Polisi Zanzibar: Sheikh Farid wa Uamsho hakutekwa; kufikishwa mahakamani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Polisi Zanzibar: Sheikh Farid wa Uamsho hakutekwa; kufikishwa mahakamani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mgomba101, Oct 21, 2012.

 1. m

  mgomba101 JF-Expert Member

  #1
  Oct 21, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,788
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Kamishna wa polisi ZNZ amesema kiongozi wa uamsho sheikh Farid hakutekwa bali alijifanya ametekwa ili kuanzisha vurugu zilizosababisha kifo cha askari.

  Pia amesema wamewakamata baadhi ya viongozi wa uamsho na watafikishwa mahakamani kesho Jumatatu.

  >>>>>>>>><<<<<<<<<<

  OKTOBA 21, 2012 | Zanzibar

  Jeshi la Polisi Zanzibar, linawashikilia watu 65 wakiwemo viongozi sita wa kundi la Uamsho na Jumuiya ya Maimam Zanzibar kwa tuhuma za kuchochea ghasia na vurugu zilizosababisha vitendo vya uporaji wa mali na uharibifu wa miundombinu ya barabara.

  Afisa Habari Mkuu wa Jeshi la Polisi Zanzibar Insptekta Mohammed Mhina, amesema kuwa pamoja na kukamatwa kwa viongozi hao wa Jumuia mbili za Kidini mjini Zanzibar, Polisi pia imewakamata watu wengine sita kwa tuhuma za mauaji ya Askari Polisi.

  Insepekta Mhina, amewataja viongozi waliokamatwa kuwa ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maimau Zanzibar Sheikh Faridi Hadi Ahmed(41) mkazi wa Mbuyuni na Sheikh Mselem Ali Mselem(52) wa Kwamtipura ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Uamsho Zanzibar.

  Wengine ni Sheikhe Azan Khalid Hamadi(48) wa Mtendeni, Hassan Bakari Suleiman(39) wa Tomondo na Ustaadh Mussa Juma Issa(33), Suleiman Juma Suleimain(66) pamoja na Mussa Juma Issa(37) wote wa Makadara mjini Zanzibar.

  Inspekta Mhina amesema viongozi waliokamatwa ni wale walikuwa wakihojiwa na Polisi tangu jana kwa lengo la kutafuta ukweli wa taarifa za kutekwa kwa Sheikh Farid Hadi Ahmed kulikopelekea ghasia na uharibifu mbalimbali kabla ya kujitokeza tena hadharani juzi.

  Akizungumza na Waandishi wa habari ofisini kwake, Kamamishina wa Polisi Zanzibar CP Mussa Ali Mussa amesema kuwa Jeshi la Polisi Visiwani humo linaendelea na operesheni maalumu ya kuhakikisha kuwa kila aliyehusika katika ghasi hizo anakamatwa na kukabili mkono wa sheria.

  Akizungumzia maendeleo ya Upelelezi wa Kesi ya Kuuawa kwa Askari Polisi CPL Said Abdarahaman Juma aliyeuawa usiku wa kuamkia Alhamis wiki iliyopita, Kamishna Mussa amesema Polisi wamefanikiwa kuwatia nguvuni watu sita kwa kuhusika na mauaji ya askari huyo.

  Amesema hadi sasa Polisi inawashikilia watu sita kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya askari huyo ambapo watuhumiwa watatu walikamatwa mjini Zanzibar na wengine watatu wamekamatwa mkoani Tanga.

  Kamishna Mussa amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Abdallah Mohammed Said(35) wa Mwanyanya, Joli Gasuli(20) wa Vuga, Bakari Juma Yusufu(22) wa Mwembe Makumbi na Amour Rished(40) wa Bububu ambao walikamatwa mjini zanzibar siku ya kwanza lilipotokea tukio hilo.

  Amewataja watuhumiwa wengine ambao wamekamatiwa Mkoani tanga na ambao tayari wamesharejeshwa Zanzibar kuwa ni Ali salum Seif(21) na Abubakari Haji Mbarouk(32) pamoja na mdogo wake Mohammed Haji Mbarouk(21) wote wakazi wa Ndagaa mkoa wa Kusini Unguja.

  Kamishna Mussa amesema Polisi bado inaendelea kuwahoji watuhumiwa hao na wale watakaobainika kuhusika na mauaji ya askari huyo watafikishwa mahakamani.

  Amesema kwa ujumla tangu kukamatwa kwa viongozi hao hali ya usalama katika mji wa Zanzibar imerejea upya na wananchi wameombwa kutoshabikia vitendo vyovyote vile vitakavyoweza kupelekea uvunjifu wa amani.

  Amewataka Wazazi na walezi kutowaruhusu watoto wao kshiriki katika mikusanyiko na kuwa chanzo cha fujo na kwamba kwa yeyote atakayekaidi agizo hilo atashughulikiwa ipasavyo na mkono wa dola.
   
 2. m

  mgomba101 JF-Expert Member

  #2
  Oct 21, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,788
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Huyu sheikh Farid amesababisha vurugu na kifo cha askari.Asipewe dhamana kama sheikh Ponda ili iwe fundisho kwa mijitu mingine yenye tabia za kipuuzi kama hizi.
   
