dubu
JF-Expert Member
- Oct 18, 2011
- 3,500
- 3,481
Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam, Hebel Mhanga.
wafanyakazi waliosimamishwa katika Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA), kwa tuhuma za kutorosha makontena 11,019 kutoka bandari kavu (ICD) na magari 2,019, wakiongezeka na kufikia 25, Jeshi la Polisi bado limekuwa na kigugumizi cha kuwafikisha mahakamani baadhi ya watuhumiwa hao.
Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam, Hebel Mhanga, aliliambia gazeti hili mwishoni mwa wiki kuwa, jumla ya wafanyakazi 25 wameshasimamsihwa kazi kwa shutuma hizo na wamekabidhi polisi ushahidi wa nyaraka zilizotumiwa na wafanyakazi hao kufanikisha uhalifu uliofanyika.
Alisema wanatarajia watumishi hao watafikishwa mahakamani upepelezi wa mashauri yao utakapokamilika na kwamba bandari itaendelea kutoa ushirikiano kwa mamlaka husika kila itakapoombwa kufanya hivyo.
Alisema kwa upande wao, bandari imejitahidi kutoa nyaraka zote inazooombwa na Polisi kwa ajili ya upelelezi hivyo hawezi kujua ni kwanini watuhumiwa hao bado hawajafikishwa mahakamani.
“Polisi wamekuwa wakituomba ushahidi na tunawapa nyaraka zote muhimu wanazohitaji kwa ajili ya upelelezi na kama watajitaji nyaraka zingine sisi tuko tayari wakati wowote kuwapatia ili kuharakisha upepelezi wao,” alisema Mhanga.
Meneja huyo alikiri kuwa upelelezi huo umechukua muda mrefu kwasababu uchunguzi wa kesi za kughushi ni mgumu.
“Sisi tunao ushahidi kwamba watumishi tuliowasimamisha walikula njama za kusaidia uhalifu ufanyike, maana huwezi kuruhusu mzigo utoke kama hujajiridhisha kwenye 'system' kwamba kweli malipo yamefanyika ndipo utoe ruhusa," alisema Mhanga.
"Kuna ujanja ujanja ulikuwa ukifanyika na sisi tumeugundua ndiyo sababu tumewasimamisha.”
Nipashe ilimtafuta Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Biswalo Mganga lakini hata hivyo alikataa kuzungumzia suala hilo limefikia wapi, akisema maadili ya kazi yake hayamruhusu kutoa taarifa kama hizo kwenye vyombo vya habari.
“Kama taaluma yako ilivyo na miiko na taaluma ya waendesha mashitaka na wapelelezi ina miiko yake pia, huwezi kutoa taarifa kama hizo kabla hazijakamilka," alisema Mganga.
"Msiwe na haraka mtaambiwa tu mambo yatakapokuwa tayari… jana (juzi) mahakamani si mmeona kilichotokea?
"Basi subirini mambo yakiwa tayari mtaona tu acheni haraka zenu.”
Biswalo alizungumzia kilichotokea mahakamani juzi akirejea watuhumiwa watatu waliofikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu, akiwemo aliyekuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato (TRA), Harry Kitilya kwa tuhuma za kutakatisha Sh. trilioni 1.3.
Fedha hizo ziligundulika kuwa 'cha juu' katika mkopo wa hati fungani wa serikali kutoka benki ya Standard ya Uingereza.
Hivi karibuni, wafanyakazi wengine saba wa Mamlaka ya Bandari walikamatwa kwa tuhuma za kuipotezea Serikali mapato ya Sh. bilioni 48.55.
Kaimu Maneja Mawasiliano wa TPA, Janeth Ruzangi alisema hivi karibuni kuwa mfanyakazi mmoja hajapatikana na polisi wanaendelea kumsaka ili afikishwe kwenye vyombo vya sheria.
“Wote walishapatikana kasoro mtumishi mmoja, Happygod Naftali, ambaye huyu alishaacha kazi siku nyingi baada ya viongozi kuanza kufuatilia suala hilo. Lakini bado polisi wanaendelea kumsaka,” alisema Ruzangi.
Naye Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro alithibitisha kukamatwa kwa watuhumiwa hao hivi karibuni na kwamba bado wanaendelea kuhojiwa kuhusu tuhuma hizo.
Watumishi waliokamtwa na polisi, kwa mujibu wa Ruzangi ni Aron Lusingu, Amani Kazumari, John Mushi, Valentine Sangawe, Bonasweet Kimaina, Zainab Bwijo na Nathan Edward.
Watumishi hao waliungana na watumishi wengine saba John Elisante, Leticia Masaro, Christina Temu, Merina Chawala, Adnan Ally, Masoud Seleman (Kova) na Benadeta Sangawe waliokamatwa na kuhojiwa kuhusu sakata hilo.
Watumishi hao saba, kwa mujibu wa Sirro, tayari walishapelekwa mahakamani.
“Ukiacha wale saba ambao tumeshawafikisha mahakamani, hawa wengine bado tuko nao tunaendelea kufanya upelelezi,” alieleza.
Tangu Rais John Magufuli aingie madarakani, uongozi wake umeibua ufisadi wa kutisha ambao ulikuwa unafanywa Bandari ya Dar es Salaama kwa kuwashirikisha wafanyakazi wa TPA na mawakala pamoja na wafanyakazi wa TRA.
Kwa mara ya kwanza utoroshaji wa makontena 349 uligundulika baada ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kutinga bandarini na kubaini makontena hayo kutolewa bandari kavu bila kulipiwa kodi.
Upotevu huo ulifanya vigogo wa TRA, akiwemo Kamishna Mkuu Rished Bade na makamishna wengine kusimamishwa kazi na wengine kufikishwa mahakamani.
Baadaye Majaliwa alibaini kupitishwa makontena 2,431 yaliyoondolewa bandari kavu bila kulipiwa ushuru wa Bandari.
Katika sakata hilo, baadhi ya mawakala wa forodha walifungiwa kufanya biashara na TPA na sakata la mwisho ni la kutoroshwa makontena 11,019 na magari 2,019 bila kulipiwa ushuru.
Chanzo: Nipashe