Polisi Nigeria yabaini jengo la kuzalisha wasichana na kuuza watoto kimagendo

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,000
9,862
Polisi nchini Nigeria jimbo la Ogun limewakamata washukiwa wawili katika jengo ambalo linatumika kushikilia wasichana na kuwatunga mimba, vilevile watoto wanaozaliwa kuuzwa kimagendo.

Msemaji wa polisi katika jimbo hilo Abimbola Oyeyemi amesema msichana aliyelaghaiwa na mmoja wa waendeshaji jengo hilo alifanikiwa kutoroka na kuripoti kisa hicho kwa polisi.

Maafisa waliovamia jengo husika walinusuru wasichana 10, wanne kati yao tayari wakiwa wajawazito, kuligana na taarifa za TVC.

Mmoja wa waliokamatwa ni msichana wa mwanamke anayesimamia jengo hilo.

Mwanamke huyo alishitakiwa kwa makosa ya ulanguzi wa binadamu na kuachiwa kwa dhamana.

Mshukiwa mwingine ni mlemavu ambaye polisi wanashuku huenda ndiye aliyewatia mimba wasichana walionusuriwa. Maeneo kama hayo hutumika kulaghai wasichana na kuwazalisha watoto ambao huuzwa kwa njia ya magendo.
 

Attachments

  • 1606908077036.gif
    1606908077036.gif
    42 bytes · Views: 1
Alishtakiwa kwa makosa ya ulanguzi wa Binadamu "na kuachiwa kwa dhamana" hii ndo Africa palipojaa rushwa ....ajira ajira ajira ajira
 
Alishatakiwa kwa makosa ya ulanguzi wa Binadamu "na kuachiwa kwa dhamana" hii ndo Africa palipojaa rushwa ....ajira ajira ajira ajira
Mpinzani akishtakiwa ni uhujumu uchumi ila mambo ya msingi kabisa kama haya ni dhamana!
 
..Dah!...biashara haramu ya watoto hiyo, watu wanajali faida kuliko utu.
 
Hapo si ajabu kuna waliokufa na maiti kutupwa maana ujauzito na mazingira kama hayo yssiyo na huduma nzuri ni hatari.....bado mtu anapewa damana kirahisi kabisa
 
Back
Top Bottom