 3. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #3
  Oct 21, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  Huo ndio ukweli wenyewe. Sheikh Farid alijiteka mwenyewe, wakaipa serikali masaa 26 kumrelease, ilipofikia masaa 26 Sheikh Farid alijirelease kutoka mafichoni, kuonyesha serikali imesalimu amri kwa Uamsho
   
 4. bemg

  bemg JF-Expert Member

  #4
  Oct 21, 2012
  Joined: Apr 25, 2010
  Messages: 2,706
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  mhh yetu macho na masikio .kazi kwenu mnaosimamia usalama wa raisa na mali zake
   
 5. Titans

  Titans JF-Expert Member

  #5
  Oct 21, 2012
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 868
  Likes Received: 1,073
  Trophy Points: 180
  haya sasa wale walofanya fujo huko znz, yani mtu huna hata hakika kama katekwa we waenda barabarani wavunja nguzo za umeme,kukata miti iliyopandwa na kuchoma matairi..sasa waliwaza kesho watapita road gani if leo wameharibu??wamewaza umeme watapata vipi ilhali leo wamevunja nguzo za umeme? utaskia "mfumo kristo"
   
 6. Myakubanga

  Myakubanga JF-Expert Member

  #6
  Oct 21, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 5,781
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Dah!
  Huyo Farid ni sheikh gaidi kabisa!
  Aibu kwa uislamu na waislamu kuwa na sheikh wa aina hiyo!!
   
 7. K

  Kagalala JF-Expert Member

  #7
  Oct 21, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 2,372
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 145
  Hapa Serikali ikicheza mchezo dhaifu na kuwachia huyu muhuni itakuwa aibu kubwa. Hasara aliyosababisha na kifo inabidi huwe ndo mwisho wa hiki kikundi. Kumbe ni wahuni hivi!
   
 8. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #8
  Oct 21, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,497
  Likes Received: 19,910
  Trophy Points: 280
  huyu jamaa amepata faida gani sasa baada ya wafuata upepo wake kumuua askari na kutaka kuua na kutishia kuua viongozi wa dini?
   
 9. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #9
  Oct 21, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,154
  Likes Received: 2,406
  Trophy Points: 280
  Huyo mtu anastahili kifungo tu cha maisha......
   
 10. takashi

  takashi JF-Expert Member

  #10
  Oct 21, 2012
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 909
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Serikali imeshateka raia mara kadhaa...Hawana mpya viongozi wa jeshi la Polisi wana chukua amri kwa viongozi wa CCM.
   
 11. takashi

  takashi JF-Expert Member

  #11
  Oct 21, 2012
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 909
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Serikali hiyo hiyo imekataa kama ilimteka dr,Ulimboka....Hawana mpya.
   
 12. a

  adolay JF-Expert Member

  #12
  Oct 21, 2012
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 7,595
  Likes Received: 3,074
  Trophy Points: 280
  Hapa tunaenda pabaya sana.

  Inawezekana vipi watu wachache kucheza na akili za watanzania na kuyumbisha Taifa zima kiasi hiki?

  Serikali inapaswa kuonesha ipo na kwa vitendo kila mmoja yampasa kutambua hivyo.

  Vitendo hivi ni kuidhalilisha serikali, kibaya zaidi watu wamekufa ........kwanini......
   
 13. Titans

  Titans JF-Expert Member

  #13
  Oct 21, 2012
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 868
  Likes Received: 1,073
  Trophy Points: 180

  mkuu..lakini waliowahi tekwa na serikali sote tunajua walivopatikana either hawana kucha na meno au maiti kabisa...lakini shehe karudi na kanzu nyeupeeeeeee hata damu na anatabasamu..hope ulimuona ulimboka alivorudi from mwabepande alikua hacheki anaugulia kiume...i dont buy ulichopost about huu utekaji wa shehe.
   
 14. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #14
  Oct 21, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,202
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Huyu gaidi nasikia anafadhiliwa na karume sijui kuna ukweli hapo wakuu?
   
 15. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #15
  Oct 21, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,228
  Trophy Points: 280
  technic ya shehe ya kitoto sana......

  Hivi anajua kutekwa?

  Hebu akamuulize ulimboka

  halafu hata hakumpanga dereva wake story zikafanana
   
 16. palalisote

  palalisote JF-Expert Member

  #16
  Oct 21, 2012
  Joined: Aug 4, 2010
  Messages: 8,352
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 0

  baada ya kuminywa korodani ameeleza ukweli mzima. chezea koleo wewe...
   
 17. H1N1

  H1N1 JF-Expert Member

  #17
  Oct 21, 2012
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 4,201
  Likes Received: 528
  Trophy Points: 280
  Unaamini wana uwezo wa kufikiri kwa uhuru wa kibinadam kama wako ? 'they are totally brain washed'
   
 18. Cathode Rays

  Cathode Rays JF-Expert Member

  #18
  Oct 21, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 1,736
  Likes Received: 182
  Trophy Points: 160
  Neno moja tu linatosha ..."INCREDIBLE"
   
 19. Pakawa

  Pakawa JF-Expert Member

  #19
  Oct 21, 2012
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,741
  Likes Received: 3,178
  Trophy Points: 280
  Wajinga ndio waliwao..wale walioandamana na kuvunja amani sasa watajua kuwa kiongozi wao ni muhuni anataka Watanzania tuingie kwenye vita ya kidini. Serikali ina kila sababu ya kumfungulia mashtaka huyu g.....
   
 20. takashi

  takashi JF-Expert Member

  #20
  Oct 21, 2012
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 909
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Sheikh Farid sio mara ya kwanza kutekwa, na kila aliyetekwa si lazima ang'olewe kucha...inategemea na mazingira...Chuki yako dhidi ya Sheikh Farid ndio inayokufanya uamini hivyo.
   
Loading...