Polisi yawataka madereva bodaboda Arusha kuwafichua wahalifu

waziri2020

Senior Member
May 31, 2019
190
451
Mwandishi wetu,

Madereva wanaojihusisha na biashara ya kupakia abiria kwa kutumia vyombo vya pikipiki maarufu kama bodaboda wilayani Arusha wametakiwa kuepuka kujihusisha na matukio mbalimbali ya uhalifu kama uporaji wa simu,pochi za wanawake na ubakaji ili kuepuka kuchafua taswira ya biashara hiyo.

Rai hiyo imetolewa jana na mkuu wa kituo cha polisi cha kati jijini Arusha,OCS Shaban Jumbe katika kikao na baadhi ya madereva hao kilichofanyika nje ya ofisi yam mtendaji wa kata ya Engutoto jijini hapa.

Akizungumza na baadhi ya madereva hao OCS Jumbe aliwataka maderava hao kufuata kanuni na sheria wakati wakitekeleza majukumu yao ili kuepuka kuchafua taswira kwamba baadhi yao ni wezi na waporaji.

OCS Jumbe alisema kwamba kumekuwa na baadhi ya matukio ya uhalifu yanayofanywa na baadhi ya madereva na kuwataka madereva hao kuchukua jukumu la kudhibiti vitendo hivyo kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama nchini.

Naye mkuu wa kituo cha polisi cha Engutoto ambaye pia ni mkaguzi msaidizi wa jeshi la polisi wilayani Arusha, Alphonce Kashuku alisema kwamba kiwango cha matukio ya uhalifu katika kata ya Engutoto kimeshuka kutokana na elimu ambayo wamekuwa wakiitoa mara kwa mara kwa madereva hao.

Kashuku,alisema kuwa ushirikiano baina ya jeshi la polisi na madereva hao katika kupeana taarifa ya vitendo vya uhalifu vimesaidia kupunguza matukio ya uhalifu katika kata hiyo huku akiwataka madereva hao kuwafichua wahalifu bila hofu.

“Kiwango cha uhalifu ukiangalia kwa sasa kimeshuka sana katika eneo hili na hii ni kutokana na ushirikiano baina ya polisi na madereva hususani katika kupeana taarifa “alisema Kashuku

Naye Mwenyekiti wa madereva wa bodaboda wilayani Arusha,Okello Costantine alipinga vikali tuhuma za madereva wa bodaboda kuhusishwa na vitendo vya uporaji huku akidai kuwa hao ni baadhi ya waendesha pikipiki wanaochafua taswira ya biashara yao ambayo inawaingizia kipato halali.

“Tuhuma za uporaji sio za kweli unajua kuna madereva wa bodaboda na waendesha pikipiki hawa baadhi yao ndio wanatuchafua sisi hii ni kazi kama kazi nyingine “alidai Okello

Mwisho

05212F02-0004-4A7D-83E3-5B817E7762F0.jpeg


DB5243D0-FA30-4622-9254-67EDF4C6EC47.jpeg


60E2281D-8326-4E26-9A38-14866FF8A473.jpeg


90EF7AA3-EA24-4B11-B7E7-5C4C8A2FE6EB.jpeg
 
Back
Top Bottom