Polisi yahojiwa kutengeneza helicopta kwa Sh 1.2 bn | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Polisi yahojiwa kutengeneza helicopta kwa Sh 1.2 bn

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by fangfangjt, Apr 2, 2011.

 1. fangfangjt

  fangfangjt JF-Expert Member

  #1
  Apr 2, 2011
  Joined: Apr 25, 2008
  Messages: 571
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 33
  Polisi yahojiwa kutengeneza helicopta kwa Sh 1.2 bn

  Exuper Kachenje
  WABUNGE wa Kamati ya Hesabu za Serikali, wamehoji matengenezo ya helkopta moja ya jeshi la Polisi kugharimu zaidi ya Sh 1,189,790,560 (dola za Marekani 849,850.4).

  Mbali ya kiasi hicho kikubwa cha fedha, wabunge hao wamehoji pia hasara ya zaidi ya Sh 560milioni (dola 400,000) iliyotokana na kucheleweshwa kulipwa kwa gharama za awali za matengenezo ya helkopta hiyo ambazoawali, zilikadiriwa kuwa Sh 774,178,342 (dola 552,984.53).

  Helkopta hiyo aina ya Bell 206L namba 5H-PAW, ilipelekwa Afrika Kusini kwa matengenezo, miaka miwili iliyopita ikiwa ni miaka minne tangu iliponunuliwa mwaka 2006.

  Wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Zainab Vullu, Wabunge Stephen Masele (Shinyanga Mjini) na Ali Mohamed Kessy (Nkasi Kaskazini), walikuwa mstari wa mbele kuwabana polisi ambao katika kikao hicho, waliongozwa na Mkuu wa Jeshi hilo, Inspekta Jenerali Said Mwema na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil.

  Walikuwa wakijadili taarifa ya ukaguzi wa fedha za jeshi hilo za mwaka ulioishia Juni 30, 2009.

  Hata hivyo, taarifa za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), zinaonyesha kuwa hakuna uhakika kama matengenezo husika, yamefanyika kwa kuwa hakuna taarifa za kiufundi za kuthibitisha hilo wala uhalali wa kufanyika malipo hayo.

  Mhasibu wa Jeshi hilo, Frank Msaki alisema kuwa hati ya kuthibitisha matengenezo ya helkopta hiyo, itapatikana baada ya kukamilika kwa matengenezo na kwamba kuchelewa kukamilika kunatokana na uhaba wa fedha. Alisema juhudi za kupata fedha hizo kutoka Hazina zinaendelea.

  Wabunge hao walisema fedha zinazotumika kwa matengenezo ya helkopta hiyo ni nyingi na kushauri iuzwe na kununuliwa helkopta nyingine.

  Kamishna wa Polisi, Coldwig Tweve alisema polisi ilituma ombi maalumu la fedha Hazina, ili kulipa madeni yake pamoja na deni hilo la helkopta lakini hawajajibiwa.

  Alisema helkopta hiyo ilinunuliwa mwaka 2006 kwa Sh5 bilioni na kwambab hivi sasa bei ya helkopta mpya ya aina hiyo imefikia Sh8.49 bilioni.

  Hata hivyo, taarifa ya CAG inaonyesha kuwa kati ya mwaka 2005/2006, polisi ilifanya matumizi ya ziada ya Sh284,265,206 bila ruhusa ikiwamo kufanya manunuzi ya Sh253,603,293. |Msaki alisema walipeleka ombi maalumu Hazina ili waruhusiwe kutumia pesa hizo pamoja na kufanya manunuzi hayo. Polisi inadaiwa zaidi ya Sh26.5 bilioni na askari wake pamoja na wazabuni.

  Kamishna Msaidizi wa Bajeti, Wizara ya Fedha, Ramadhani Hamisi alisema Hazina itawasilisha katika kikao kijacho cha Bunge, hati ya matumizi hayo ya dharura.

  Inspekta Jenerali Mwema alisema helkopta hiyo ilinunuliwa ili kusaidia utendaji wa kazi za jeshi hilo na kwamba kuharibika kwake kunakwaza utendaji wao wa kazi.
   
 2. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #2
  Apr 2, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  WABUNGE wa Kamati ya Hesabu za Serikali, wamehoji matengenezo ya helikopta moja ya jeshi la Polisi kugharimu zaidi ya sh 1, 189,790,560 (dola za Marekani 849,850.4). Mbali ya kiasi hicho kikubwa cha fedha, wabunge hao wamehoji pia hasara ya zaidi ya sh 560 milioni (dola 400.000) iliyotokana na kucheleweshwa kulipwa gharama za awali za matengenezo ya helikopta hiyo ambayo awali, zilikadiriwa kuwa sh 774,178,342 (dola 552,984.53)
  Helikopta hiyo aina ya Bell 206L namba 5H-PAW,ilipelekwa Africa Kusini kwa matengenezo, miaka miwili iliyopita ikiwa ni miaka minne tangu iliponunuliwa mwaka 2006 kwa Sh 5 bilioni, kwa sasa bei ya helikopta mpya ya aina hiyo imefikia Sh 8.49 bilioni.
  SOURCE: Mwananchi Aprili 2, 2011
   
 3. Ngisibara

  Ngisibara JF-Expert Member

  #3
  Apr 2, 2011
  Joined: Jan 2, 2009
  Messages: 2,083
  Likes Received: 431
  Trophy Points: 180
  Je walihoji kama iliponunuliwa ilikuwa kama Dowans?
   
 4. Ngisibara

  Ngisibara JF-Expert Member

  #4
  Apr 2, 2011
  Joined: Jan 2, 2009
  Messages: 2,083
  Likes Received: 431
  Trophy Points: 180
  Ilitengenezwa mwaka 1979 na kama kweli ilinunuliwa 2006 basi ilikuwa mtumba

  5H-PAW
  260
  22/12/1979TANZANIA POLICE AIRWING P.O.BOX 18006 DAR-ES-SALAAM BELL 206L-1
  45292
  19794250 / 1928GENERAL AVIATIONALLISON 250-028B


  Angalia uthibitisho wa TCAA

  Aircraft Particulars
  Reg:
  5H-PAW
  C of R Number:
  260
  Manufacturer:
  KILIMANJARO AERO CLUB
  Type:
  BELL 206L-1
  Serial Number:
  45292
  Year of Manufactured:
  1979
  Name of Owner:
  TANZANIA POLICE AIRWING
  Operator:
  Address:
  P.O.BOX 18006 DAR-ES-SALAAM
  Date of Issue of C of R:
  22/12/1979
  Category:
  GENERAL AVIATION
  Type of Engine(s)/Propeller:
  ALLISON 250-028B
  All Up Mass (IBS/KGS):
  4250 / 1928
  C OF A EXPIRY DATE :
  26/11/2006

  Naamini na hayo malipo ni mtumba
   
 5. Ngisibara

  Ngisibara JF-Expert Member

  #5
  Apr 2, 2011
  Joined: Jan 2, 2009
  Messages: 2,083
  Likes Received: 431
  Trophy Points: 180
  Si bora wangenunua hii kuliko kwenda kulipa Billion kwa mtumba ule

  [​IMG]For Sale - $375,000, N617TT; 8106 TT; Nice Bell Jet Ranger B II with great component times remaining and 530 Garmin-Current and ready for work or pleasure. Seller wants it gone by mid March. USA Jet & Helicopter
  Phone: (843)492-7828
  or (843)361-8400
  Fax: (843)361-8402


   
Loading...