Polisi yatoa mkwara mzito kwa operesheni sangara zanzibar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Polisi yatoa mkwara mzito kwa operesheni sangara zanzibar

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee wa Kale, Feb 13, 2009.

 1. M

  Mzee wa Kale Member

  #1
  Feb 13, 2009
  Joined: Feb 7, 2009
  Messages: 44
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jeshi la Polisi asubuhi ya leo lieweka kikao kizito chini ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi RPC Khatib Abdalla Shaaban huku wakipitia kwa makini mkanda wa Mkutano wa Uzinduzi wa Operesheni Sangara iliyozinduliwa na Viongozi wa Chadema Visiwani hapa uliofanyika katika uwanja wa Komba wapya.

  Katika Mkutano huo kashfa ya matumizi mabaya ya fedha za Umma iliibuliwa, kitendo ambacho Jeshi la Polisi walikiona kama ni matusi ya nguoni dhidi ya viongozi wa Serikali, hatua hiyo ya Polisi ni badala ya pia viongozi wa Chadema kupeleka barua ya kuwapa taarifa polisi kwamba wanaendelea na mikutano ya Operesheni Sangara kesho katika Viwanja vya Kibandamaiti Zanzibar, Hivyo Viongozi wa CHADEMA walitakia waripoti asubuhi ya leo katika Makao Makuu ya Polisi Mkoa wa mjini Magharibi Mwembe Madema,

  Kiongozi mmoja wa Chadema aliyekwenda kusikiliza wito huo alilikuta jopo la maafande wa Polisi wakiendelea kuangalia mkanda wa mkutano huo.

  Alipoingia kwenye ukumbi huo alipewa mkwala mzito kwamba aone matusi waliyokuwa wakiwatukana viongozi, na pia wakamwambia kwamba walitaka kukutana na viongozi wote wa CHADEMA Zanzibar, kwa bahati mbaya aliwajibu kwamba Polisi haikutoa barua ya wito huo, ndio maana alikuja yeye peke yake kusikiliza wito.

  Kamanda wa Polisi wa Mkoa RPC alisema kwamba tulitaka kuuzuia mkutano wenu lakini kwa kuwa ni haki yenu mimi nawaruhusu ila muhakikishe kwamba mnatangaza sera zenu na msijihusishe kabisa na masuala mengine ya ukosoaji wa Serikali.

  Du hii kali kweli iliyotokea asubuhi hii, sijui Kibanda maiti kesho itakuwaje nairusha kwenu wana JF kwa mjadala Ahsanteni.
   
Loading...