Polisi Z`bar wayapiga stop maandamano ya waumini wa Kanisa la Anglikana dayosis Z'bar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Polisi Z`bar wayapiga stop maandamano ya waumini wa Kanisa la Anglikana dayosis Z'bar

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by papason, Dec 30, 2010.

 1. papason

  papason JF-Expert Member

  #1
  Dec 30, 2010
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 2,317
  Likes Received: 634
  Trophy Points: 280
  Polisi Z`bar wayapiga stop maandamano ya waumini


  Na Mwinyi Sadallah


  30th December 2010

  Jeshi la Polisi Zanzibar wamezuia maandamano ya kupinga kuvamiwa kwa zaidi ya ekari 10, mali ya Kanisa la Anglikana dayosisi ya Zanzibar.

  Waandamanaji walisema jana kuwa maandamano hayo yalipangwa kufanyika Jumapili ijayo baada ya misa ya asubuhi kuanzia katika Kanisa la Mkunazini na kumalizikia Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Magharibi.

  Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibu, Azizi Juma alisema: “Tumezuia maandamano kwa sababu wanayempelekea malalamiko hafanyikazi Jumapili.”

  Alisema kwa vile ambaye angeyapokea maandamano hayo na kusikiliza malalamiko atakuwa hayupo hivyo hakuna sababu ya waumini hao kuandamana.

  “Tulichofanya ni kutoa ushauri kwa waumini kupeleka malalamiko kimya
  kimya siku ya kazi,” alisema Juma.

  Katibu Mkuu wa Kanisa hilo, Nuhu Salanya, alisema waumini wameamua kuandamana baada ya sehemu ya eneo la kanisa huko Mbweni, Mfuuni kuvamiwa bila ridhaa yao.

  Alisema eneo hilo limevamiwa na mtoto wa Rais mstaafu, wa Zanzibar Amani Abeid Karume na tayari ujenzi umeanza kufanyika katika eneo hilo tangu juzi.

  Alisema ombi la waumini kutaka kuandamana kupinga uvamizi huo limepelekwa polisi kwa taarifa ili watoe ulinzi wa kufanikisha maandamano hayo kufanyika kwa amani.

  Kwa mujibu wa Salanya, kanisa hilo lilinunua eneo hilo kabla ya Mapinduzi ya mwaka 1964 likitumika kama shamba baada tu kusitishwa kwa biashara ya utumwa.

  Alisema sehemu moja ya eneo hilo ilitengwa kwa matumizi ya makaburi na sehemu nyingine ilitengwa kwa ajili ya maendeleo ya huduma za kanisa.

  “Tumeamua kuandamana baada ya kukosa msaada kila tulipopeleka malalamiko yetu serikalini,” alisema na kuongeza kuwa baadhi ya ofisi zilizopelekewa malalamiko hayo ni pamoja na Wizara ya Ardhi na Ikulu wakati wa serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Amani Abeid Karume.

  Alisema iwapo ujenzi utaendelea kufanyika, waumini watazidi kuamini kuwa malalamiko yao yamepuuzwa na watakachofanya ni kubomoa.

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Makazi, Ardhi, Maji na Nishati hakupatikana kutoa ufafanuzi.  CHANZO: NIPASHE
   
 2. papason

  papason JF-Expert Member

  #2
  Dec 30, 2010
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 2,317
  Likes Received: 634
  Trophy Points: 280
  Hii haikubaliki kabisaa, tena apa inaonekana kuna njama za makusudi kabisa huko visiwani ya kudhofisha Makanisa!
   
 3. N

  Nonda JF-Expert Member

  #3
  Dec 30, 2010
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Mkuu,
  Anayeona, anayehisi hafanyiwi haki basi anawajibu wa kulalamika na kudai haki yake.
  Lakini kusema kuna njama za kudhoofisha makanisa visiwani halina mashiko.

  Umeshawahi kufika huko visiwani?


  Mimi nimeshatembelea huko na kujionea mwenyewe kuwa makanisa yamejengwa na yameongezeka kila sehemu wanayoishi wakristo.

  Kumbuka Zanzibar inasemwa ni 90% muslims.

