Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,899
Jeshi la Polisi Wilayani Geita mkoani humo linatuhumiwa kuhusika na mauaji ya kijana aliyekuwa mlizi wa kampuni ya Jerusalemu Security Ltd. ambaye ni mkazi wa mtaa wa Mwatulole kata ya Buhalahala Mjini Geita anayedaiwa kufariki dunia katika mazingira ya kutatanisha.
Kifo cha kijana huyo aliyefahamika kwa jina la Baraka Vitalis mwenye umri wa miaka 23 kimetokea wakati ndugu na kaka yake wakihaha kumtafuta katika kituo cha polisi, ambapo imeelezwa kabla ya uamuti marehemu alikamatwa Novemba 8 2018 majira ya saa 12 jioni katika eneo la nyumbani kwake na kupelekwa kituo cha Polisi Geita kwa tuhuma za wizi baada ya kutajwa na wenzake 10 wanaoshikiliwa na jeshi hilo ambapo majira ya saa tatu usiku alifikishwa katika hospitali ya rufaa akiwa amefariki.
Polisi Mkoani humo imekiri kutokea kwa kifo cha Baraka lakini imesema mpaka sasa inaendelea na uchunguzi wa tukio hilo ili kubaini chanzo cha kifo.