Polisi yazuia mtoto wa shule kuolewa mfanyabiashara | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Polisi yazuia mtoto wa shule kuolewa mfanyabiashara

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Mar 6, 2010.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Mar 6, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 36,011
  Likes Received: 6,826
  Trophy Points: 280
  Polisi yazuia mtoto kuoa mwanamke

  [​IMG]
  JESHI la Polisi nchini, limezuia kufungwa ndoa ya mwanafunzi wa kidato cha tatu Hasira Seif (17) wa Shule ya Sekondari Uhuru Mchanganyiko jijini Dar es Salaam.
  Akizungumzia sakata hilo jana, Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, alisema mwanafunzi huyo alitaka kufunga ndoa juzi na Hillary Salum (29), ambaye ni mfanyabiashara wa jijini lakini askari wakafanikiwa kuizuia.
  “Tumefanikiwa kuzuia ndoa ya mwanafunzi wa kidato cha tatu wa Shule ya Sekondari Uhuru Mchanganyiko lakini sitatolea maelezo zaidi hadi Jumatatu, napitia kwanza vifungu vya sheria kwa sababu vinakinzana.
  “Nawasiliana na wanasheria wakati na mimi nikiisoma sheria ya ndoa kwa umakini ili kujua kama ndoa ile ilikuwa kinyume cha sheria na haki za watoto,” alisema Kamanda Kova alipozungumza na Tanzania Daima na kuongeza kwamba ndoa ya mwanafunzi huyo ilikuwa ifanyike juzi.
  Wakati huo huo, askari polisi usiku wa kuamkia jana walifanikiwa kuwatia mbaroni watuhumiwa sita wa ujambazi wanaodaiwa kufanya uhalifu kwenye makao makuu ya Kampuni ya Simu ya Sasatel na vituo viwili vya mafuta.
  Katika hilo, Kamanda Kova alisema watuhumiwa hao wamekutwa na mitungi miwili ya gesi, aina tofauti ya funguo bandia zipatazo 73, mitalimbo minne, washeli 12, kisu kimoja, koleo mbili, plasta kubwa moja na festa ya umeme.
  Alisema majina ya watuhumiwa hao yamehifadhiwa kwa sababu za kiusalama, kwa kuwa polisi wanaendelea kuwatafuta watuhumiwa wengine.
  “Hawa watu sita walikamatwa kutokana na operesheni ya polisi ya kudhibiti uhalifu inayoendelea jijini, wanadaiwa kuiba kwenye Kampuni ya Sasatel makao makuu, kituo cha mafuta GAPCO cha Kunduchi Mtongani na GAPCO Oysterbay. “Tutawashikilia na kuwahoji hadi tutakapowapata watuhumiwa wengine wa ujambazi huu, kwa sababu wanaendelea kutajana. Ni watu hatari sana hawa, hivi vitu walivyokutwa navyo ni mabomu, haya yanaweza kulipuka,” alisisitiza Kamanda Kova, aliyedai kuwa watafikishwa mahakamani pindi upelelezi utakapokamilika. Aidha, jeshi hilo limefanikiwa kukamata bangi na gongo katika msako huo vikiwa vimefungwa kwa namna tofauti na kusema polisi wamo kazini muda wote, ili kuhakikisha hadi tunafika kwenye kipindi cha Uchaguzi Mkuu, matukio ya uhalifu yawe yamepungua.


  [​IMG]


   
 2. Maria Roza

  Maria Roza JF-Expert Member

  #2
  Mar 6, 2010
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 6,776
  Likes Received: 110
  Trophy Points: 160
  Hivi sheria inaruhusu kutaja jina la mtu kabla ya kufikisha miaka 18?? naomba msaada kwa wanasheria plz??
   
 3. Fisherscom

  Fisherscom JF-Expert Member

  #3
  Mar 6, 2010
  Joined: Mar 13, 2008
  Messages: 1,478
  Likes Received: 278
  Trophy Points: 180
  Angalau polisi wameweza kuliona hilo,yapo mengi mitaani kama hayo yanatokea. Nadhani polisi jamii inahitaji nguvu zaidi.
   
 4. RayB

  RayB JF-Expert Member

  #4
  Mar 6, 2010
  Joined: Nov 27, 2009
  Messages: 2,754
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Nieleweshe hapo kwenye bold ni mtoto mwenyewe ndo alitaka kuolewa au?
   