  Usifikiri tu,usidhanie tu wala usikubali kupotoshwa.
  Usishabikie migogoro ya kidini, kusanya facts. Unless unazungumzia kiushabiki hapo sawa.

  Haya malumbano ya dini na udini yanakuwa fashion sasa humu JF.
   
 4. m

  muh Member

  #4
  Dec 30, 2010
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jipeni moyo mtashida, Mungu akiwa upade wenu ni nani aliye juu yenu?
   
 5. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #5
  Dec 30, 2010
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Njia za kistarabu za kutafuta haki zikishindikana mtu anaenda mahakamani, huko ndiko anaweza kuomba kizuizi cha kusimamisha ujenzi. Kwanini kanisa hilo mpaka sasa halijaona umuimu wa kufikisha suala lao mahakamani?
   
 6. Higash

  Higash JF-Expert Member

  #6
  Dec 30, 2010
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 844
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 45
  ufisadi mpaka kwenye mali ya kanisa!!
   
 7. N

  Nonda JF-Expert Member

  #7
  Dec 30, 2010
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Papason,

  Huo ukoo wa Karume huko Zenj wanachukua kila sehemu wanayoitaka. Kama unamjua mzenj yeyote au mwandishi anayefanyia kazi huko muulize akupe story za huko za huu ukoo wa Karume.
  Hawana tofauti na CCM huku bara, wanajichukulia kila tu...kumba kumba Ltd!!!
  If you like call it fisadi!!
   
 8. M

  Mtwike Senior Member

  #8
  Dec 30, 2010
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 116
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hivi kanisa halijui kuwa ardhi yote baada ya mapinduzi imetaifishwa?! si Babu Karume aliyetaifisha ardhi za Wakfu za Waislamu? lakini ardhi yenyewe siyo waliopewa na Masultani? Agustino keshastaafu, si afunguwe kesi ya madai. tunaomba wenye data visiwani!
   
 9. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #9
  Dec 30, 2010
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Kadhia ya uvamizi wa maeneo ya Kanisa la Anglikan hapo kisiwani yapo muda mrefu! Ilifika mahala hadi marehemu askofu Douglas Toto kumkemea rais wa visiwa hivyo.
   
 10. The Dreamer

  The Dreamer JF-Expert Member

  #10
  Dec 30, 2010
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 1,280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Rafiki yangu kumbe wakati mwingine unakuwa rational? Ubarikiwe
   
 11. N

  Nancy Tweed Senior Member

  #11
  Dec 30, 2010
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 123
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ninavyoelewa mimi Anglican Church maana yake ni Church of England. Kwa kiswahili sanifu ni Kanisa la Waingereza. Sasa kwanini waingereza waruhusiwe kumiliki ardhi ya Zanzibar?
   
 12. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #12
  Dec 30, 2010
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Kwa ufahamu wako nini maana ya kumiliki ardhi?
   
 13. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #13
  Dec 30, 2010
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Mashamba yote yalishataifishwa na Karume Sr., ikiwa hilo lilikuwepo kabla 1964, wasahau!
   
 14. c

  charityboy Senior Member

  #14
  Dec 30, 2010
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  watulie huko znz, wakianza kuleta mambo ya bara katika ardhi ya watu watakosa kila kitu. Wao wapo below 1% sasa watulie wasitafute kujenga hojakama wanaonewa kwa sababu wakristo. SMZ imekuwa mstari wa mbele kutoa haki kwa makanisa. Huo ni ujanja wa makanisa kuvuruga nchi.
   
