mshumbusi
JF-Expert Member
- Oct 24, 2011
- 457
- 232
Jeshi la Polisi Zanzibar, wamefuta ratiba ya mahojiano yao na Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi - CUF, Maalim Seif Shariff Hamad ambaye pia alikuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar 2010-2015 yaliyokuwa yamepangwa kufanyika kesho Ijumaa, tarehe 27 Mei, 2016, Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, Ziwani, Zanzibar.
Sababu za kufutwa kwa ratiba hiyo hazijawekwa wazi na mahojiano hayo yatapangwa siku nyengine. Aidha watu wengi wamekuwa wakitoa maoni yao juu ya hatua hiyo ya Polisi inayooonekana kama na kisiasa zaidi kuliko kiusalama wa raia na mali zao, maana Maskani ya kisonge imekuwa ikitoa kauli tata na chongani na hakuna hata kiongozi mmoja wa Kisonge aliyeitwa Polisi kwa mahojiano.
Baadhi ya wanasiasa kama Silima Mtumwa Borafya (Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mjini Unguja) maye pia amekuwa akitoa kauli tata na chongani lakini haijawahi kuelezwa ni lini ataitwa na jeshi la Polisi kwa mahojiano, sababu hizo na nyengine nyingi ndizo zinazofanya baadhi ya wadadisi wa masuala ya kisiasa Zanzibar kuhoji busara ya Polisi katika zoezi hili na kuonekana likielemea kisiasa kwa chama tawala.
Huku hayo yakiendelea imeelezwa baadhi ya wanachama wa CUF hususani kisiwani Pemba wanaendesha visomo kumshitakia Mungu juu ya madhila wanapopatiwa na Polisi huku wanasheria wa CUF wakikusanya vielelezo juu ya vitendo vya ukatili dhidi ya binaadamu kwa ajili ya kuanzisha mashitaka ya kimataifa.
Chanzo : zanzibar post