Polisi yaruhusu mikutano CHADEMA tangu jana: NINI MAANA YAKE? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Polisi yaruhusu mikutano CHADEMA tangu jana: NINI MAANA YAKE?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by AmaniKatoshi, Nov 30, 2010.

 1. A

  AmaniKatoshi Senior Member

  #1
  Nov 30, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 158
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Polisi yaruhusu mikutano CHADEMA.


  Na Tumaini Makene.

  SIKU moja baada ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kulilalamikia Jeshi la Polisi juu ya kutoa amri ya kuzuia mikutano yake ya hadhara na ile ya kuwapokea wabunge wa chama hicho maeneo mbalimbali nchini, jeshi hilo limeondoa rasmi zuio hilo.

  Jeshi hilo limesema kuwa limeondoa rasmi zuio hilo kuanzia jana baada ya 'uchaguzi kumalizika rasmi juzi' kwa mujibu wa taratibu za ndani za usimamizi wa shughuli ya uchaguzi, ambazo walikuwa wamejiwekea, ambazo hazikuwa zikimlenga mtu wala chama chochote cha siasa.

  Jana CHADEMA kilikaririwa na vyombo vya habari kikisema kuwa vitendo hivyo vya polisi vilikuwa vinashiria hatari kwa demokrasia nchini, kuvunja haki za kikatiba na za kisheria za wananchi, huku vikiwa ni dalili ya nchi kupelekwa katika 'dola ya kipolisi,' kama vile ilivyokuwa katika nchi za Zimbabwe, Afrika Kusini wakati wa utawala wa makaburu na Kenya wakati wa utawala wa Rais wa Pili, Daniel Arap Moi.

  Vyombo vya habari vilimnukuu Mkurugenzi wa Haki, Sheria na Katiba wa CHADEMA, Bw. Tundu Lissu akisema kuwa chama hicho hakitakuwa tayari kunyamazia hatua hiyo, kwani ingeweza kuwa mwendelezo wa kuminya haki ya watu kujumuika na kujadili mustakabli wa nchi yao, kwa mujibu wa katiba ya nchi.

  Akizungumza na Majira jana kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Said Mwema, Mkurugenzi wa Utawala na Fedha, Kamishna wa Polisi Clodwig Mtweve alisema kuwa uzuiaji huo wa maandamano na mikusanyiko ya kuwapokea wabunge na mikutano mingine ya kawaida ya hadhara, ilikuwa sehemu ya utaratibu wa jeshi hilo wakati na baada ya uchaguzi.

  Bw. Mtweve alisema kuwa uzuiaji huo haukumlenga mtu yeyote wala chama chochote kile cha siasa, bali ulikuwa ukizingatia hali halisi ya nchi baada ya uchaguzi, ambapo "serikali ilikuwa haijaundwa wala mawaziri hawajateuliwa," hivyo wameondoa rasmi amri hiyo jana.

  "Kusema ukweli nimeshaongea na vyombo vya habari vingi leo juu ya suala hilo na nimeshatoa ufafanuzi. Tulichokuwa tumezuia ni maandamano na kupongezana si mikutano...unajua baada ya bunge kumalizika kulitolewa maombi mbalimbali ya maandamano watu wakitaka kuwapokea wabunge wao.

  "Lakini unajua maandamano ni kitu kingine na mikutano ni kitu kingine, kila kimoja kina utaratibu wake, mapema ilikuwa imetolewa amri ya kiutendaji ndani ya Jeshi la Polisi kusimamia mambo yote hayo ya maandamano na mikutano...lakini amri hiyo sasa imeondolewa rasmi leo (jana) baada ya uchaguzi kuisha rasmi jana (juzi)," alisema Bw. Mtweve na kuongeza;

  "Kwa mujibu wa utaratibu tuliokuwa tumejiwekea ndani ya jeshi, uchaguzi umemalizika jana (jana)...ma-OCD walipewa maelekezo ya kutoruhusu masuala ya maandamano kwani yale hayaangalii tu kitendo chako cha mwisho, bali yanahusisha taasisi nyingi na masuala ya usalama wa mali za watu, suala hilo halikumlenga mtu wala chama cha siasa...

  "Hata hivyo, tulijaribu kuhoji kama ni suala la kupongezana kwani ni lazima watu wapongezane kwa kukusanyika uwanjani, wangeweza kufanya hata hotelini au ukumbini mahali," alisema.