 15. K

  Kizibao JF-Expert Member

  #15
  Dec 30, 2010
  Joined: Aug 24, 2010
  Messages: 739
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 80
  Muh hilo la kushinda na kupewa tena ardhi hiyo wasahau... kwani kama walivyosema wadau hapo ardhi yote ilitaifishwa na kuwa ni mali ya serikali na siyo ardhi tu mpaka majumba ambayo mengine hivi sasa ni maeneo ya serikali na ardhi nyingi sana ilikatwa eka 3 na kupewa wale wasikuwa na ardhi kwa masharti hawaruhusiwi kuiuza... sasa kama kanisa likitaka kurejeshewa ardhi yake na wakarejeshewa basi na wale wote waliotaifishwa maliza zao wanatakiwa kurejeshewa na wana legitimate reasons ya kurejeshewa. na hiyo hitoawaathiri wananchi wa kawaida tu kwani katibu 40% au zaidi ya ardhi iliyotaifishwa wamepewa masikini kwa kuendesha kilimo na vile vile ofisi nyingi sana za serikali inaabidi sihamishiwe sehemu nyengine kwa serikali kujenga majengo mapya kwani ofisi za sasa hivi ziko kwenye majumba yaliyoptaifishwa...Na kitu cha kushangaza kwa nini waamuwe kuandamana siku isiyo ya kazi wakati wanaompelekea malalamiko yao ni mkuu wa mkoa na siku hiyo hayuko kazini....there is something smelling here... baada ya kuona majumba yamefujwa juzi wakahisi na issue yao itasikilizwa na itapata attension ya media kama wakiandamana sasa hivi kwa ni dharihi walifanya bila ya kufikiria...nataka watu wa JF kuna watu kibao ZNZ wanaenda na nyaraka zao halali erikali kila leo kutaka warudishie mali zao na hujasikia kuandamana.....Na sifikirii ya kuwa SMZ itafanya kosa la kuirudisha hiyo ardhi kwa ZNZ kutakuwa hakukaliki...
   
 16. M

  Mtwike Senior Member

  #16
  Dec 30, 2010
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 116
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Waislamu ni kosa lenu, mmezubaa, wakristo japo ni wachache, lakini wameamka! hamjapata kulalamika, lisha kuandamana! mmevunjiwa miskiti (mabuluu) na karume, mmefanya nini?
   
 17. c

  charityboy Senior Member

  #17
  Dec 30, 2010
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  MS nakutakia kila lakheri katika Phd yako. Usinisahau. Ukirudi niletee utaalamu wa e-agriculture. Mimi ni mkulima kama pinda, sio mvivu kama vijana wengi siku hizi
   
 18. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #18
  Dec 30, 2010
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Sipendi kukujibu, ila nafanya hivi kwa kumbukumbu za baadae. Ardhi ni mali ya serikali kwa mjibu wa sheria ya ardhi ya mwaka 1985(SMZ). Hii ina maana kuwa serikali ndio yenye wajibu wa kupima na kugawa ardhi visiwani hapo.

  Kiwanja cha kanisa huko Mbweni kilishapimwa na kumilikishwa kwa kanisa hilo, na iwapo atatokea mtu mwingine yoyote kuendeleza eneo hilo ni wazi kuwa atakuwa ni mvamizi. Hivyo basi ni jukumu la kanisa kuona kuwa eneo lao halivamiwi.
   
 19. K

  Kizibao JF-Expert Member

  #19
  Dec 30, 2010
  Joined: Aug 24, 2010
  Messages: 739
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 80
  Kijana unaonesha hichi kitu huna uhakika nacho...Katika madai yao walisema ya kuwa kiwanja walikinunua hata kabla ya mapinduzi na hakuna ushahidi wowote baada ya mapinduzi kiwanja hicho kilipimwa tena na kumilikishwa wao!na sifikirii kama SMZ itafanya kosa kama hilo, ninachoomba kuwa na ushahidi kwanza ndiyo unazungumza kitu.....
   
 20. C

  CHE GUEVARA2 Member

  #20
  Dec 31, 2010
  Joined: Aug 16, 2010
  Messages: 33
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hayati Abeid karume alitaifisha ardhi zote za mkoloni baada ya mapinduzi inawezekana kuwa hiyo Ardhi wanaosema kuwa ni yao Kanisa la Anglikana walipatiwa na Wakoloni sio!!
  Kibunango kawambie babu zako wasiweke nia na matumaini ya kupewa hiyo Ardhi kitu hicho wasahau kabisa!!!!
  any way Zanzibar ni nchi ya Waislamu 99% ya raia wake ni Waislam.....Makanisa yaliyojengwa yanatosha kwa Wageni waliopo zanzibar...Wa Zanzibar hawataki tena kujengwa Makanisa katika nchi yao kwa sababu hayana faida yeyote kwa taifa lao na watu wao!!!!!:painkiller:
   
Loading...