Mzee wa Kale
Member
- Feb 7, 2009
- 44
- 0
Na Mwinyi Sadallah
8th January 2010.
Jeshi la Polisi Zanzibar, limezuia maandamano ya kudai kurejeshwa kwa huduma ya umeme Zanzibar.
Hatua hiyo imetokana na polisi kukabiliwa na maandalizi ya maadhimisho ya miaka 46 ya Mapinduzi ya Zanzibar yatakayofanyika Januari 12, kisiwani Pemba.
Maandamano hayo yalitayarishwa na Chama cha Demokrasia Tanzania (Chadema) yalikuwa yafanyike Januari 10, mwaka huu, kuanzia viwanja vya Maisara na kupokewa na Mwenyekiti wa taifa wa chama hicho, Freeman Mbowe katika uwanja wa Kibandamaiti.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi, alisema maandamano hayo yamezuiwa kutokana na askari polisi kwa sasa kukabiliwa na majukumu mazito ya kufanikisha maadhimsho ya sherehe za Mapinduzi.
Askari wengi wanakabiliwa na maandalizi ya maadhimisho ya miaka 46 ya Mapinduzi, hivyo, wasingeweza kutoa ulinzi wa kutosha katika maandamano hayo, alisema Kamanda Bakari.
Hata hivyo, alisema Jeshi la Polisi lipo tayari kuruhusu mandamano hayo kama viongozi wa Chadema wataomba baada ya kumalizika kwa maadhimisho ya sherehe hizo.
Kwa mujibu wa barua ya polisi yenye kumbukumbu namba RPHQ/MJN/SO.7/2ª/OL1/171, wakati huu askari wanakabiliwa na harakati nyingi za kufanikisha maadhimisho ya miaka 46 ya Mapinduzi ya Zanzibar, hasa kwa kuzingatia Zanzibar itakuwa na wageni wengi wa kitaifa hivyo wasingeweza kujihusisha katika shughuli mbili kwa wakati mmoja.
Hata hivyo, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Hamad Mussa Yussuf, alisema chama hicho kitatoa msimamo wake leo, baada ya viongozi kukutana na kujadili uamuzi uliofikiwa na Jeshi la Polisi Zanzibar.
Alisema uamuzi huo umewasikitisha kwa vile maandamano hayo yalipangwa kufanyika Januari 10, mwaka huu wakati maadhimisho ya miaka 46 yanatarajiwa kufanyika Januari 12, Kisiwani Pemba.
Alisema lengo kubwa la maandamano hayo ni kumshindikiza Waziri Kiongozi, Shamsi Vuai Nahodha, kuchukua hatua ya kujiuzulu pamoja na Waziri wa Nishati ya Umeme, Mansour Yussuf Himid.
Naibu Katibu Mkuu huyo alisema Zanzibar imekosa umeme kutokana na uzembe wa viongozi katika kusimamia majukumu yao kwa vile waya wa umeme unaopokea huduma hiyo kutoka Tanzania Bara umeamaliza muda wake wa matumizi wa miaka 30 na hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa ya kuweka njia mpya kabla ya kumalizika muda wake.
Zanzibar imeanza kukosa umeme tangu Desemba 10, mwaka jana, baada ya kifaa kinachounganisha umeme kutoka Tanzania Bara aina ya Spliter kulipuka katika kituo cha Fumba na kusababisha huduma za kijamii na kiuchumi kuathirika.
CHANZO: NIPASHE