Polisi yapiga marufuku maandamano ya CHADEMA

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
52,015
114,360
1.jpg

Jeshi la Polisi limetoa tamko kuhusu tangazo la Baraza la Vijana wa Chadema (BAVICHA) kuwa kesho wamepanga kufanya maandamano hadi Ikulu kwa lengo la kuishinikiza serikali kubadili msimamo wake kuhusu TBC kutorusha Live baadhi ya vikao vya Bunge.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Siro amepiga marufuku maandamano hayo na kuwataka vijana hao kutumia njia mbadala za kupata ufumbuzi wa suala hilo badala ya maandamano.

Akitoa sababu za kuzuia kufanyika kwa maandamano hayo, Kamanda Sirro alisema kuwa hakuna taarifa na pia hakuna uthibitisho kuwa maandamano hayo yatapokewa na Rais Magufuli.

Pia, Kamanda Sirro alieleza kuwa BAVICHA hawakuanisha barabara ambazo wanatarajia kutumia katika maandamano hayo.

“Siku hiyo sio nzuri sana kwa sababu ni siku ambayo watu wanakuwa kazini. Ni siku ambayo wengi watataka kutumia barabara hizo kwa ajili ya huduma za kijamii. Na kwa sababu kuna option nyingine ya kuweza kupata suluhu hiyo, nisema tu kwamba maandamano hayo yamepigwa marufuku,” alisema.
 
Hahahaa...eti makamanda! Unakuta kajamaa kamekondaaa hakana stamina alaf kamepiga viroba kanajiita kamanda, uzito wa jina kamanda unapotea skuizi.
Tufanyeni kazi tujenge nchi. Kama ni ujumbe tumeni watu kadhaa waupeleke ikulu wengine pigeni kazi tusipotezeane muda.
 
Nani kamsababishia akonde
Ni ccm iliyoshindwa kuweka Sera nzuri za kiuchumi ili kuhakikisha zinawainua wananchi na kuwatoa ktk Lindi LA umaskini
Ccm imebaki kuwapa elfu mbili za kupiga kura baada ya hapo watajijua wataachaje kukonda?

Wanene wote ni ishara ya ufisadi mkubwa
 
Polisi kanda ya Dar es Salaam imepiga marufuku maandamano yetu makamanda.Makamanda tulitoa taarifa ya kutaka kuandamana mpaka Ikulu kwenda kutoa madukuduku juu ya hali ya kisiasa na kijamii.Polisi inasema kesho siku ya kazi hivyo italeta msongamano....Nchi imeanza kukosa demokrasia

fanya kazi, demokrasia gani wataka weye.
 
Nani kamsababishia akonde
Ni ccm iliyoshindwa kuweka Sera nzuri za kiuchumi ili kuhakikisha zinawainua wananchi na kuwatoa ktk Lindi LA umaskini
Ccm imebaki kuwapa elfu mbili za kupiga kura baada ya hapo watajijua wataachaje kukonda?

Wanene wote ni ishara ya ufisadi mkubwa
Sasa kama anashindia gongo na viroba asikonde tu?
 
Polisi kanda ya Dar es Salaam imepiga marufuku maandamano yetu makamanda.Makamanda tulitoa taarifa ya kutaka kuandamana mpaka Ikulu kwenda kutoa madukuduku juu ya hali ya kisiasa na kijamii.Polisi inasema kesho siku ya kazi hivyo italeta msongamano....Nchi imeanza kukosa demokrasia
Hili jeshi la police linaumwa ujue
 
Polisi kanda ya Dar es Salaam imepiga marufuku maandamano yetu makamanda.Makamanda tulitoa taarifa ya kutaka kuandamana mpaka Ikulu kwenda kutoa madukuduku juu ya hali ya kisiasa na kijamii.Polisi inasema kesho siku ya kazi hivyo italeta msongamano....Nchi imeanza kukosa demokrasia

Huyo Kijana Sembeye Wa BAVICHA Anajiamini Nini Hadi Anajifanya Ana KIMBELEMBELE Hivi? Kaamua Kujitoa MUHANGA au? Familia Yake Imemruhusu?
 
Hahahaa...eti makamanda! Unakuta kajamaa kamekondaaa hakana stamina alaf kamepiga viroba kanajiita kamanda, uzito wa jina kamanda unapotea skuizi.
Tufanyeni kazi tujenge nchi. Kama ni ujumbe tumeni watu kadhaa waupeleke ikulu wengine pigeni kazi tusipotezeane muda.
Sa tutapigaje kazi bila kuvuta bhange maana mbunge wetu amesema tukivuta bhange tunalima sana
 
Hivi Bavicha wanaenda kumuona Rais gani? Hivi Rais wao si ni Lowasa? Ni Lini wameanza kumtambua Rais Magufuli?

Nikiwaambieni Kuwa Rais Mstaafu Mkapa Ni Nabii Mwenye Maono YALIYOTUKUKA Mnakataa! Hivi Mnadhani Alivyowaita Hawa Wapinzani Hasa CHADEMA Kuwa Ni " Wapumbavu Na Malofa " Alikosea au Labda Alikuwa AMELEWA? Tunaoujua Ujiniasi Wa Mzee Mkapa Wala HATUKUSHANGAA Kwani ALISEMA UKWELI MTUPU.
 
Back
Top Bottom