Polisi yasema bado inaendelea kumsaka Dk. Mwaka

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
Kamishina msaidizi wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, Salum Hamdan amesema bado wanamtafuta mmiliki wa kampuni ya Foreplan Juma Mwaka kama walivyoagizwa na Naibu Waziri wa Afya.

Alisema vijana wake wapo kazini kuhakikisha wanampata ndani ya saa 24 kama walivyoagizwa hapo jana.

Hatua hiyo ni utekelezaji wa agizo la Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Hamisi Kigwangalla la kumtafuta baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika jengo hilo na kukuta huduma zinaendelea.

Akiwa katika jengo hilo akikagua ndani mara baada ya kupata kibali cha Polisi cha kufanya upekuzi, wateja wa Dk Mwaka walikuwa wanaendelea kuingia kufuata huduma ya matibabu huku wengi wao wakiwa kina mama.

Chanzo: Mwananchi
 
Hawajampata tu huyu kiumbe???? Hivi hii ya kuwakwepa polisi tena ukiwa unajua wanakutafuta,sio kosa kisheria???
 
Polisi wangemshauri Waziri apambane na vifo vya watoto na uhaba wa damu pamoja na vifaa vyabkutolea damu ukosefu wa dawa za msingi plus huduma mbovuu sana za afya katika Hospital za Serikali hasaa Temeke na Mwananyamala.
 
This iz shamful mtu anatibu wanaweka figisu tatizo lake nn kawekeza na kwenye ndondo bado tyuuuu duh waone aibu bhanaaa
 
Polisi wangemshauri Waziri apambane na vifo vya watoto na uhaba wa damu pamoja na vifaa vyabkutolea damu ukosefu wa dawa za msingi plus huduma mbovuu sana za afya katika Hospital za Serikali hasaa Temeke na Mwananyamala.

Na inasemekana jacho kwa watoto zimeadimika nchini...?
 
Kamishina msaidizi wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, Salum Hamdan amesema bado wanamtafuta mmiliki wa kampuni ya Foreplan Juma Mwaka kama walivyoagizwa na Naibu Waziri wa Afya.

Alisema vijana wake wapo kazini kuhakikisha wanampata ndani ya saa 24 kama walivyoagizwa hapo jana.

Hatua hiyo ni utekelezaji wa agizo la Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Hamisi Kigwangalla la kumtafuta baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika jengo hilo na kukuta huduma zinaendelea.

Akiwa katika jengo hilo akikagua ndani mara baada ya kupata kibali cha Polisi cha kufanya upekuzi, wateja wa Dk Mwaka walikuwa wanaendelea kuingia kufuata huduma ya matibabu huku wengi wao wakiwa kina mama.

Chanzo: Mwananchi
Naipenda demokrasia ya Tanzania. Hivi naibu waziri au kiongozi yoyote anayo haki kisheria kuliamuru jeshi la Polisi kumkamata mtu na kutoa hata muda wa kutekeleza amri hiyo? Hivi tutasalimika na waungu watu hawa?
 
Hii dunia utajificha wapi atapatikana tu stay tuned.
Sawa!atapatikana na atatoka kwA dhamana,
Issue ni kwanini Huyu Mwaka anatumia nguvu,muda mwingi kusumbuana n'a Mwaka utafikiri Kuna personel issue....
Kuna shida nyingi huko mahospital bado

Ova
 
Naipenda demokrasia ya Tanzania. Hivi naibu waziri au kiongozi yoyote anayo haki kisheria kuliamuru jeshi la Polisi
kumkamata mtu na kutoa
hata muda wa kutekelez
a amri hiyo? Hivi
tutasalimika na waungu
watu hawa?
Sahvi polisi wanatumika vibaya......kidogo utasikia kamata yule
 
Naipenda demokrasia ya Tanzania. Hivi naibu waziri au kiongozi yoyote anayo haki kisheria kuliamuru jeshi la Polisi kumkamata mtu na kutoa hata muda wa kutekeleza amri hiyo? Hivi tutasalimika na waungu watu hawa?

Mimi ukiingia mtaani kwangu bila taarifa nakuweka ndani masaa 2 halafu bado nina uwezo wa kuongeza kama sijaridhika hii ni Tanzania hata balozi wa nyumba kumi ni kigogo.
 
Kamishina msaidizi wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, Salum Hamdan amesema bado wanamtafuta mmiliki wa kampuni ya Foreplan Juma Mwaka kama walivyoagizwa na Naibu Waziri wa Afya.

Alisema vijana wake wapo kazini kuhakikisha wanampata ndani ya saa 24 kama walivyoagizwa hapo jana.

Hatua hiyo ni utekelezaji wa agizo la Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Hamisi Kigwangalla la kumtafuta baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika jengo hilo na kukuta huduma zinaendelea.

Akiwa katika jengo hilo akikagua ndani mara baada ya kupata kibali cha Polisi cha kufanya upekuzi, wateja wa Dk Mwaka walikuwa wanaendelea kuingia kufuata huduma ya matibabu huku wengi wao wakiwa kina mama.

Chanzo: Mwananchi
akina mama ndio victim wa miujiza. si kwa mwaka kwa gwajima et al utawakuta. lazima tuwalinde mama zetu na hawa matapeli
 
Hawajampata tu huyu kiumbe???? Hivi hii ya kuwakwepa polisi tena ukiwa unajua wanakutafuta,sio kosa kisheria???
Unafikiri yeye hana akili kuwa ukienda polisi leo ni mpaka jumanne? watulize ball ataenda tu jumanne, kwani kuna ushahidi gan kwamba hizi taarifa zimemfikia, ndo maana wanashindwa kesi kizembe
 
Back
Top Bottom