MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,171
- 23,991
Magazeti yanahabarisha, Jeshi la Polisi linawasaka wahariri wa gazeti la Mawio kutokana na habari mbali mbali ambazo wamekuwa wakizichapisha.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Siro alisema wahariri hao wanatafutwa kwa ajiri ya kusaidia uchunguzi unaofanyika kuhusu habari mbali mbali walizokuwa wakiziandika ambazo zina utata.
Kamanda Siro amesema taarifa kamili kuhusu msako wa wahariri wa Mawio itatolewa leo.
Wakati huo huo, Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo, Nape Nnauye amelifungia maisha Gazeti la Mawio kutokana na kushindwa kujirekebisha katika uandishi wa habari ambao unachonganisha jamii, uchochezi na kuhatarisha amani ya wananchi na nchi kwa ujumla.
Hii hatua imekuja baada ya kuandikiwa barua mara nane na msajiri wa Magazeti nchini kuanzia Juni 2013 mpaka January 2016 ya kuwataka wajirekebishe lakini wamekaidi na kudharau.
Uamuzi huu umetolewa kwa mujibu wa sheria ya Magazeti Sura 229, kifungu cha 25(1) na pia kwa mujibu wa sheria ya mawasiliano ya kielektroniki na posta Sura ya 306.
Nape ametolea mfano wa magazeti mengine mengi kama Mwananchi, Mtanzania, Mzalendo ambayo kila yanapokumbushwa wajibu wao na msajiri wa magazeti huchukua jukumu la kujirekebisha.
VIDEO: