Polisi yazuia Operation Sangara ya CHADEMA Morogoro kisa hakuna Askari

Sioni ajabu serikali ikipeleka suala la kuzuia mikutano ya CHADEMA mahakamani kisha wakatumia kama kisingizio kuwa suala la mikutano lipo mahakamani so hairuhusiwi mpaka kesi itakapomalizika 2016.
 
Wapuuzi wakubwa na hao viongozi wao,eti watailazimisha chadema kutii sheria,hivi chadema wanavunja sheria ipi wakifanya mikutano???
Wanaziba jua kwa mfuko wa plastik ngoja uwayeyukie,maana njinsi wanavyozua mikutano ndivyo imani inavyoongezeka kwa watz.

Long live cdm!!!!!!
 
Hii ni Tanzania zaidi ya uijuavyo, wamalawi wako busy wanataka kutupiga, sisi tunahangaika na chadema

Very true indeed! Malawi wameshatudharau hata wako tayari kuzichapa na sisi afu sisi tunapeleka askari kuwadhibiti watawala halali wa kesho! Funny!
 
Habari wakuu!
Ikiwa yamebakia almost masaa 5 kabla ya kuanzia mkutano mkubwa wa CHADEMA chini ya M4C na viongozi wa kitaifa Mbowe, Dr.slaa etc,
Asubuhi leo polisi(FFFU) wengi wakiwa kwenye magari yao yenye bendera nyekundu, wameanza operation maalum ya kupita kila kona ya mji ili kutisha watu wasihudhurie ktk mkutano huo wa CDM.

MY OUTLOOK :
kazi ya dola kusupress upinzan nchii yaanza kazi rasmi, Tusiogope tusonge mbele wana CHADEMA.
"the thing that we have to fear, its only fear"

FEAR NOT.
Mbona walisema hawana polisi wa kutosha kufanya ulinzi katika mkutano wa chadema na hao wametoka wapi?
 
Polisi katika manispaa ya mji wa Morogoro wamezuia operation sangara ya CHADEMA kwa sababu za kuwa hakuna askari wa kutosha kusimamia mikutano yao katika mkoa wa Morogoro.

Lakini pamoja na makatazo hayo CDM wamedai wao wataendelea na mikutano yao kama kawaida kwa sababu haisuani na fujo wala vurugu na siku zote Polisi huwa hawawasaidii kwa lolote.

Concern

Jeshi la PolisiCCM liko kwa ajili ya kuzuia CDM sio kulinda

Mkuu Hivi sababu ni kutokuwepo kwa polisi wa kulinda amani au CCM nao wana mkutano?
 
Saa ya ukombozi yaja. ukiwa morogoro leo unaweza ukashangaa kila round about kuna defender ya polisi.
 
Polisi katika manispaa ya mji wa Morogoro wamezuia operation sangara ya CHADEMA kwa sababu za kuwa hakuna askari wa kutosha kusimamia mikutano yao katika mkoa wa Morogoro.

Lakini pamoja na makatazo hayo CDM wamedai wao wataendelea na mikutano yao kama kawaida kwa sababu haisuani na fujo wala vurugu na siku zote Polisi huwa hawawasaidii kwa lolote.

Concern

Jeshi la PolisiCCM liko kwa ajili ya kuzuia CDM sio kulinda

Mkuu Hivi sababu ni kutokuwepo kwa polisi wa kulinda amani au CCM nao wana mkutano?
 
Wana JF.
Kulikuwa na taarifa kuwa M4C ipo Morogoro leo ingawa taarifa za Polisi zilionesha kuwepo zuio la harakati za M4C hapo morogoro. Ninaomba kama kuna mwenye taarifa mpya atu-update.
 
Kwa wale mliopo moro tunaomba mtutupie up dates juu ya kinachoendelea kuhusiana na mkutano wa CHADEMA.
 
Kwa wale mliopo moro tunaomba mtutupie up dates juu ya kinachoendelea kuhusiana na mkutano wa CHADEMA.

