Polisi yazuia maandamano ya 'kuunga mkono hotuba ya JK' Dar

Ningeshangaa kama yangefanyika hayo maandamano. Nani aandamane, wenyewe kwa wenyewe wananyoosheana kidole na kueleza waziwazi kuwa Kikwete hajafanya lolote, sasa waandamane kwa lipi?

Au wangeandamana kutaka ajibu hoja za chadema, apunguze bei ya sukari, aongeze mishahara ya wafanyakazi n.k.
 
Ukweli wenyewe Polisi hawawezi kuzia maandamano ya Chadema yajao kwa sababu hakuna sababu za msingi,kama hii ndio gia wanaingiza ili waje wakatae basi nadhani ni wrong gear
 
ni sawa kuyazuia maana hicho kikundi zidhani kama kina usajili wowote. na kama wangeruhusu vingejitokeza vikundi vingi vyenye majina mbalimbali na sababu mbalimbali. kama ni maandamano ya chama fulani sawa na ijulikane ni chama gani. maana kusema kikundi cha wapenda amani haitoshi.
 
HAPANA!!!!!!!!! NASEMA HAPANA! hiii ni janja ya CCM na POLISI, wanawatega CHADEMA siku wakiomba wataambia sababu kama hizi!

Wajanja tumestukaaa!

Hawana lolote
 
Changa la Macho ilo,yaan bado wana2chukulia mafalaaaaaaaaaa waonyeshn kwa vtendo 2mekuwa na 2najua 2nachotaka na 2na uwezo wa kvtendo kukpata kvyovyote.

Aibu yao hio
 
1. HUO NI MPANGO WA KUJA KUZUIA MAANDAMANO YA CHADEMA!
2. SISIEM WAMESTUKIA KUWA HAYATAPATA SUPPORT i.e WATU HAWATA JITOKEZA.
3. WAMEOGOPA AIBU!

CHAKACHUA NI CHAKACHUEEEEEEEEEEEEEEEEE!
 
Hakika wamekimbia aibu hawa watu thus why wameyasimamisha haya maandamano,polisi ni wao kamwe hawezi kuwazuia coz wameona watapata aibu na watu kuwazomea mjini.

Aibu yao aibu yetu.............aibu yao wenyewe
 
Naomaba ushahidi wa maandishi wa Polisi kwamba wamezuia, Nakubaliana na wale wanaosema wastuka baada yakuona vijana hawatakuja kuandamana hata wakipewa rushwa ili waandamane na pia ni njia ya kujenga hoja ya kuja kuzuia maandamano ya Chadema, Chadema andaane maandamano JPili huwa hakuna foleni kubwa tuone janja yao.
 
Mengi tutasikia na kuyana, mpaka miaka mitano iishe! Naamini kuna watu huko ndani ya system wanatamani mwaka uwe ni siku moja ili watue zigo
 
Kuna sababu kuu mbili zimetumika kuyazuiya:
1.Waandaaji wameona ayaungwi mkono na wazarendo.

2. Ni njia ya kuyazuiya maadamano ya CHADEMA ya hapa dar kwa kuwa na ya UVCCM YALIZUIWA kwa hiyo ndo njia imetumika.

3. NI MISINTELLIGENCE ya polisi imegundua.
 
Hili ni wazi ni mpango wa dhati wa kuzui maandamano ya CDM. Na siku itakapo fika ya watu wa ukweli kuandamana watadai ni foleni.

Hii wana CDM ni wazi watafanya mpango kutuzuia.

Tujipange!
 
nilitaka waandamane tuwaone, then tujibu mapigo kwa kuandamana hapa DSM tuone who is who!!! wamekwepa aibu.eti kumpongeza jk..te te te !!!! poleni.
 
Yale Maandamano yaliyokuwa yafanyike leo kuunga mkono Hotuba ya JK yamezuiwa na Polisi kwa madai kuwa yatasababisha msongamano kwenye barabara watakazopita.

Nauliza:
Polisi/CCM wameshtukia nini?
Je! Ni ujanja wa kuja kuzuia maandamano yenye tija kutoka Chadema kwa sababu hiyo hiyo?

Kapotolo ni kama ulikuwa ubongoni mwangu............. tumewaza kitu sawa sawa. I second thinking yako mkuu
 
Ukweli uko wazi, waandamanaji walikuwa wanapeleka viwiliwili na si mioyo yao, mioyo na hisia zao zote wamezielekeza katika maandamano ya kupunguza umaskini na bei za bidhaa kuw juu.

Polisi wangewaruhusu wala hata wasingesumbuka na kuwapa ulinzi, wangejitokeza vijana wachache mno na ingekuwa ni aibu kubwa kwa waandaaji.
 
Kapotolo ni kama ulikuwa ubongoni mwangu............. tumewaza kitu sawa sawa. I second thinking yako mkuu

Mkuu hapo kwenye RED kama kuna kamusi mpya yenye maneno mapya imetoka naomba tujulishane otherwise hapo mimi naona chenga tu.
 
hakuna watu waliokuwepo kuandamana..... so ilikuwa ni aibu kusema kuna maandamano wakati kusingetokea watu.

nani hapa DSM angeenda kushiriki maandamano ya CCM... huo ni UCHURO tu.... ni kama bundi kulia juu ya bati la nyumba yako.
 
sijajua lengo la polisi kuwazuia, lakini hakukua na sababu yoyote ya maandamano kwa watu wenye akili timamu, kwani jk ameshatoa hotuba ngapi? kwa nini hawakuandamana, kuziunga mkono?. ccm waachane na uchapwa wa kufikiri, kwani hotuba ya raisi wao haukuwa na kitu cha muhimu, zaidi ulivyzwa na uoga dhidi ya hoja za cdm pamoja na uvivu wa fikra kutoka kwa namba moja wetu.
 
Toka lini wakaandamana hawa? Si hukutana pale Diamond na kutoa kauli za mbayuwayu?Lbda sasa hawana hela ya kulipia ukumbi...
 
Yale Maandamano yaliyokuwa yafanyike leo kuunga mkono Hotuba ya JK yamezuiwa na Polisi kwa madai kuwa yatasababisha msongamano kwenye barabara watakazopita.

Nauliza:
Polisi/CCM wameshtukia nini?
Je! Ni ujanja wa kuja kuzuia maandamano yenye tija kutoka Chadema kwa sababu hiyo hiyo?

Jibu umeshatoa
 
Back
Top Bottom