Polisi yakamata watuhumiwa tisa wa ujambazi Dar es Salaam

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,801
11,961
1658506652702.png

Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa tisa (9) kwa tuhuma za kujihusisha na matukio ya ujambazi. Tukio hilo limetokea Tarehe 22/07/2022 majira ya saa 9:40 usiku maeneo ya kiwanda cha SHERI Automotive Germany Barabara ya Mbozi Keko Wilaya ya Temeke.

Jeshi la Polisi lilipata taarifa ya kuwepo kwa wahalifu hao eneo hilo na kufika haraka eneo la tukio, Baada ya kufika wahalifu hao ambao walikuwa wamejihami kwa bunduki aina ya bastola na mapanga walianza kuwashambulia askari Polisi kwa risasi lakini wakadhibitiwa baada ya kujeruhiwa kwa risasi wakati Polisi wakijihami kuwakamata.

Baada ya kupekuliwa watuhumiwa hao, walikutwa na bastola moja iliyofutwa namba ikiwa imebakia na risasi tatu, na silaha za jadi mapanga manne na funguo nyingi aina mbalimbali za kufungulia magodown na ofisi za kiwanda hicho, Wahalifu hao pia wakiwa ndani ya godown hilo walikutwa wakiwa na gari No. T 201 DXN HIACE ikiwa tayari imemekwisha pakiwa mali za wizi box zaidi ya 70 za

vipuri, Wahalifu hao baadhi yao wamepelekwa hospitali kwa matibabu na baada ya kupata nafuu wataendelea kuhojiwa kwa kina juu ya tukio hilo. Wito wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam ni kutoa onyo na tahadhali kuwa wahalifu waache kujihusisha na vitendo vilivyo kinyume na sheria kwani Polisi Dar es salaam tayari wamemsikia na kumuelewa Mkuu mpya wa Jeshi la Polisi nchini kuwa na anawataka askari watumie mbinu zote kuzuia na kukabiliana na vitendo vya kihalifu huku wakizingatia haki na sheria.

Muliro J. MULIRO – ACP

KAMANDA WA POLISI KANDA MAALUM DAR ES SALAM.
 
Hao walikuwa wamekula deal na walinzi sema kuna muhuni kachomoa betri
Kibongo tunamuita snitch! Kawaharibia wana hivi hivi.

Haya ndiyo moja ya mambo ya siri za biashara. Unajiuliza mbona jamaa anajenga tu majumba halafu duka lake la spea ni dogo kuliko hili la kwangu?

Kumbe wenzako usiku hawalali. Kwenye biashara nyingi, bila kupita njia ya mkato, hutoboi.
 
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa tisa (9) kwa tuhuma za kujihusisha na matukio ya ujambazi. Tukio hilo limetokea Tarehe 22/07/2022 majira ya saa 9:40 usiku maeneo ya kiwanda cha SHERI Automotive Germany Barabara ya Mbozi Keko Wilaya ya Temeke.

Jeshi la Polisi lilipata taarifa ya kuwepo kwa wahalifu hao eneo hilo na kufika haraka eneo la tukio, Baada ya kufika wahalifu hao ambao walikuwa wamejihami kwa bunduki aina ya bastola na mapanga walianza kuwashambulia askari Polisi kwa risasi lakini wakadhibitiwa baada ya kujeruhiwa kwa risasi wakati Polisi wakijihami kuwakamata.

Baada ya kupekuliwa watuhumiwa hao, walikutwa na bastola moja iliyofutwa namba ikiwa imebakia na risasi tatu, na silaha za jadi mapanga manne na funguo nyingi aina mbalimbali za kufungulia magodown na ofisi za kiwanda hicho, Wahalifu hao pia wakiwa ndani ya godown hilo walikutwa wakiwa na gari No. T 201 DXN HIACE ikiwa tayari imemekwisha pakiwa mali za wizi box zaidi ya 70 za

vipuri, Wahalifu hao baadhi yao wamepelekwa hospitali kwa matibabu na baada ya kupata nafuu wataendelea kuhojiwa kwa kina juu ya tukio hilo. Wito wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam ni kutoa onyo na tahadhali kuwa wahalifu waache kujihusisha na vitendo vilivyo kinyume na sheria kwani Polisi Dar es salaam tayari wamemsikia na kumuelewa Mkuu mpya wa Jeshi la Polisi nchini kuwa na anawataka askari watumie mbinu zote kuzuia na kukabiliana na vitendo vya kihalifu huku wakizingatia haki na sheria.

Muliro J. MULIRO – ACP

KAMANDA WA POLISI KANDA MAALUM DAR ES SALAM.
Hivi wahalifu wakiacha kazi hiyo polisi, magereza, wapishi, wanasheria na vinyozi watakosa ajira.
 
Back
Top Bottom