Wakuu mpaka sasa naona magari ya M4C yanaranda randa tu barabarani,polisi nao wamejaa kwa wingi mno ila hawasumbuki nayo kabisa,bado hatujajua hatima ya mkutano,ila nimeongea na baadhi ya askari wengi kama si wote ni pro Cdm,hawakubaliani na sababu zilizotolewa na ma boss wao kuzuia juu ya mkutano,wanakiri kua ni amri toka serikalini na wala si muingiliano wa mikutano kati ya cdm na c.c.m kama walivyodai,wanasema dola inaogopa sana sumu zinazotemwa kwenye operesheni sangara,ni wazi c.c.m inaelekea ukingoni!!Moro ilikua ngome ya c.c.m,sasa hawaamini kua Moro nayo inawageuka sasa,ndio maana wanatumia nguvu kubwa kwa uoga wao!
 
Kwa taarifa kamili:
ilibidi kamanda wa polisi ampigie Mbowe simu ili kuwakataza vijana wa CDM waliokuwa wamejaa sana ktk ofisi za CDM za hapa moro, makundi makubwa ya vijana yaliendelea kujaa sana tayar kwa maandamano lakini walikuja viongozi wa CDM Benson kigaila, Rwakatare na mwita waitara wakatangaza kusitisha mkutano wake na badala yake utafanyika tarh 18 na hii imetokana na polisi kuwaplease sana viongzoi wa CDM kwani hali ilikuwa tete sana japo asubuhi 2.
Lakini kiukweli hapa Moro kuna mwamko mkubwa sana na hii ndio image nzima ya anguko la CCM mkoani hapa.

Mkuu hao vijana kwani na wao wameletwa na mafuso kama wale wa chama tarajiwa cha upinzani?
 
Wana JF.
Kulikuwa na taarifa kuwa M4C ipo Morogoro leo ingawa taarifa za Polisi zilionesha kuwepo zuio la harakati za M4C hapo morogoro. Ninaomba kama kuna mwenye taarifa mpya atu-update.

sasa unaanzisha thread ya nn wakati hujui chochote??acha kukurupuka!
 
Tunapenda tu kupata habari je hizo taarifa unazozitaka utazifanyia kazi kweli?au ukasimulie bar na sehemu nyinginezo tu utazani ulikuwepo eneo la tukio haisadii hiyo!!jamani
 
Nipo Moro kwakweli polisi ni kila kona na inaonekana kama polisi wanaweza zuia kwani hapa nipo maeneo ya Masika Wale jamaa wa kutuliza ghasia wamejaa maenneo ya B one Jirani na Bank ya CRDB lakini hakika muamko ni mkubwa sana wa watu kutaka mkutano ufanyike. Kila Mtu maeneo ya katikati ya mji analaani vikali mpango mzimwa wa kuzima mkutano wa leo. Hapa nataka kurudi tena viwanja vitakavyofanyika mkutano maana mpaka saa saba na nusu mchana kulikuwa bado hakujaeleweka ila nasi tunawajuza yatakayojiri huku mji kasoro bahari
 
Kwataarifa Rasmi mikutano ya chadema imeahirishwa, mpaka tarehe 08 nasiyo tarehe 18 Na hii nikutokana na viongozi wa juu wa chama pamoja na viongozi wa juu wa police kujadiliana, na ziara hii itaanzia ifakara.

Sasa huyo Shilogile si alisema anazuia kwasababu ya nane nane, je 08.08 si ndiyo siku yenyewe au lengo lao ni kuwagawa kuwa wengine waende nane nane na wengine waende kwenye mkutano wa chadema na hapo watakuwa wamefanikiwa malengo yake....
 
Taarifa rasmi kutoka kwa kamanda wangu aliyeko Morogoro ni kwamba polisi wamesalimu amri na wamekubali M4C ianze wiki ijayo tarehe 08
 
Back
Top Bottom