Polisi yasema itapambana na watakaovuruga uchaguzi mdogo wa marudio

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
3,162
2,000
UF3A1262.jpg
POLISI Wilaya ya Kinondoni imesema itapambana na watakaovuruga uchaguzi mdogo wa marudio katika Jimbo la Kinondoni unaotarajiwa kufanyika Februari 17 mwaka huu. Pia imesema maiti aliyeokotwa katika ufukwe wa Coco Beach jijini Dar es Salaam ni mwanachama wa chama gani.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Kamanda wa Polisi Wilaya ya Kinondoni, Jumanne Muliro, amesema jukumu lake ni kuhakikisha mchakato wote wa masuala ya uchaguzi unafanyika katika misingi ya sheria, kanuni na taratibu za uchaguzi.

Pia ametoa rai kwa wananchi kujitokeza kwa wingi siku hiyo ili waweze kutekeleza haki yao ya kikatiba kwa kufuata sheria na taratibu watakazoelekezwa bila kuleta vurugu.

Katika hatua nyingine, jeshi hilo limesema lilipokea habari kutoka kituo cha polisi cha Oyster Bay ambako msamaria mwema aliripoti kuokotwa kwa maiti ya mtu mmoja katika ufukwe wa Coco Beach wa Bahari ya Hindi.

“Jeshi la polisi liliwatuma askari kwenda eneo la tukio na kukuta mwili wa mtu mwenye jinsia ya kiume anayekadiriwa kuwa na umri kati ya mika 30-35 ukiwa na majeraha mengi mwilini ambapo ulichukuliwa na kupelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili ambapo madaktari walibaini kuwa amekwishafariki,” alisema .

Mmoja waandishi wa habari alipouliza kuhusiana na mtu huyo kuwa mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kama ilivyodaiwa kuripotiwa na chamahicho, Muliro alisema kuwa hana taarifa ya chama cha marehemu huyo.

Muungwana
 
gimanini

JF-Expert Member
Jun 20, 2015
1,414
2,000
Polisi wakifanya kazi bila upendeleo kwa chama Fulani ni wazi uchaguzi utakuwa huru na wa haki.hivyo na wao wazingatie usawa na haki ktk ulinzi na usalama kuelekea na wakati wa uchaguzi.
 
owomkyalo

JF-Expert Member
Dec 26, 2017
4,501
2,000
Wameanza kutoa vitisho policcm Yaani ...awa police sijui ...uwa wanamaisha gani? mshahara wa Elfu mbili ndo unawafanya kufanya ...upuuziii.
 
nyabhingi

JF-Expert Member
Oct 12, 2010
14,373
2,000
huwa najiuliza kama dunia ya kimataifa inayaona haya au nyerere aliweka mzizi hatari hadi maovu hayaonekani!!!!
this all garbage started with him..may god forgive his soul
 
BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
103,145
2,000
Wanaovuruga uchaguzi uchwara wako Ikulu na NEC.
 
GAZETI

JF-Expert Member
Feb 24, 2011
5,118
2,000
Mh! Sasa kuna wakati polisi ndo huvuruga uchaguzi, yaani sijui ni lini Mungu ataihurumia Afrika?
 
owomkyalo

JF-Expert Member
Dec 26, 2017
4,501
2,000
View attachment 695698 POLISI Wilaya ya Kinondoni imesema itapambana na watakaovuruga uchaguzi mdogo wa marudio katika Jimbo la Kinondoni unaotarajiwa kufanyika Februari 17 mwaka huu. Pia imesema maiti aliyeokotwa katika ufukwe wa Coco Beach jijini Dar es Salaam ni mwanachama wa chama gani.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Kamanda wa Polisi Wilaya ya Kinondoni, Jumanne Muliro, amesema jukumu lake ni kuhakikisha mchakato wote wa masuala ya uchaguzi unafanyika katika misingi ya sheria, kanuni na taratibu za uchaguzi.

Pia ametoa rai kwa wananchi kujitokeza kwa wingi siku hiyo ili waweze kutekeleza haki yao ya kikatiba kwa kufuata sheria na taratibu watakazoelekezwa bila kuleta vurugu.

Katika hatua nyingine, jeshi hilo limesema lilipokea habari kutoka kituo cha polisi cha Oyster Bay ambako msamaria mwema aliripoti kuokotwa kwa maiti ya mtu mmoja katika ufukwe wa Coco Beach wa Bahari ya Hindi.

