Polisi yakamata magunia 64 ya bangi bila watuhumiwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Polisi yakamata magunia 64 ya bangi bila watuhumiwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pdidy, Nov 9, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Nov 9, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,132
  Likes Received: 5,571
  Trophy Points: 280
  NINI MAONI YAKO?

  Moses Mashalla, Arusha

  JESHI la Polisi Mkoani Arusha limeendesha operesheni ya kukamata dawa za kulevya aina ya bangi wilayani Arumeru mkoani Arusha na kufanikiwa kukamata magunia 64 ya bangi ambapo kila gunia moja lina zaidi ya kilo 100 za bangi iliyohifadhiwa.

  Akizungumza na waandishi wa habari jana ofisini kwake Kaimu Kamanda wa jeshi hilo ambaye pia ni Mkuu wa upelelezi mjini hapa, Leonard Paul alisema bangi hiyo ilikamatwa katika vijiji viwili tofauti vya Kisimiri Juu na Lesenoni wilayani Arumeru.

  Alisema operesheni hiyo ilianza juzi saa 7:00 mchana na kumalizika saa 2:30 usiku wa kuamkia jana ambapo jeshi hilo lilikamata magunia hayo yaliyokuwa yamehifadhiwa katika nyumba za watu mbaimbali kijijini hapo humo.

  Kaimu kamanda huyo alibainisha kwamba magunia hayo ya bangi yalikuwa mbioni kusafirishwa kuelekea katika nchi za jirani na kusema katika operesheni hiyo jeshi hilo
  halikufanikiwa kumkamata mhusika yoyote katika tukio hilo.

  "Magunia hayo ya bangi yalikuwa yamehifadhiwa majumbani mwa watu katika vijiji hivyo hata hivyo tumebaini kwamba bangi hiyo ilikuwa mbioni kusafirishwa kuelekea nchi za jirani," ┬Łalisema Leonard.

  Akizungumzia changamoto katika operesheni hiyo, Leornad alisema polisi haikifanikiwa kuwakamata wahusika kutokana na wakazi wengi kuyakimbia makazi yao mara baada ya kubaini polisi kuanza operesheni hiyo.

  Hata hivyo, alisema kwa sasa bangi hiyo imehifadhiwa katika chumba maalumu katika kituo kikuu cha polisi kati ikisubiri kuteketezwa huku mkakati uliopo sasa ukiwa kuwatafuta wahusika wake.

  Katika tukio jingine jeshi hilo hilo limefanikiwa kuteketeza mashamba mawili ya mirungi yaliyopo katika kijiji cha Losirwa wilayani Longido . Kaimu kamanda huyo aliwaambia waandishi wa habari kwamba mashamba hayo yaliteketezwa katika operesheni iliyofanyika juzi wilayani humo ambapo mbali na hayo jeshi lake lilifanikiwa kuwakamata watuhumiwa wawili wamiliki wa mashamba hayo.
   
 2. Mndundu

  Mndundu JF-Expert Member

  #2
  Nov 9, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 225
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Hiyo mbona simpo tu, wamuulize mwenyekiti wa kijiji nani anakaa kwenye nyumba fulani? kama hajui uongozi wa kijiji lazima useme nani alikuwa anaishi hapo au hata majirani wanaweza saidia.

  Kwanini wasiweke mlinzi kwenye hizo nyumba hadi mtu atakapotokea? Kwani walikuwa wanaharaka gani kutangaza kabla hawajawapata hao wahalibifu?

  Sema kwasababu hio dili na wao wamo ndio maana wanatuletea habari za ajabu ajabu kama hizi.
   
Loading...