Polisi Zanzibar wadaiwa kusuasua kutoa idhini ya maandamano

Sokomoko

JF-Expert Member
Mar 29, 2008
1,915
127
Polisi Zanzibar wadaiwa kusuasua kutoa idhini ya maandamano
Na Muhibu Said

JESHI la Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, kisiwani Unguja, linadaiwa kusita kuruhusu maandamano ya amani yaliyoandaliwa na Chama cha Wananchi (CUF) kisiwani humo ambayo yamepangwa kufanyika kesho.


Maandamano hayo yanatarajiwa kuongozwa na Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba kwa lengo la kukishinikiza Chama Cha Mapinduzi (CCM), kusaini rasimu ya makubaliano yaliyofikiwa katika mazungumzo ya kutafuta mwafaka wa kisiasa visiwani Zanzibar kati ya vyama hivyo.


Makubaliano hayo yalifikiwa na vyama hivyo kupitia kamati zao wiki chache baada ya kukamilika kwa mazungumzo hayo yaliyodumu kwa miezi 14.


Moja kati ya makubaliano yaliyofikiwa ni pamoja na kuundwa kwa serikali shirikishi, maarufu kama "serikali ya mseto" itakayoshirikisha vyama hivyo katika uundaji wa serikali visiwani humo.


Habari zilizolifikia gazeti hili kutoka Zanzibar, zinaeleza kuwa, hadi kufikia jana, polisi walikuwa hawajatoa uamuzi wowote wa kuruhusu au kutoruhusu kufanyika kwa maandamano hayo, licha ya uongozi wa CUF kisiwani humo, kutoa taarifa kwa Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Magharibi, juzi.


Hata hivyo, haijafahamika sababu za polisi kupata kigugumizi cha kuruhusu maandamano hayo, ingawa habari zinaeleza kuwa, tangu uongozi wa CUF upeleke taarifa hiyo polisi, viongozi wa jeshi hilo kisiwani humo, wamekuwa wakikutana kujadili suala hilo.


Hadi tunakwenda mitamboni jana jioni, hakukuwa na taarifa zozote za polisi kuhusiana na maandamano hayo huku uongozi wa CUF, ukihaha katika vituo vya polisi kufuatilia.


Akizungumza na Mwananchi kwa njia ya simu kutoka Zanzibar jana, Mkurugenzi wa Haki za Binadamu na Mahusiano na Umma wa CUF Zanzibar, Salim Bimani, alisema wameshangazwa na kimya hicho cha polisi ambacho alidai ni kinyume cha sheria.


Hata hivyo, Bimani alisema, jana waliendelea kufuatilia suala hilo polisi ili kuhakikisha maandamano hayo yanaruhusiwa kufanyika kesho.


Tamko la kufanyika maandamano hayo, lilitolewa na Lipumba katika mkutano wake na wazee, viongozi wa chama hicho wa Mkoa wa Dar es Salaam, katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam Aprili 6, mwaka huu.


Mkutano huo ulihudhuriwa na viongozi wakuu wa vyama vya Chadema, TLP na NCCR-Mageuzi, ili kutoa ufafanuzi kuhusiana na mazungumzo hayo na kujibu hotuba ya Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Kikwete, aliyoitoa katika ukumbi huo, Aprili 2, mwaka huu.


Katika hotuba yake hiyo, Kikwete alitetea uamuzi wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC-CCM), uliofikiwa katika kikao chake kilichofanyika katika kijiji cha Butiama, mkoani Mara, Machi 29-30, mwaka huu wa kutaka ifanyike kura ya maoni Zanzibar, ili kupata ridhaa ya wananchi ya kuundwa au kutoundwa kwa serikali ya mseto visiwani humo.


Hata hivyo, uamuzi huo ulipingwa vikali na viongozi wakuu wa CUF kwa nyakati tofauti, akiwamo Katibu Mkuu, Maalim Seif Shariff Hamad na kuhitimishwa na Lipumba kwa hoja kwamba, suala hilo halikuwamo katika ajenda za mazungumzo wala sheria za nchi na kuibuliwa kwake ni ghiliba za CCM kutaka kurefusha muda wa mazungumzo.


Maandamano hayo yanatarajiwa kuhudhuriwa na wabunge wa CUF ambao pamoja na wenzao wa vyama vya Chadema na UDP, Jumanne wiki hii walisusia kikao cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kinachoendelea mjini Dodoma.


Hawa jamaa nia yao ni kuendeleza mauaji kama yale waliyoyafanya 1964, si mnajua mapinduzi daimaaaa.
Mpaka watu wazima wanalia hawataki Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ibadilike iwe ya shirikisho!
 
Back
Top Bottom