Polisi Zanzibar yapiga `stop` maandamano kudai umeme

Mzee wa Kale

Member
Feb 7, 2009
44
0
Na Mwinyi Sadallah

8th January 2010.

Jeshi la Polisi Zanzibar, limezuia maandamano ya kudai kurejeshwa kwa huduma ya umeme Zanzibar.

Hatua hiyo imetokana na polisi kukabiliwa na maandalizi ya maadhimisho ya miaka 46 ya Mapinduzi ya Zanzibar yatakayofanyika Januari 12, kisiwani Pemba.

Maandamano hayo yalitayarishwa na Chama cha Demokrasia Tanzania (Chadema) yalikuwa yafanyike Januari 10, mwaka huu, kuanzia viwanja vya Maisara na kupokewa na Mwenyekiti wa taifa wa chama hicho, Freeman Mbowe katika uwanja wa Kibandamaiti.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi, alisema maandamano hayo yamezuiwa kutokana na askari polisi kwa sasa kukabiliwa na majukumu mazito ya kufanikisha maadhimsho ya sherehe za Mapinduzi.

“Askari wengi wanakabiliwa na maandalizi ya maadhimisho ya miaka 46 ya Mapinduzi, hivyo, wasingeweza kutoa ulinzi wa kutosha katika maandamano hayo,” alisema Kamanda Bakari.

Hata hivyo, alisema Jeshi la Polisi lipo tayari kuruhusu mandamano hayo kama viongozi wa Chadema wataomba baada ya kumalizika kwa maadhimisho ya sherehe hizo.

Kwa mujibu wa barua ya polisi yenye kumbukumbu namba RPHQ/MJN/SO.7/2ª/OL1/171, wakati huu askari wanakabiliwa na harakati nyingi za kufanikisha maadhimisho ya miaka 46 ya Mapinduzi ya Zanzibar, hasa kwa kuzingatia Zanzibar itakuwa na wageni wengi wa kitaifa hivyo wasingeweza kujihusisha katika shughuli mbili kwa wakati mmoja.

Hata hivyo, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Hamad Mussa Yussuf, alisema chama hicho kitatoa msimamo wake leo, baada ya viongozi kukutana na kujadili uamuzi uliofikiwa na Jeshi la Polisi Zanzibar.

Alisema uamuzi huo umewasikitisha kwa vile maandamano hayo yalipangwa kufanyika Januari 10, mwaka huu wakati maadhimisho ya miaka 46 yanatarajiwa kufanyika Januari 12, Kisiwani Pemba.

Alisema lengo kubwa la maandamano hayo ni kumshindikiza Waziri Kiongozi, Shamsi Vuai Nahodha, kuchukua hatua ya kujiuzulu pamoja na Waziri wa Nishati ya Umeme, Mansour Yussuf Himid.

Naibu Katibu Mkuu huyo alisema Zanzibar imekosa umeme kutokana na uzembe wa viongozi katika kusimamia majukumu yao kwa vile waya wa umeme unaopokea huduma hiyo kutoka Tanzania Bara umeamaliza muda wake wa matumizi wa miaka 30 na hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa ya kuweka njia mpya kabla ya kumalizika muda wake.

Zanzibar imeanza kukosa umeme tangu Desemba 10, mwaka jana, baada ya kifaa kinachounganisha umeme kutoka Tanzania Bara aina ya Spliter kulipuka katika kituo cha Fumba na kusababisha huduma za kijamii na kiuchumi kuathirika.

CHANZO: NIPASHE
 
Of course Sangara hawaeleweki huko Zanzibar hivyo kinachoeleweka (tatizo la umeme) kinaweza kutumiwa kukampeni.

Cha kujiuliza Jee nani atakuwa anadaiwa autowe huo umeme?
 
Mkuu Ngekewa,

Kinachofanywa na CHADEMA ni kuhakikisha uwajibikaji unakuwepo, ili viongozi waweze kuwajibika kwa matendo yao, sina hakika kama unajua Mawaziri zaidi ya 20 wa SMZ kila mmoja ana gari la kifahari lenye thamani ya zaidi ya 200 M. lakini hawana fedha za dharura kwa ajili ya kukabiliana na janga linalotukabili, vifo vya watanzania wasio na hatia vimesharipotiwa katika hospitali ya Mnazi mmoja, viwanda vimeshafunga kuzalisha bidhaa, huduma za maji safi hakuna, magonjwa ya mripuko yameshaanza kuripotiwa,

Wakati nchi ikikabiliwa na kila aina ya matatizo watawala wanajiandaa na sherehe za miaka 46, kisiwani Pemba ambazo zitaligharimu Taifa zaidi ya 3.5 Bilioni. na huku wakishindwa kusaidia wananchi kutokana na janga hili lililopo, sina hakika ulitaka CHADEMA waweze kuchukua hatua gani zaidi ya hii ambayo wametaka kuichukua.

