Game Theory
JF-Expert Member
- Sep 5, 2006
- 8,545
- 799

SADI YAKUBU ANASEMA HIVI:
Picha hapo juu inaashiria utumiaji wa nguvu kubwa kuliko ''kosa'' lenyewe. Wanakijiji wameandamana kuomba wenzao waachiliwe, wakitaka maelezo ya msingi ya kukamatwa kwa wenzao, wana kilio cha msingi kuhusu fukuzwa fukuzwa kwenye ardhi yao. Kuna manung'uniko ya msingi hapa, kilichohitajika ni maelezo na mtu mwenye mamlaka kuzungumza nao sio kipigo.
Pichani Askari Kanzu husika ana bunduki mkono mmoja, bakora mkono mwingine, kama mpiga picha anavyoeleza kuwa huyu mama anafukuzwa huku akicharazwa viboko, huu ndio utaratibu bora kweli kwa kumkamata mwanamama huyu au ilikuwa lazima ''kumuadabisha''?
Wakati mwingine hujiuliza tunaitwaje kisiwa cha amani wakati kuna haya yanatokea....
http://www.saidiyakubu.blogspot.com/