Polisi yapiga marufuku taa za mwanga mkali kwenye magari

Mapya Yaja

JF-Expert Member
Feb 8, 2013
560
403
Jeshi la Polisi limepiga marufuku kwa wenye magari na pikipiki kufunga taa zenye mwanga mkali kutokana na kulalamikiwa kuwa chanzo cha ajali wakati wa usiku.

Source: ITV-habari saa 2:00 usiku leo.

NB: Nawapongeza sana polisi kwa kuliona hili. Kuna watu wamefunga tube light kwenye magari na pikipiki. Sijui huwa wanajisikiaje wanaposumbua madreva wengine kwa vitaa vyao hivi.
 
Nani atakuwa anaamua kuwa huu ni Mwanga Mkali au kutakuwa na Viwango maalum?
Maduka yanayouza hizo taa yametaarifiwa kuwa sasa hizo bidhaa ni haramu hapa Tanzania?

Siku hizi haishangazi hata Sinza unaweza ukakamatwa kwa kosa la kuendesha kwa Mwendo kasi na huwezi kubisha kwa kuwa hakuna Viwango sasa tujiandae na hili la kosa la taa zenye Mwanga Mkali
 
Si kwenye magari tu,hata ktk BODABODA utakuta jitu limefunga nyuma,inakuwa kero sana mfano wake hauelezeki
 
Nani atakuwa anaamua kuwa huu ni Mwanga Mkali au kutakuwa na Viwango maalum?
Maduka yanayouza hizo taa yametaarifiwa kuwa sasa hizo bidhaa ni haramu hapa Tanzania?

Siku hizi haishangazi hata Sinza unaweza ukakamatwa kwa kosa la kuendesha kwa Mwendo kasi na huwezi kubisha kwa kuwa hakuna Viwango sasa tujiandae na hili la kosa la taa zenye Mwanga Mkali

Atakayekuwa amemulikwa ndiye ataamua kuwa ni mwanga mkali!!!
 
Kuna Mpuuzi mmoja pale Darajani Mlandizi, lile daraja aliloliandika Mwigulu jina lake, alikua na Landcruiser aisee alinipiga zile Taa nikataka kupotea kabisa. Yaani jamaa alikua amezifunga kila mahali. Ni hatari sana Sana, zipigwe faini kabisa
 
Jeshi la Polisi limepiga marufuku kwa wenye magari na pikipiki kufunga taa zenye mwanga mkali kutokana na kulalamikiwa kuwa chanzo cha ajali wakati wa usiku.
Source ITV-habari saa 2:00 usiku leo.
NB: Nawapongeza sana polisi kwa kuliona hili. Kuna watu wamefunga tube light kwenye magari na pikipiki. sijui huwa wanajisikiaje wanaposumbua madreva wengine kwa vitaa vyao hivi.
Nilitaka nimuulize kamanda Mpinga hizi stupid LED bars zinazowekwa kwenye magari kiholela ni sawa?

Bado wale ambao wamefanya taa za brake disco lights.

Hoongera jeshi la polisi.
 
Jeshi la Polisi limepiga marufuku kwa wenye magari na pikipiki kufunga taa zenye mwanga mkali kutokana na kulalamikiwa kuwa chanzo cha ajali wakati wa usiku.
Source ITV-habari saa 2:00 usiku leo.
NB: Nawapongeza sana polisi kwa kuliona hili. Kuna watu wamefunga tube light kwenye magari na pikipiki. sijui huwa wanajisikiaje wanaposumbua madreva wengine kwa vitaa vyao hivi.
tuwakumbishe na zile horn za emergency kuwekwa kwenye bajaj na pikipiki...
 
Nani atakuwa anaamua kuwa huu ni Mwanga Mkali au kutakuwa na Viwango maalum?
Maduka yanayouza hizo taa yametaarifiwa kuwa sasa hizo bidhaa ni haramu hapa Tanzania?

Siku hizi haishangazi hata Sinza unaweza ukakamatwa kwa kosa la kuendesha kwa Mwendo kasi na huwezi kubisha kwa kuwa hakuna Viwango sasa tujiandae na hili la kosa la taa zenye Mwanga Mkali
Taa hizo ni za kuongezea. Wanafunga mtaani, LED bars, its illegal.
 
Back
Top Bottom