Naomba utafakari na wewe uweze kuchukua hatua.
 
Of course Sangara hawaeleweki huko Zanzibar hivyo kinachoeleweka (tatizo la umeme) kinaweza kutumiwa kukampeni.

Cha kujiuliza Jee nani atakuwa anadaiwa autowe huo umeme?

Hata na wewe pia ni one of the great?Kuandamana ni haki ya kikatiba ya kila mwananchi katika ulimwengu wa demokrasia.

Huyo mwandishi ni Sadallah, ni kibaraka wa CCM katika gazeti la Mengi ambae nae pia ni mwanachama wa CCM.

Kwa ufupi, kuwazuia kuandamana ni ukandamizaji demokrasia.Kusema police wako bizzi, kwani tulitarajia wawe hawana kazi?Basi tuvunje jeshi la polici kama kuna siku huwa hawana kazi....kusimamia maandamano ni muhimu sawa na sherehe nyengine zozote zile.
 
Mkuu Ngekewa,

Kinachofanywa na CHADEMA ni kuhakikisha uwajibikaji unakuwepo, ili viongozi waweze kuwajibika kwa matendo yao, sina hakika kama unajua Mawaziri zaidi ya 20 wa SMZ kila mmoja ana gari la kifahari lenye thamani ya zaidi ya 200 M. lakini hawana fedha za dharura kwa ajili ya kukabiliana na janga linalotukabili, vifo vya watanzania wasio na hatia vimesharipotiwa katika hospitali ya Mnazi mmoja, viwanda vimeshafunga kuzalisha bidhaa, huduma za maji safi hakuna, magonjwa ya mripuko yameshaanza kuripotiwa,

Wakati nchi ikikabiliwa na kila aina ya matatizo watawala wanajiandaa na sherehe za miaka 46, kisiwani Pemba ambazo zitaligharimu Taifa zaidi ya 3.5 Bilioni. na huku wakishindwa kusaidia wananchi kutokana na janga hili lililopo, sina hakika ulitaka CHADEMA waweze kuchukua hatua gani zaidi ya hii ambayo wametaka kuichukua.

Naomba utafakari na wewe uweze kuchukua hatua.

Hivyo wewe kama wewe unaweza kutowa suluhiisho gani ambalo viongozi wa Zanzibar wachukuwe ili kutatua tatizo hili zaidi ya hatuwa zilizokwishachukuliwa?
Hili suwala la magari nafikiri haliwezi kutatuwa matatizo kwani hiyo ni hallisa yao kuwa na magari ambayo kwa bei ya sasa 200 milioni ni gari ya kawaida tu.
Tukija kwenye mada yenyewe hivyo tangu lini suwala la umeme wa Zanzibar likawa katika sera za CHADEMA? Hivyo hao CHADEMA hawaelewi kuwa suwala la umeme kutegemea kutoka Bara ni tatizo kubwa kwa Zanzibar? Lini walilisemea hilo au sera yao inasema kuwa ulinvamazie tatizo mpaka itokee ajali ndipo ulieleze? Hivyo CHADEMA wa Bara na Visiwani hawashuhudii Zanzibar inavyonyanyaswa kwa umeme huo na ndugu zao wa Bara, mbona kila mara wananyamaz kimya? Kwa kweli ningewaona wana ajenda ya maana kama tatizo hili wangekuwa wakilifuatilia badala ya kusubiri ajali na kutaka kujikweza kisiasa.

Maoni yangu kwa CHADEMA ni kuwa kwa mtaji huu hawawezi kujijenga kisiasa Zanzibar kwani huko hakuna ile 70% aliyosema JK.

Mimi si mpenzi wa utawala wa CCM kule Zanzibar lakini kwa hili namuunga mkono Karume kwa hapo chini:

President Karume snubs opposition over resignation pressureMost Read

ISSA YUSSUF in Zanzibar, 8th January 2010 @ 15:03, Total Comments: 0, Hits: 406

PRESIDENT Amani Abeid Karume has dismissed the pressure, calling on some of his ministers to resign due to the current power crisis, saying it was unjustified.

“I read some newspaper headlines this morning. One of the papers said the Minister responsible for Energy and the Chief Minister should resign because of power blackout. This was an accident and not someone’s fault,” Mr Karume said at a function yesterday to open an FBME Bank branch at Kisiwandui.