  Bw. Mtweve aliongeza kusema kuwa haikuwa vizuri baada ya uchaguzi kuruhusu maandamano na mikutano ya hadhara kwani nchi ilikuwa imetoka katika uchaguzi, huku 'mambo yakiwa hayajakaa sawa', serikali ikiwa haijaundwa na mawaziri hawajateuliwa.

  Majira lilipotaka kujua kama jeshi hilo lilikuwa na wasiwasi zaidi na maandamano na mapokezi ya wabunge kwa nini lilizuia hata mikutano ya hadhara kama vile huko Segerea, Dar es Salaam, Bw. Mtweve alisema kuwa hiyo ilikuwa ni kwa mujibu wa "operetion order" (amri ya utendaji).

  Alisisitiza kuwa kuanzia jana utaratibu wa kuomba na kukubaliwa mikutano ya hadhara na maandamano unarudi kama kawaida chini ya makamanda wa polisi wa wilaya.

  Wakati huo huo, CHADEMA kimepongeza hatua ya kuondoa amri hiyo na kusema kuwa ni jambo zuri lakini halizuii kusudio lake la kufikisha hoja yake bungeni juu ya uvunjifu wa Sheria ya Haki, Mamlaka na Kinga ya Bunge ya mwaka 1988, kikisema kuwa polisi hawana ruhusa ya kuzuia mikutano ya wabunge "pale serikali inapokuwa haipo."

  Akipongeza hatua hiyo, Mkurugenzi wa Haki, Sheria na Katiba wa CHADEMA, Bw. Tundu Lissu alisema "Kama wameiondoa basi ni jambo zuri sana...ni kitendo kizuri lakini hakituzuii kwenda kuhoji bungeni kwa nini wabunge wetu walizuia kufanya kazi...kufanya mikutano.

  "Hakuna sheria yoyote inayowaruhusu polisi kuvunja au kukiuka sheria ya haki, mamlaka na kinga ya bunge ikiwa serikali haipo au mawaziri hawajateuliwa," alisema Bw. Lissu ambaye pia ni Mnadhimu Mkuu wa Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni

  Chanzo ni Gazeti la Majira la tarehe 30/11/2010 GAZETI HURU LA KILA SIKU:

  My take:

  1. Kwa nini kizuizi kuondolewa siku moja baada ya Lisu na Chadema kutoa tamko?
  2. Je linahitajika somo kwa polisi kuhusu vifungu vya katiba?
  3. Hiyo mamlaka ya juu Mtweve anayotaja niipi?
  4. Kama Mwema alizuia kwa kuongea na media, kwa nini jana anamtuma mkurugenzi wa fedha?

  There are more questions than answers!
   
 2. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #2
  Nov 30, 2010
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Baada ya Mawaziri kuapishwa na rasmi, na jeshi la polisi kuhakikisha kuwa kutakuwa na usalama wa kutosha kwa raia wote, wawe Chadema, CCM, Cuf au wa chama kingine chochote na wale wasio na chama.

  Walizuiliwa kufanya maandamano.

  Sasa wafanye mikutano, kumbuka, sio maandamano. Mikutano.

  Na ikiwa hiyo mikutano itasabisha uvunjifu wa amani. Basi hao wavunja amani watashughulikiwa ipasavyo.
   
 3. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #3
  Nov 30, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Kuapishwa kwa mawaziri kunahusiana vp na mikutano ya CHADEMA na wananchi?
  Kumbuka swala ni mikutano na sio vurugu.
  Pia haimanishi kwamba watu wakiandamana basi wanafanya fujo. Noo
   
 4. LoyalTzCitizen

  LoyalTzCitizen JF-Expert Member

  #4
  Nov 30, 2010
  Joined: Sep 15, 2010
  Messages: 1,807
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  :amen:
   
 5. M

  Misterdennis JF-Expert Member

  #5
  Nov 30, 2010
  Joined: Jun 4, 2007
  Messages: 1,521
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 160

  Sawa afande tumekusikia ... lakini na maandamano tutafanya pia.
   
 6. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #6
  Nov 30, 2010
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  hiyo tz zaidi tuijuavyo,nimewahi kuuliza swali hapa jf kuwa hawa polisi wapo kwa maslahi ya nani? sikupata majibu sasa polepole majibu yanakuja juu ya jeshi la polisi la tz,nadhani wapo kwa maslahi ya watu wachache ambao wakisema jambo basi polisi hutekeleza kwa vitendo.
  ipo siku tutaliona jsho la kunguni

  mapinduziii daimaaaa
   
 7. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #7
  Nov 30, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,823
  Likes Received: 10,120
  Trophy Points: 280
  Hicho kikao chao walikaa juzi usiku na kuondoa hiyo amri usiku huohuo hadi jana asubuhi watangaze kuondoa rasmi? hivi uchaguzi unaisha baada ya kuhesabiwa kura na mshindi kupatikana au ni hadi baraza litangazwe? na kama hivyo ndivyo? kwani baraza lilitangazwa jana au juzi? kuna uhusiano gani wa baraza na mikutano ya vyama? shiiiii.....
   
