Polisi yawakamata wawili kwa mauaji ya Kiongozi wa CHADEMA. Kamanda Mambosasa akataza maandamano ya mitandaoni

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata watu wawili kwa tuhuma za kuhusika na mauji ya Kiongozi wa CHADEMA Kata ya Hananasif, Daniel John.

Kamanda Mambosasa amesema majina ya watu hao yanahifadhiwa kwa sasa kwa sababu za kiupelelezi. Wamekamatwa Mwanaume na Mwanamke.

=====
UPDATES..

Kuhusu Watu hatari waliotajwa na Musiba, Kamanda Mambosasa amesema Jeshi linafanyia kazi kila taarifa hata kama imetoka kwa Kichaa.

"Kuhusu taarifa iliyosambaa kuwa kuna watu hatari hatari kwa Taifa, nawataka Watanzania waache kushabikia vitu hivyo. Kama mtu anaona kuna tishio watoe taarifa Polisi. Na hao wanaodaiwa kuwa ni hatari, hizo ni taarifa tu kama taarifa nyingine ingawa hatupuuzi" - Kamanda Mambosasa

Aidha, kuhusu Maandamano yanayozungumziwa mitandaoni amesema Jeshi halitoruhusu mpango huo.


-------

Taarifa zaidi..

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amefunguka na kusema kuwa wamefanikiwa kumkamata Rajabu Muhamed maarufu kwa jina la Rajeshi mwenye umri wa miaka 25 ambaye anatuhumiwa kwa kuteka wamama, kuwabaka na kuwapora mali.

Kamanda Mambosasa amesema kuwa mtu huyo hutumia gari aina ya Fun Cargo akikutana na wanawake huwalazimisha kuingia kwenye gari hiyo na kisha kuwatisha yeye ni Freemason hivyo watoe mali zao wasipofanya hivyo huwatishia kuwakata sehemu zao za siri.

"Hutumia gari namba T 172 BLH aina ya Fun Cargo rangi ya Silver huwakamata wanawake, huwanyang'anya wafanyabishara wanaoendelea kufanya shughuli zao na akishawakamata huwaingiza kwenye gari yake kwa nguvu kisha kudai vitu mbalimbali ikiwa pamoja na kuchukua mabegi na baadaye huzunguka nao mtaani huku akiwatisha kuwa yeye ni Freemason na kuwa atawauwa na kuwanyonya damu.

Kitendo hicho hupelekea wa kina mama hao kukabidhi kila walichokuwa nacho lakini pia huwatishia wakatoa password za benki chini ya tishio kubwa la kuwatoa uhai na kuwakata sehemu za siri, huyu ni mnyama wa kutosha ana sura za binadamu lakini ni mnyama" alisema Mambosasa

Kamanda Mambosasa aliendelea kusema kuwa Rajabu Muhamed ameshawafanyia vitendo vya kinyama wanawake wengi sana hapa mjini ikiwa pamoja na kuwabaka na kuwadhalilisha

"Anafanya vitendo vya unyang'anyi kwa kutumia nguvu na hasa kwa wanawake, ubakaji na unyanyasaji wa kila aina, amefanya vitendo vingi sana mjini hapa vya unyanyasaji wa kina mama anawateka anajifanya ni Freemason anawapeleka mahali anapowapeleka na kuwafanyia vitendo vyote vya kinyama.

Huyu muhuni huyu na anachoniambia mimi kwamba ameacha lakini amewadhuru wanawake wengi sana hapa mjini na wachache wenye ujasiri walifika kuripoti na ndiyo tukafuatilia na kufanikiwa kumtia mbaroni jana usiku maeneo ya Kinondoni".
 
Movie nyingine hii
Mnataka kupotezea habari ya Sugu
Weakening majina hadharani yule aliyejeruhiwa awatambue
Isije kuwa na yeye ni mmoja wao, unakumbuka tuliambiwa matokeo ya uchunguzi wa mauaji haya utatushangaza!!
 
Yasije yakajirudia ya Mkenya mwenye mtindio wa akini na kanisa la Gwajima maana ni zilipendwa.
 
Back
Top Bottom