Polisi yainyima kibali Chadema cha kuaga maiti NMC | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Polisi yainyima kibali Chadema cha kuaga maiti NMC

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Jan 10, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Jan 10, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  VIONGOZI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Polisi mkoani Arusha wameingia katika msuguano kuhusu mahali pa kuagia watu wawili waliouawa katika vurugu za
  maandamano.

  Wakati Mwenyekiti wa Mkoa wa Chadema, Samson Mwigamba akisisitiza shughuli hiyo kufanyika katika uwanja wa NMC, inadaiwa Polisi iko tayari kutoa kibali cha sehemu nyingine lakini sio NMC.

  Mwigamba alidai jana kuwa kibali cha Polisi kimekubaliwa lakini sehemu ya kuaga inaleta utata mpaka sasa lakini akaelezea matumanini yake kuwa katika muda mfupi ujao, utapatiwa ufumbuzi.

  Kiongozi huyo aliahidi kwenda ofisini kwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Thobias Andengenye kuzungumza naye kwa kina, ili amfafanulie sababu za chama hicho kupendekeza ibada hiyo ifanyike katika uwanja huo.

  ‘’Andengenye niliongea naye katika simu juu ya kufanya ibada katika uwanja wa NMC, lakini alionesha kukataa na kushauri twende eneo lingine.

  “Sisi tumesema haitawezekana kwani pale kuna heshima yake kwa vyama vya upinzani na ndio maana nikamwambia nitakwenda kwake,’’ alidai Mwigamba.

  Katibu huyo alisema hata hivyo Chadema haihitaji ulinzi wa Polisi katika ibada hiyo, ila imetoa taarifa ya kuwepo kwa mkusanyiko wa watu ambao wana lengo la kufanya ibada na si vinginevyo.

  Alisema haamini kama Polisi watakuja katika msiba na mabomu kwani eneo hilo kesho litakuwa na majonzi kwa wakazi Mkoa wa Arusha na mikoa mingine ya jirani.

  ‘’Nafikiri hata polisi siku hiyo hawahitajiki, wao wakae huko huko waliko na watuachie sisi tumalize kufanya ibada ya kuwaombea marehemu na halafu wakazikwe,’’ alisema.

  Kamanda Andengenye alipopigiwa simu ili kupata ufafanuzi zaidi, simu yake ya mkononi ilipokewa na msaidizi wake ambaye hakutaka kujitambulisha jina, akadai kuwa kamanda huyo yuko katika kikao hivyo hawezi kuzungumza.

  Wakati huo huo majeruhi wawili waliojeruhiwa kwa risasi katika vurugu za Januari 5 mwaka huu kwa kupigwa risasi, wamehamishiwa katika hospitali ya rufaa ya KCMC kwa matibabu zaidi baada ya hali zao kuwa mbaya.

  Majeruhi hao ni Frank Joseph na Fredrick Elia ambao Chadema imewapeleka katika hospitali hiyo baada ya madaktari wa hospitali ya Mkoa ya Mount Meru kutoa ushauri huo.
  HabariLeo | Polisi yainyima kibali Chadema cha kuaga maiti NMC
   
 2. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #2
  Jan 10, 2011
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Hawa polisi wana matatizo gani?
   
 3. s

  seniorita JF-Expert Member

  #3
  Jan 10, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 674
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Pathetic, frustrating, a system full of fear....hata mahali pa kuaga maiti ni malumbano, jamani nchi imekosa kabisa mwelekeo hasa the so called polisi, wamekuwa kweli polisi wa ccm
   
 4. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #4
  Jan 11, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Ieleweke kabisa kuwa kazi ya polisi ni kulinda usalama na si kuamulia watu ni wapi wanapaswa kukusanyika.
   
 5. JoJiPoJi

  JoJiPoJi JF-Expert Member

  #5
  Jan 11, 2011
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 2,471
  Likes Received: 1,424
  Trophy Points: 280
  Yanini malumbano hadi mazishini, hawa polisi soon watapata wanachotaka!! Haaa tumechoka kuwavumilia sasa
   
 6. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #6
  Jan 11, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Human beings must have action; and they will make it if they cannot find it.

   
 7. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #7
  Jan 11, 2011
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Chadema wapeleke hizo maiti uwanjani kama police wanataka wazipige mabomu na hizo maiti!
   
 8. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #8
  Jan 11, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,971
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Naunga mkono kwa asilimia 100 kwani hao maiti watasababisha nini au wanaogopa kuona uovu walioutenda. Watakosa amani mpaka wafe
   
 9. S

  Somi JF-Expert Member

  #9
  Jan 11, 2011
  Joined: Feb 7, 2009
  Messages: 579
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Polisi mujue sisi wananchi ndio tumewaajiri na tunawalipa mshahara kwa kodi zetu . huu uovu munaofanya mpaka wa kudhalilisha waombolezaji eti kwakuwa ni chadema utazidi kuleta machungu na kuchochea uadui mkubwa.
   
 10. seniorgeek

  seniorgeek JF-Expert Member

  #10
  Jan 11, 2011
  Joined: Sep 18, 2008
  Messages: 500
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Kama vipi, wachague Stadium. Tena pale ndio itakua bomba zaidi.
   
 11. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #11
  Jan 11, 2011
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  kweli hawapolic wamelewa madaraka kwa mtajhg wanataka sisi maboc waow tuwachukulie hatua
   
 12. M

  MONTESQUIEU JF-Expert Member

  #12
  Jan 11, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 847
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mungu awalaze pema marehemu!
   
 13. M

  Mpendagiza Member

  #13
  Jan 11, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 37
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ndo aana wanakufa maskini na roho zao mbaya,na watakaaa ktk vijumba vya bati hadi wafe pumbavu zao
   
 14. M

  MzeePunch JF-Expert Member

  #14
  Jan 11, 2011
  Joined: Jun 8, 2009
  Messages: 1,412
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Mbona huyu Saidi Mwema alipopata cheo alitamba kwamba atalibadilisha jeshi la polisi liwe la kisasa zaidi? Sasa nini anafanya huyu afande? Anakuwa kama hajasoma bwana! Hii inaudhi sana. I hate cops!
   
Loading...