 5. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #5
  Mar 6, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,378
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  wanatimiza maagizo ya ilani ya taasisi ya ISLAMU, si hata mhammadi alifanya hivyo? mi naona polisi imevuka mpaka, lakini ni mtazamo tu,
   
 6. Mazingira

  Mazingira JF-Expert Member

  #6
  Mar 7, 2010
  Joined: May 31, 2009
  Messages: 1,837
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Uislamu ni mzigo mzito katika ulimwengu huu. Wanaiga alichokuwa anafanya Mwamedi mtume wao maana alikuwa dume la mbegu. mmmmh!
   
 7. Hassani

  Hassani JF-Expert Member

  #7
  Mar 7, 2010
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 276
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  Hakuna kizuizi chochote,kinachomzuia Kova kutaja majina ya hao watu kwenye viombo vya habari.Especial wakati huu kesi bado haijafika mahakamani.
   
 8. Mbogela

  Mbogela JF-Expert Member

  #8
  Mar 7, 2010
  Joined: Jan 28, 2008
  Messages: 1,371
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Sheria ya ndoa ya mwaka 1978 ilikataa mtoto aliyechini ya miaka 18 kuolewa kwa namna yoyote ile, lakini miaka ya 90 (wakati huo akina Kitwana Kondo wakiwa kwenye ligi) sheria hiyo ilirekebishwa 1. Ilishusha umri wa mtoto wa kike kuolewa kwa hiari bila ridhaa ya wazazi kutoka miaka 21 mpaka miaka 18, 2. Inaruhusu mtoto wa kike aliye na miaka 16 kuolewa ili mradi tu wazazi wake wameridhia.

  Kwa kesi hii unaona huyo mtoto anavuka miaka 16 kwa hiyo kama wazazi wake waliridhia basi hakuna kosa hapo, si kwa muolewaji wala muoaji. Inakuwaje kamanda mzima kama Kova ndio anasoma sheria leo wakati jeshi tayari limeshaingilia kati arusi ya watu? Kama itaonekana hakutenda kosa (hakuna kifungu cha sheria cha kumbana) Je Polisi na serikali watawajibika kulipa gharama walizoingia maharusi pamoja na personal damage waliowasababishia kwa jamii? Arusi haikuwa ajenti kiasi hicho lazima walisikia fununu mapema angeweza kwenda kujikumbusha sheria inasemaje kabla hajafanya arrest.

  Sheria ya shule haiwa-include watoto wa sekondari, kama ambavyo sheria ya kusoma shule kwa lazima inawacover watoto wa shule za msingi tu ndivyo ambavyo sheria ya mimba, ndoa inavyowaacha waototo wa shule za sekondari nje.

  watu wengi siku hizi tunafanyia kazi matamko ya viongozi wetu na matamko ya kampeni za wanaharakati na NGO kwenye kampeni zao kama za akina "Fataki" kama sheria. watu wakisikia JK akisema waokoeni watoto wa shule wasiolewe akina kova badala ya kukaa chini wakatafuata kipengere cha sheria chakusimamia kutekeleza agizo la bosi wao wanapweteka na kuanza kukamata kamata watu bila kijiridhisha kama kuna sheria ya kutosha kucover hilo kosa. Kuna udhaifu mkubwa sana wa sheria kwenye eneo hili.

  Sheria ya Makosa ya kujamiiana ya mwaka 1997 ilijaribu kiasi fulani kuaddress hizi issues lakini watungaji wa ile sheria na wanaharakati wa wakati ule walijaribu sana kumlinda mwanamke aliyeolewa na mwanamke mtu mzima anayevutia kwa macho mbele ya mwanamme ( si ndio zile sheria za kukonyeza zikawekwa humo). Kwa hiyo nayo iliacha mianya juu ya watoto hasa wa sekondari na vyuo (mfano vyuo vya walimu ni bado watoto sana wengi wanamaliza F.IV wakiwa na miaka 16 anakuwa chuoni akiwa na miaka chini ya 18) wanapaswa kulindwa na sheria
   
 9. Ruge Opinion

  Ruge Opinion JF-Expert Member

  #9
  Mar 8, 2010
  Joined: Mar 22, 2006
  Messages: 1,734
  Likes Received: 336
  Trophy Points: 180
  Kumbe kama hakuna uchaguzi polisi inakuwa usingizini? That explains it. For once Kova has said the truth.
   
 10. B

  Bao3 JF-Expert Member

  #10
  Mar 8, 2010
  Joined: Aug 7, 2009
  Messages: 318
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Hahaha msamehe bure, jamaa hakumaanisha inaonekana ni tatizo la communication skills in the sense that "he doesn't know what to talk,where and in what manner". Wenzetu wazungu hapo wangesema jamaa ame"flip-flop"!
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...