Polisi yazuia maandamano ya 'kuunga mkono hotuba ya JK' Dar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Polisi yazuia maandamano ya 'kuunga mkono hotuba ya JK' Dar

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kapotolo, Mar 16, 2011.

 1. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #1
  Mar 16, 2011
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Yale Maandamano yaliyokuwa yafanyike leo kuunga mkono Hotuba ya JK yamezuiwa na Polisi kwa madai kuwa yatasababisha msongamano kwenye barabara watakazopita.

  Nauliza:
  Polisi/CCM wameshtukia nini?
  Je! Ni ujanja wa kuja kuzuia maandamano yenye tija kutoka Chadema kwa sababu hiyo hiyo?
   
 2. L

  LAT JF-Expert Member

  #2
  Mar 16, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  maandamano hayo yasingefanikiwa na yangekuwa ni aibu kubwa sana kwa serikali na rais .... hivyo wamepotezea kwa kisababu cha polisi
   
 3. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #3
  Mar 16, 2011
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 722
  Trophy Points: 280
  bahat yao hawakufanya......ngoja nikategue .........
   
 4. Joseph

  Joseph JF-Expert Member

  #4
  Mar 16, 2011
  Joined: Aug 3, 2007
  Messages: 3,527
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Walikuwa wapi siku zote kuandamana mpaka waje na wazo hilo leo? Tangu JK atoe hotuba ni muda mrefu sana hata hivyo hotuba yenyewe haina tija kwa taifa zaidi ya kueleza vitu visivyotekelezeka.

  Polisi wangewaacha tu waandamane tuone nguvu yao ipo wapi kama si kukodi watu kwa kuwalipa ili waandamane.
   
 5. L

  Leonard Mwanja Member

  #5
  Mar 16, 2011
  Joined: Jan 8, 2010
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Hayana tija afadhali yamezuiwa.Tumechoka na maadamano ya kupongezana ujinga na kupoteza muda tu hongera polisi kwa kuona hilo
   
 6. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #6
  Mar 16, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  sababu za kiintellejesia teh! wamesitisha wakitaka kutuhadaa wapo nyutro kwa vyama vyote!
   
 7. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #7
  Mar 16, 2011
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,856
  Likes Received: 2,432
  Trophy Points: 280
  ccm walitaka KUKWEA MNAZI NA MSULI!
   
 8. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #8
  Mar 16, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,791
  Likes Received: 2,399
  Trophy Points: 280
  ya kwetu CDM tutafanya usiku hakuna msongamano.yataanzia manzese,mbagala,bunju,kibamba,kigamboni mpaka karimjee!jk akiamka asubuhi akute tupo tayari ikulu
   
 9. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #9
  Mar 16, 2011
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,856
  Likes Received: 2,432
  Trophy Points: 280
  tunaomba wawaachie waanamane kama ni foleni waanzie magomeni to mazense ikishindikana hataa wafanye public rally, tunataka kuwaona maadui wa umma kwa sura zao
   
 10. Kurunzi

  Kurunzi JF-Expert Member

  #10
  Mar 16, 2011
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 4,006
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  Wangeachwa waandamane kwani ni haki ya msingi kama tatizo ilikuwa route si wangeshauriana na polisi then wabadilishe route? Na vipi gharama walizotumia?

  Mimi nafikiri kuna namna hapa ikiwa polisi waneweza kuzuia maandamano ya kikundi kisichokuwa na impact kwa sababu nyepesi 2 ya foleni namnagani maandamano ya CDM ambayo yatavuta idadi kubwa ya watu nafikiri pana tatizo.
   
 11. Jembe Ulaya

  Jembe Ulaya JF-Expert Member

  #11
  Mar 16, 2011
  Joined: Oct 27, 2008
  Messages: 456
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wanahofia maandamano ya Chadema. Hivyo siku Chadema wakiomba kibali watakataliwa na kuambiwa hata CCM tuliwakatalia.
   
 12. Konakali

  Konakali JF-Expert Member

  #12
  Mar 16, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 1,508
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Hii ndio wameshtukia........!

  Na hii ndio ilikuwa target yao kwa maslahi yao.......! Shame on them.....!
   
 13. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #13
  Mar 16, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  wameambiwa kuwa hawatapata waandamaji wakakwepa aibu? au huenda Dr. augustine mrema kashtuka, si mnajua yule mzee ni kinyonga? kesharudi loliondo?
   
