Polisi wetu na visingizio vya taarifa za kiintelijensia. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Polisi wetu na visingizio vya taarifa za kiintelijensia.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Omumura, Jan 5, 2011.

 1. O

  Omumura JF-Expert Member

  #1
  Jan 5, 2011
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mara kadhaa utawasikia viongozi wa jeshi la polisi wakitoa kauli zenye utata ili kuzuia ama maandamano au mikutano ya kisiasa ya wananchi eti wamepata taarifa za kiintelijensia juu ya uvunjifu wa amani kitu ambacho mara nyingi ni propaganda tu ya kuzuia haki za msingi za wananchi. Nchi hii ina safari ndefu hadi kufikia kilele cha demokrasia ya kweli.

  Leo hii makamba anao uwezo wa kumpigia simu IGP ili azuie maandamano au mkutano wa wapinzani naye bila ajizi ataita press conference kwa mbwembwe na kusema kwamba taarifa za kiintelijensia zinaonesha kutakuwa na vurugu kumbe ni cooked story originated from makamba!!!
   
 2. m

  mafutamingi JF-Expert Member

  #2
  Feb 24, 2012
  Joined: Feb 14, 2011
  Messages: 859
  Likes Received: 172
  Trophy Points: 60
  Imekuwa kawaida ya Jeshi la Polisi kuzuia maandamano ya vyama za siasa kwa kisingizio kwamba kutokana na taarifa za kiintelijensia walizonazo fujo itatokea.

  Hii ilitokea Januari 2011 huko Arusha ambapo watu 3 walifariki. Watu wengi wamekuwa wakisema kwa uhakika kwamba Jeshi la Polisi lina mapungufu mengi na halina utaalamu wala uelewa wa kukabiliana na maandamano.

  Je katika haya mauaji ya Songea Jeshi la Polisi lilipata taarifa za kiintelijensia? Mbona sijasikia Polisi waki wakizingumzia hicho wanachokiita taarifa za kiintelijensia? Au taarifa hizo huwa wanakuwa nazo tu wakati vyama vya siasa vya upinzani hasa CHADEMA wanapokuwa wanataka kufanya maandamano?
   
 3. MchukiaUonevu

  MchukiaUonevu JF-Expert Member

  #3
  Feb 24, 2012
  Joined: Feb 17, 2012
  Messages: 207
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Wanaweza kuwa nazo au wasiwe nazo, na hiyo hatuwezi ku-conclude kuwa jeshi la polisi halifai au hawafanyi kazi yao!

  Hawa ni binadamu kama sisi, hawana ukatili kiasi wanachosemwa, stop calling them bad names and demoralizing languages to them,these guys are working in a very difficult environment and yet they are among the least paid workers in this country. So far there's a lot of improvements kwenye jeshi la polisi chini ya Inspekta Jenerali Mwema.

  Maandamano hapa kwetu hasa ya vyama vya siasa (kwa uzoefu wangu) huwa ni vurugu,tofauti na hizo nchi tunazochukua reference.

  Hata kama kuandamana ni haki ya kiraia, lakini haikuweki juu ya sheria dhidi ya yule asiyetaka maandamano.
   
 4. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #4
  Feb 24, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  Wewe ni kaburu tu hata kama ni mweusi, ni kaburu tu!!!!!
   
 5. MchukiaUonevu

  MchukiaUonevu JF-Expert Member

  #5
  Feb 24, 2012
  Joined: Feb 17, 2012
  Messages: 207
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Mkuu kama umeona ndio tusi linalonifaa its ok, it will never stop me from criticizing when i have to!
   
Loading...