Mr Karume thanked the Executive Chairperson of the FBME Bank Mr Ayoub Farid Saab for considering Zanzibar as a convenient place for the business. He called upon the business community and Zanzibaris to use the bank, which has been recording success since its establishment on the islands in 2003.

The visibly angry president expressed his disappointment with the press for ‘publishing stories which could divide people and may ignite conflicts.’

“In such difficult times, the media and well-wishers should sympathize with us and console us instead of pointing an accusing finger at someone,” he noted.

There have been critics from the media and the opposition parties, particularly CHADEMA that Zanzibar authorities had not done enough to prevent the blackout, asking the minister for energy Mr Mansour Yussuf Himid and the Chief Minister Mr Shamsi Vuai Nahodha to resign.

CHADEMA had planned a mass demonstration on Sunday to express their discontent, but the police turned down the party’s plan.

CHADEMA also had asked Mr Karume to dissolve his cabinet and fire some ministers for failing to act responsibly “You start demanding that the minister should resign, the next might be the chief minister and who next if not the president? Definitely this is unacceptable,”

Mr Karume said, adding that Zanzibar was going through ‘a very trying moment’.

In a separate meeting with journalists yesterday afternoon, Mr Masour Yussuf Himid said that electricity in Unguja would be restored on February 20th if the current efforts to restore power would materialize.

“We have already allocated about USD 500,000 for the restoration of power, which includes procurement of materials from South Africa and Sweden.

“Ericsson network technologies from Sweden has been contracted to upgrade the submarine cable at Ras Kiromoni in the mainland, and Fumba in Unguja,” Said Mr Mansour.

He noted that the main work was to replace the cable’s cooling system, which uses oil with new silicon type terminations that will not require oil. The minister said the outdated oil cooling system has been part of intermittent power failure on the submarine cable.

Mr Mansour also said that the government was in negotiations with its development partners and the union government to purchase standby generators as temporary measures.
 
...unapoona mwananchi ananyimwa haki yake ya msingi kudai haki yake, ndio ujue safari bado ni ndefu kuelekea kwenye demokrasia ya kweli!

...huwezi kusema maandamano kudai umeme ni mabaya kwakuwa tu opposition party ndio iloyaitisha.

Kukosekana kwa umeme Zanzibar hakujali CCM, CUF, jeshi la polisi, KMKM wala nani, ...wote mnateseka!

Stand up for your rights you people!
 
Hata na wewe pia ni one of the great?Kuandamana ni haki ya kikatiba ya kila mwananchi katika ulimwengu wa demokrasia.

Huyo mwandishi ni Sadallah, ni kibaraka wa CCM katika gazeti la Mengi ambae nae pia ni mwanachama wa CCM.

Kwa ufupi, kuwazuia kuandamana ni ukandamizaji demokrasia.Kusema police wako bizzi, kwani tulitarajia wawe hawana kazi?Basi tuvunje jeshi la polici kama kuna siku huwa hawana kazi....kusimamia maandamano ni muhimu sawa na sherehe nyengine zozote zile.

The same to you my brother, YOU ARE ONE OF GREAT THINKERS! Lakini nafikiri tuna wajibu wa kuelimishana na sio kupambana na kuelimishana ni kukubali ukweli. Kwa hili la CHADEMA na maandamano pia tuna haki ya kujadili kuona kuwa kuandamana kuwemo na maana ya kufanya hivyo na siyo kwa ajili ya kufanya tu.
Mbona tuna matatizo mengi Zanzibar na CHADEMA wako kimya nayo?
Na hili la kuzuiliwa na Polisi mbona sioni tatizo hivyo lazima wafuatwe CHADEMA na tarehe yao wakati wamwshaambiwa wachaguwe tarehe nyengine? Ivyo wanachama wachache wa CHADEMA na wananchi wengi wa Zanzibar wepi wapewe umuhimu zaidi?
Kila kitu ni mipangilio na kitu kisicho na mpangilio ni ajali peke yake basi tusiyafanye maandamano ya CHADEMA kuwa ajali na kulazimika kufanywa siku wanayotaka na wapange siku nyengine kwani kama nilivyosema hapo awali suala la tatizo la umeme Zanzibar limekuwepo na litaendelea kuwepo kwa muda mrefu.
 
...unapoona mwananchi ananyimwa haki yake ya msingi kudai haki yake, ndio ujue safari bado ni ndefu kuelekea kwenye demokrasia ya kweli!