 14. M

  Marytina JF-Expert Member

  #14
  Mar 16, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,035
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  karudi leo saa nane atakuwa Bahkresa manzese akiwadanganya wajinga.Yeye ndiye main speaker wa huu mkutano wa ccm na wake zake cuf,nccr
   
 15. M

  Marytina JF-Expert Member

  #15
  Mar 16, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,035
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  ila nadhan hayo maandamano kwa upande mwingine yangeongeza chuki dhidi ya serikali so yangeibeba CDM dats why yamepigwa stop.Personaly nlitaka waandamane tena wabebe mabongo yakumsifu JK na Pinda.
   
 16. Smartboy

  Smartboy JF-Expert Member

  #16
  Mar 16, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,110
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Duh! Kweli Jf kuna great thinkers jana kuna mtu alitoa híi kwamba yatazuiliwa na polisi naona yamekosa watu, vijana wamechukua chao af wakaingia mitini.
   
 17. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #17
  Mar 16, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Wajanja hao, wameshtuka! Ingekuwa ni aibu ya karne. Nguvu ya umma ingejibu mapigo ndiyo wangeona cha moto. Kikwete anashindwa kutamka hadharani tu lakini ukweli ni kwamba hana raha na jinsi wananchi walivyomchoka.

  Hata wakitumia propaganda za maandamano ya kuunga mkono hotuba yake haitasaidia kitu kwani hata wanaccm wenzie wamemchoka.
   
 18. Papa D

  Papa D JF-Expert Member

  #18
  Mar 16, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 687
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Vijana wa CCM wameahirisha maandamano ya kumuunga mkono JK baada ya kuzuiliwa na polisi kwa madai kuwa maandamano hayo yatasababisha usumbufu kwa watumia barabara ya morogoro.[Mbona kampeni za uchaguzi hawakuzuia?!!!!!!!!!!].
  Hawa vijana wakamalizia kwa utamu zaidi walipomualika mrema kuwa mgeni rasmi!!
  Kule Kigoma Mbatia na Lipumba wameungana kupambana na CDM. Kwa hayo mapambano ya anga na ardhini kutoka kona zote za nchi, CDM mtatoka?
  CCM WONT SLEEP, CCM WONT EAT, CCM WONT LISTEN AND CCM WONT STOP UNTILL THEY BRING YOU DOWN........... THEY ARE AFTER YOU GUYZ AND YOUR ONLY SURVIVAL IS STOPPING BEING CHASED RATHER CHASE THEM!!!!
   
 19. P

  Paul J Senior Member

  #19
  Mar 16, 2011
  Joined: Oct 25, 2010
  Messages: 193
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Si kwamba maandamano yamezuiliwa ila waandaaji wameshutukia baada ya kuona hawatapata vijana wa kuandamana maana vijana wa kukodisha wangetakiwa kulipwa jana ili leo ndo waandamane, baada ya utafiti ikagundulika vijana walikuwa wanataka hela tu na wasingetokea kwenye maandamano. Kuondoa haibu wakasingizia maandamano kuzuiliwa na polisi kwa sababu ya foleni.

  The route was clear from day one na kama ni kuyazuia sababu ya foleni isingelikuwa ya kushutukiza to that extent! Watanzania wa sasa wameamka, pesa watakula na kuandamana hawataandamana. Kwa mkutano itakuwa hivi ukifika kabla ya kuingia mktanoni unapewa posho na kuesikotiwa ili usitoroke mkutano!

  Aibu tupu
   
 20. S

  SUTU BUTUGURI Member

  #20
  Mar 16, 2011
  Joined: Mar 8, 2011
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hawana jipya hao wanaoitwa 'VIJANA WA CCM'. Kwanza siyo vijana wa CCM, ni vijana wa mafisadi. CCM haipo, ilishakufa. Kilichopo ni genge la mafisadi. Hakuna mtu anayeweza kuandamana kuunga mkono wapambe wa mafisadi halafu akajiita ni 'KIJANA WA CCM YA NYERERE'. Hakuna kitu kama hicho. Wapuuzwe kwani ni watoto wa mafisadi, nao ni mafisadi au ndiyo wako darasani wakifundishwa ufisadi ...
   
Loading...