Polisi yamwachia Dk. Shika baada ya kujidhamini mwenyewe

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,287
Kamanda Mambosasa amesema ameagiza Dk Shika ajidhamini na awe anaripoti polisi

Dar es Salaam. Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema limefikia uamuzi wa kumtaka Dk Louis Shika ‘bilionea wa nyumba za Lugumi’ ajidhamini yeye mwenyewe baada ya kukosa mtu yeyote aliyejitokeza kwenda kutaka kumwekea dhamana.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumanne Novemba 14, Kamanda wa kanda hiyo, Lazaro Mambosasa amesema “uchunguzi wa tuhuma dhidi yake unaendelea lakini mpaka sasa hakuna mtu yeyote aliyefika kutaka kumwekea dhamana, yaani anaishi kama mtu wa nyikani.”

Mambosasa ameongeza, “nimeagiza watendaji wangu wamwachie kwa dhamana yaani ajidhamini yeye mwenyewe na awe anakuja kuripoti,” amesema Mambosasa

Kamanda huyo ametoa kauli hiyo mara baada ya Mwananchi kumtafuta kutaka kujua hatima ya Dk Shika ambaye ameshikiliwa tangu Novemba 9 akituhumiwa kuvuruga mnada wa nyumba za kifahari za mfanyabishara Said Lugumi

Dk Shika tangu siku hiyo amekuwa gumzo sehemu mbalimbali kutokana na kile alichokifanya siku ya mnada alipokuwa akipandisha bei dhidi ya washindani wake na moja ya kauli zake zinaendelea kutumika hadi sasa ni ‘Mia 900 itapendeza.’

Chanzo: Mwananchi

=====

UPDATES: Dr Shika ameachiwa baada ya kujidhamini mwenyewe

View attachment 630826

Dar es Salaam. Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limefikia uamuzi wa kumuachia Dk Louis Shika ‘bilionea wa nyumba za Lugumi’ baada ya kutimiza masharti ya dhamana ya kujidhamini yeye mwenyewe baada ya kukosa mtu yeyote aliyejitokeza kwenda kutaka kumwekea dhamana.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumanne Novemba 14, Kamanda wa kanda hiyo, Lazaro Mambosasa amesema “uchunguzi wa tuhuma dhidi yake unaendelea lakini mpaka sasa hakuna mtu yeyote aliyefika kutaka kumwekea dhamana, yaani anaishi kama mtu wa nyikani.”

Mambosasa ameongeza, “nimeagiza watendaji wangu wamwachie kwa dhamana yaani ajidhamini yeye mwenyewe na awe anakuja kuripoti,” amesema Mambosasa

Kamanda huyo ametoa kauli hiyo mara baada ya Mwananchi kumtafuta kutaka kujua hatima ya Dk Shika ambaye ameshikiliwa tangu Novemba 9 akituhumiwa kuvuruga mnada wa nyumba za kifahari za mfanyabishara Said Lugumi

Dk Shika tangu siku hiyo amekuwa gumzo sehemu mbalimbali kutokana na kile alichokifanya siku ya mnada alipokuwa akipandisha bei dhidi ya washindani wake na moja ya kauli zake zinaendelea kutumika hadi sasa ni ‘Mia 900 itapendeza.’

Chanzo: Mwananchi
 
Kamanda Mambosasa amesema ameagiza Dk Shika ajidhamini na awe anaripoti polisi

Dar es Salaam. Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema limefikia uamuzi wa kumtaka Dk Louis Shika ‘bilionea wa nyumba za Lugumi’ ajidhamini yeye mwenyewe baada ya kukosa mtu yeyote aliyejitokeza kwenda kutaka kumwekea dhamana.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumanne Novemba 14, Kamanda wa kanda hiyo, Lazaro Mambosasa amesema “uchunguzi wa tuhuma dhidi yake unaendelea lakini mpaka sasa hakuna mtu yeyote aliyefika kutaka kumwekea dhamana, yaani anaishi kama mtu wa nyikani.”

Mambosasa ameongeza, “nimeagiza watendaji wangu wamwachie kwa dhamana yaani ajidhamini yeye mwenyewe na awe anakuja kuripoti,” amesema Mambosasa

Kamanda huyo ametoa kauli hiyo mara baada ya Mwananchi kumtafuta kutaka kujua hatima ya Dk Shika ambaye ameshikiliwa tangu Novemba 9 akituhumiwa kuvuruga mnada wa nyumba za kifahari za mfanyabishara Said Lugumi

Dk Shika tangu siku hiyo amekuwa gumzo sehemu mbalimbali kutokana na kile alichokifanya siku ya mnada alipokuwa akipandisha bei dhidi ya washindani wake na moja ya kauli zake zinaendelea kutumika hadi sasa ni ‘Mia 900 itapendeza.’

Chanzo: Mwananchi
Ianzishwe harambee ya kumchangia nauli ya kwenda polisi daily. Kwenda na kurudi 900 itapendeza zaidi!!
 
Mara imetokea Paap Dr. Shika kapewa bonge la shavu, mtaona jinsi ndugu zake wanavyoibuka na kujifanya kumjali. Kuna watu watamfungashia Senene na sato na kumletea toka huko kanda ya ziwa.

Watanzania wanafiki sana. Ndiyo walijitokeza kwa wingi kumzika yule mbakaji pale kinondoni makaburini huku wakiongozwa na rais na baraza lake la mawaziri, na serikali nzima huku kale kabint kalikokua kakibakwa kakiwa ndani nyuma ya nondo za mahabusu
 
Mara imetokea Paap Dr. Shika kapewa bonge shavu, mtaona jinsi ndugu zake wanavyoibuka na kujifanya kumjali. Kuna watu watafungashia Senene na sato na kumletea toka huko kanda ya ziwa.
Watanzania wanafiki sama. Ndiyo walijitokeza kwa wingi kumzika yule mbakaji pale kinondoni makaburini huku wakiongozwa na rais na baraza lake la mawaziri, na serikali mzima huku kale kabint kalikokua kakibakwa kakiwa ndani nyuma ya ndindo za mahabusu
Mkuu Kanumba alikugongea nini?
 
Back
Top Bottom