Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,801
- 11,961
Saa chache tangu kutoka kwa tukio la watu kujeruhiwa kwa mapanga na kikundi kinachodaiwa kuwa ni 'Panya Road' katika eneo la Kunduchi Mtongani Jijini Dar es Salaam, watu sita wanashikiliwa na Jeshi la Polisi.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Muliro Jumanne Muliro amezungumza hayo leo Mei 2, 2022 akieleza kuwa wanawashikilia watu hao kwa mahojiano ili waeleze walipo wenzao na wanapeleka wapi vitu hivyo baada ya kuiba.
Amesema watuhumiwa ni vijana wadogo ambao waliamua kuacha shule na kujihusisha na matumizi ya dawa za kulevya aina ya bangi.