Polisi yaokoa mifugo Tarime

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
POLISI Kanda Maalumu ya Tarime/Rorya, imefanikiwa kuokoa mifugo kadhaa iliyokuwa imeibwa katika kaya za Daudi Wankuru na Marwa Mihinda wanaoishi Nyakarima kata ya Ganyange, mkoani Mara.

Polisi walilazimika kutumia nguvu kurejesha mifugo hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake hapo Desemba 14, Kamanda wa Polisi Tarime/Rorya, Costantine Massawe alisema wizi huo ulitokea saa 8 usiku wa kuamkia Jumanne.

Alisema kundi la watu zaidi ya 8 waliokuwa na silaha wanaosadikiwa kutoka Kenya wakishirikiana na wezi wenzao kutoka Tanzania walivamia makazi ya Daud Wankuru na kumpora ng'ombe 7, mbuzi 10 na kondoo 4 na kisha kuvamia kaya ya Marwa Mihinda na kupora ng'ombe 2 na kuondoka nao.

Kamanda Massawe alisema jeshi lake baada ya kupata taarifa ya wizi huo walifika mapema katika Kitongoji hicho na kuungana na wananchi kufuata nyayo hadi kijiji cha Nyantira kilichopo mpakani mwa Kenya na Tanzania ambapo waliikuta mifugo hiyo na watuhumiwa.

Katika mapambano hayo, ng'ombe 2 walijeruhiwa kwa risasi.

Katika siku za karibuni wizi wa mifugo umeanza kuibuka tena kutokana na shughuli za tohara (Saro) zinazoendelea wilayani hapa ambapo wezi hutumia mwanya huo wakati watu wamekwenda kwenye sherehe hizo na kuiba mifugo.
 
Back
Top Bottom