wanaogoma na kuhatarisha maisha ya waafrika masikini
   
 14. m

  mr.dominick JF-Expert Member

  #14
  Jul 1, 2012
  Joined: Jun 21, 2012
  Messages: 244
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mbona Gavana kasema ukweli tu , wakati wa Nyerere hata chumvi ya kuweka katika chakula ununue kwa magendo, wqewe ulikuwa hujazaliwa nini???

  hao vitimbakwiri wanaweka maslahi yao kuliko maslahi ya taifa kwanza . Daktari kule Zanzibar hata hawafiki milioni mshahara wao na huwasikii kugoma kwa uzalendo hawa wanaotumiliwa na waarabu na masultani ndio mbio wanataka kuleta ugaidi wa kuua waafrika masikini za Mungu
   
 15. b

  bantulile JF-Expert Member

  #15
  Jul 1, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 1,439
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  Hakuna haja ya kukimbilia nje ya nchi. Tanzania ni yetu wote. Kwa mwenye cheo cha Uraisi, uwaziri ukurugenzi hata asiye na cheo chochote maadamu ni mzawa asili ya Tanzania tushirikiane kuondoa uozo wowote kama upo.

  Ikulu ni yetu silaha ni zetu askari ni wetu, hatuwezi kukimbia kuachia nchi yetu mbwa.

  Hata wakiua watu 100 hata elfu lakini iko siku nchi itakomboka. Vizazi vyetu vitafaidi hayo matunda. Haki haitolewi kama zawadi kwenye kisahani- inadaiwa kwa udi na uvumba. Dr. Uli angekuwa mwoga hata posho zilizoongezeka zisingeongezeka.

  Damu ya Dr. Uli ni gharama kila jema lililotendeka katika seta ya Afya bila kusahau kumng'oa Blandina Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.

  Nimepita JKT ya Nyerere. Wewe uliyetoa wazo lakuwa wakimbizi umenichochea hasira. Nikimbie nikateseke nchi ya watu niwakimbie watanzania wenzangu. HAIWEZEKANI, TUTABANANA HAPA.
   
 16. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #16
  Jul 1, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  serikali yetu ilivyo ya kimafia hata ukikimbilia canada watakufuata huko huko wakumalize usifanye mchezo na hii nchi
   
 17. Christine1

  Christine1 JF-Expert Member

  #17
  Jul 1, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 12,276
  Likes Received: 1,204
  Trophy Points: 280
  Hiv ww ni mgeni hapa Tz?manaake its like u dont knw wht is going on
   
 18. meningitis

  meningitis JF-Expert Member

  #18
  Jul 1, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 8,020
  Likes Received: 911
  Trophy Points: 280
  Nimekusoma!
  THREE MAY KEEP A SECRET IF TWO OF THEM ARE DEAD
   
 19. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #19
  Jul 1, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,744
  Likes Received: 12,820
  Trophy Points: 280
  Sidhani kama umefikiria vizuri kabla ya kupost
   
 20. Keen

  Keen JF-Expert Member

  #20
  Jul 1, 2012
  Joined: Sep 27, 2007
  Messages: 620
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kuna daktari namfahamu anatibu wagonjwa kwa kutumia baadhi ya vifaa vya kununua yeye mwenyewe na akimaliza kazi siku hiyo anaondoka navyo!!

  On a serious note, hospitali nyingi za umma hazina vitendea kazi. Hata hivyo suala la kutekwa na kufanyiwa unyama dkt Ulimboka sina hakika sana kama serikali ina hizo asilimia zote (99.9%) za watanzania wanaoamini kuwa imehusika.

  Kama kweli imehusika basi ni failure ya state intelligency kwani sitegemei kama serikali inaweza ikafanya kitu cha ki-intelijensia ambacho almost kila mtu anaweza ku-associate kwa urahisi na serikali.

  Kwa mtizamo wangu kulikuwa na njia nyingi za kufanya ikiwemo kumfungulia kesi kama ambavyo wengine wanadai kuwa amesababisha vifo kwa kuchochea mgomo wa madaktari, etc. kuliko hatua waliyochukua.
   
Loading...