 8. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #8
  Nov 30, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  CCM wajinga sana...yaani ukiwa mwizi unakuwa muoga sana sijui kwa nini
   
 9. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #9
  Nov 30, 2010
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Hizi sababu za polisi mbona hazikutolewa katika hati ya zuio (kama ulikuwepo)? Lakini Chadema kwa mara nyingine wamethibitisha umakini wao na uwezo wa kudai haki kwa kufuata sheria na taratibu zilizopo. Wamevumilia na kudai haki yao bila kuleta fujo ingawa katika mchakato huo baadhi watu tayari walidai Chadema wanataka kuleta fujo

  well done Chadema, lazima tutafika
   
 10. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #10
  Nov 30, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Asanteni sana.
   
 11. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #11
  Nov 30, 2010
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Hata wakizuia mikutano si wananchi wenye akili nzuri wameshajua kwamba rais wao hakushinda kihalali? Chadema kususa hotuba ilikuwa bao la dhahabu
   
 12. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #12
  Nov 30, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Hao ndo Polisi bana! wanatishiwa asubuhi, jioni wanaondoa ban!! hahahaha!
   
 13. L

  LAT JF-Expert Member

  #13
  Nov 30, 2010
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  Al zawahiri hajambo?....mmemaliza mafunzo
   
 14. Mabel

  Mabel JF-Expert Member

  #14
  Nov 30, 2010
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 1,018
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Tatizo polisi hawajui sheria wala katiba ya nchi, na wanasema na kutenda kutokana na maamuzi ya wanasiasa na si kwa mjibu wa kanuni na sheria. Jeshi la polisi limekuwa genge la wahuni, watu wanakwenda siku hizi kwa sababu tu mtaani panachimbika na si kwa nia na moyo thabiti wa kutumikia wananchi.
   
 15. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #15
  Nov 30, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Polisi na CCM wana mambo ya kikoloni kweli
   
 16. K

  KERENG'ENDE JF-Expert Member

  #16
  Nov 30, 2010
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 398
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  IGP Mwema naye yupo kwenye genge la waasisi wa kuvunja amani nchini linaloongozwa na Mkwere na RH wa CUF
   
 17. P

  Preacher JF-Expert Member

  #17
  Nov 30, 2010
  Joined: Aug 25, 2008
  Messages: 328
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hivi mbona nchi nyingine zinafanya maandamano??? Tanzania maandamano wanayaogopa sana - why????? Na polisi wa CCM - yaani wenyewe wana shida kama nini - ila hata mseme mnafanya maandamano kwa ajili ya kuwatetea - bado watakataa - ama kweli umaskini saa ingine unaweza kuingia hadi kwenye ubongo wa mtu!!!!!!!!!!

  Wanatakakiwa POLISI nao waandamane siku moja.......................:teeth::teeth::teeth:
   
 18. kabila01

  kabila01 JF-Expert Member

  #18
  Nov 30, 2010
  Joined: Apr 21, 2009
  Messages: 3,013
  Likes Received: 1,825
  Trophy Points: 280
  Wameogopa nguvu ya wananchi. Usicheze na peoples power. CHADEMA ni chama cha wasomi baada ya kuona CHADEMA imetoa vifungu vya sheria vinavyowakaba ndo wanajifanya wanatengua Amri. Plato alishasema kazi za polisi ni za Iron boys, watu wanaotumia nguvu nyingi kuliko akili ndo maana wanafanya mambo bila kutafakari
  Hivi CUF hawakuliona suala hili na vifungu vya sheria hawakuviona? Kweli CUF sio chama cha upinzani nadhani 2015 tutakipoteza kabisa kwa huku bara kitabaki visiwani
   
 19. BigTime

  BigTime Member

  #19
  Nov 30, 2010
  Joined: Sep 17, 2008
  Messages: 43
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  :confused2:
  :nono:
   
 20. b

  baraka boki Senior Member

  #20
  Nov 30, 2010
  Joined: Sep 20, 2010
  Messages: 181
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 0
  Peoples power
   
Loading...