...huwezi kusema maandamano kudai umeme ni mabaya kwakuwa tu opposition party ndio iloyaitisha.

Kukosekana kwa umeme Zanzibar hakujali CCM, CUF, jeshi la polisi, KMKM wala nani, ...wote mnateseka!

Stand up for your rights you people!

Mbona tunashindwa kutofautisha kuzuiliwa na kutakiwa kufuata utaratibu? Kwa bahati mbaya haki zote ziko kwenye utaratibu hivyo utaratibu unapotuzuia kwasababu fulani basi hilo haliitwi kunyimwa haki. CHADEMA hawajakatazwa lakini wamelazimika kufuata taratibu kwani si walioomba kibali? Kama haki yao ni kuandamana tu bila ya utaratibu basi kweli wamenyimwa haki lakini kama walifuata taratibu nao wakajibiwa kwa mujibu wa taratibu tatizo lio wapi hapo?
 
The same to you my brother, YOU ARE ONE OF GREAT THINKERS! Lakini nafikiri tuna wajibu wa kuelimishana na sio kupambana na kuelimishana ni kukubali ukweli. Kwa hili la CHADEMA na maandamano pia tuna haki ya kujadili kuona kuwa kuandamana kuwemo na maana ya kufanya hivyo na siyo kwa ajili ya kufanya tu.
Mbona tuna matatizo mengi Zanzibar na CHADEMA wako kimya nayo?
Na hili la kuzuiliwa na Polisi mbona sioni tatizo hivyo lazima wafuatwe CHADEMA na tarehe yao wakati wamwshaambiwa wachaguwe tarehe nyengine? Ivyo wanachama wachache wa CHADEMA na wananchi wengi wa Zanzibar wepi wapewe umuhimu zaidi?
Kila kitu ni mipangilio na kitu kisicho na mpangilio ni ajali peke yake basi tusiyafanye maandamano ya CHADEMA kuwa ajali na kulazimika kufanywa siku wanayotaka na wapange siku nyengine kwani kama nilivyosema hapo awali suala la tatizo la umeme Zanzibar limekuwepo na litaendelea kuwepo kwa muda mrefu.

Ni kawaida ya polisi Zanzibar kuzuia watu kuandamana, excuses hazishi.Na wewe unaonekana kufurahia, ukiona watu hawapei fursa ya kuandamana.

Watanzania ni lazima tukubali kwenda na wakati, tumekubali demokrasia then lets go with the flow!!

Dar iko nyuma kimisingi ya demokrasia, Zanzibar ndio imeoza kabisa.Kuandamana, vyombo vya habari, ni bora tuite tubadili jina tuite Myanmar :D
 
...ebana wee, polisi kukataa kutoa kibali cha maandamano eti kwakuwa wanajiandaa na sherehe za Mapinduzi sio sababu ya msingi. Huu ni uzembe unaotakiwa kulaaniwa vikali.

7 june 2007

Zanzibar gov't pledges to improve electricity supplies

The government of Zanzibar on Wednesday promised that by the end of next year the residents on both Unguja and Pemba islands will get more reliable electricity supplies.

The promise was made by Zanzibar Energy Minister Mansour Yusuf Himid while discussing the on-and-off power supply blues with the Zanzibar Electricity Company.

Zanzibar is laying a submarine cable to provide electricity from mainland Tanzania to Pemba with the financing support from the government of Norway.
The submarine cable project is expected to complete in two years time, with a projected cost of 400 billion Tanzanian shillings (320 million U.S. dollars).

The minister urged the management of the Zanzibar Electricity Company to better implement the rural electrification program which aims at providing electricity to 67 villages in Unguja and Pemba, the main islands of the Indian Ocean archipelago.
Source: Xinhua
Zanzibar Blackout to Last Another 90 Days, Says Expert.
Salma Said

4 June 2008
  • Zanzibar — The power blackout on Tanzania's paradise island of Zanzibar will drag on for at least three months, according to a Norwegian expert
Zanzibar blackout to last six more weeks: minister

AFP - Saturday, January 9, 2010

STONE TOWN, Tanzania (AFP) - – Zanzibar's energy minister said Friday that a month-long power blackout would last six more weeks, amid mounting criticism of the government over a crippling electricity crisis.

"We expect that we shall have power on the island on February 20," Mansour Yussuf Himid said at a press conference in the semi-autonomous Tanzanian island's capital Stone Town.

The archipelago's main island, Unguja, has been without power since December 10 due to a breakdown affecting the 30-year-old undersea cable providing electricity from the mainland.
 
Back
Top Bottom