“Jeshi la polisi liliwatuma askari kwenda eneo la tukio na kukuta mwili wa mtu mwenye jinsia ya kiume anayekadiriwa kuwa na umri kati ya mika 30-35 ukiwa na majeraha mengi mwilini ambapo ulichukuliwa na kupelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili ambapo madaktari walibaini kuwa amekwishafariki,” alisema .

Mmoja waandishi wa habari alipouliza kuhusiana na mtu huyo kuwa mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kama ilivyodaiwa kuripotiwa na chamahicho, Muliro alisema kuwa hana taarifa ya chama cha marehemu huyo.

Muungwana
Nyie police tumewavumilia mda mrefu ...tabia zenu zakupiga watu na kuwalemeza..sio sawa ..siku ya kupiga kura tutaonana.sasa...mje mjidai mnawabeba ccm mje muone.
 
Retired

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
25,808
2,000
huwa najiuliza kama dunia ya kimataifa inayaona haya au nyerere aliweka mzizi hatari hadi maovu hayaonekani!!!!
this all garbage started with him..may god forgive his soul
Exactly, he is the architecture of this dictatorship regime we are in. He left a shithole constitution of which he admitted was and still is of a dictatorial nature, when in the hands of a dictator . I never glorify Nyerere!
 
nyabhingi

JF-Expert Member
Oct 12, 2010
14,373
2,000
Exactly, he is the architecture of this dictatorship regime we are in. He left a shithole constitution of which he admitted was and still is of a dictatorial nature, when in the hands of a dictator . I never glorify Nyerere!
history books need to be re-written
 
Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
78,135
2,000
Mulilo, siku ya hukumu mbele ya Mungu CCM haitakuwepo, utasimama peke yako. Tenda haki!
Huko mbona mbali sana ! Aliyekuwa IGP wa Tanzania anayetambulika kwa jina la OMARI MAHITA , ambaye rekodi yake ya ukatiri haijavunjwa , baada ya kustaafu ALIBURUZWA MAHAKAMANI KWA KOSA LA AIBU LA KUMPACHIKA MIMBA HOUSE GIRL WAKE MWENYEWE NA KURUKA MATUNZO YA MTOTO , BADO HAIJAFAHAMIKA KAMA ALIMBAKA KWA KUMTISHA NA MAVYEO YAKE AU WALIKUBALIANA
 
Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
78,135
2,000
Nyie police tumewavumilia mda mrefu ...tabia zenu zakupiga watu na kuwalemeza..sio sawa ..siku ya kupiga kura tutaonana.sasa...mje mjidai mnawabeba ccm mje muone.
Polisi isipoingilia kati mgombea wa ccm hawezi kupata hata kura 500 , hali ni mbaya mno !
 
new sheby

Member
Nov 30, 2017
43
125
View attachment 695698 POLISI Wilaya ya Kinondoni imesema itapambana na watakaovuruga uchaguzi mdogo wa marudio katika Jimbo la Kinondoni unaotarajiwa kufanyika Februari 17 mwaka huu. Pia imesema maiti aliyeokotwa katika ufukwe wa Coco Beach jijini Dar es Salaam ni mwanachama wa chama gani.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Kamanda wa Polisi Wilaya ya Kinondoni, Jumanne Muliro, amesema jukumu lake ni kuhakikisha mchakato wote wa masuala ya uchaguzi unafanyika katika misingi ya sheria, kanuni na taratibu za uchaguzi.

Pia ametoa rai kwa wananchi kujitokeza kwa wingi siku hiyo ili waweze kutekeleza haki yao ya kikatiba kwa kufuata sheria na taratibu watakazoelekezwa bila kuleta vurugu.

Katika hatua nyingine, jeshi hilo limesema lilipokea habari kutoka kituo cha polisi cha Oyster Bay ambako msamaria mwema aliripoti kuokotwa kwa maiti ya mtu mmoja katika ufukwe wa Coco Beach wa Bahari ya Hindi.

“Jeshi la polisi liliwatuma askari kwenda eneo la tukio na kukuta mwili wa mtu mwenye jinsia ya kiume anayekadiriwa kuwa na umri kati ya mika 30-35 ukiwa na majeraha mengi mwilini ambapo ulichukuliwa na kupelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili ambapo madaktari walibaini kuwa amekwishafariki,” alisema .

Mmoja waandishi wa habari alipouliza kuhusiana na mtu huyo kuwa mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kama ilivyodaiwa kuripotiwa na chamahicho, Muliro alisema kuwa hana taarifa ya chama cha marehemu huyo.

Muungwana
Huyu nae katoka wapi
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom