Polisi wetu na sheria mkononi-- picha ya Tundu Lisu

Mbona hapo haionyeshi akipewa mkong'oto? Natamani sana hao CDM wapewe kichapo cha maana cuz wanatuvurugia amani yetu! Big up Kamanda Masawe, unafanya kaz yako vizuri!
Hahahaha....! Mnavyoumbuana Arusha nawapongezeni sana, lakini sio kwa hili.....!
 
Inatia hasira sana kuona kiongozi halali wa wananchi, na mtunga sheria ndani ya bunge la Jamhuri anadhalilishwa kwa misingi ya kichama. Polisi nao imefika wakati watumie hata elimu ya utu wa mtu. Mbunge sio jambazi hawezi kimbia wala jificha, lazima atakamatwa, kwa nini kumdhalilisha ?

Hapo najifunza je kama mti mbichi unawaka moto mkavu utakuwaje? Gharama za kuwa mpinzani ni kubwa, gharama za kuitoa CCM ni kubwa na gharama za kutetea mali za Tanzania ni kubwa mno. Hya wananchi twende kazi.
ndo tatizo la hawa watoto wa darasa la saba na div four na ziro...polisi wengi ni failure understanding capacity yao ni ndogo sana ndio maana wanatumia nguvu tu bila akili..shame on them.
 
Tundu Lisu na wenzako, msichoke, hamko wenyewe kuna kundi nyuma yenu. Stephano alipokuwa anapigwa mawe aliinua macho mbinguni akaona kundi la malaika na mlango wa mbinguni umefunguka kwa ajili yake kulipigania Jina la Yesu. Kuna kundi kubwa linalowaangalia na kuwaombea nguvu, amani na ulinzi (siyo wa mabundi na askari wa nyama). Imefika hatua Viongozi serikalini wajitafakari sana kuhusu laana itakayowapata kutupa maiti barabarani!!! na wamekaa kimya. Kukaa kimya nalo ni JIBU
Mungu aliyetupa Tanzania na raslmali zilizoko na akawaleta akina Tundu Lisu katika kipindi hiki - Atatupigania na kutuvusha kama alivyowavusha wale wana wa Israel. Yoel 3:2
 
Tabia kama hizi za polisi zilishamiri sana Afrika Kusini, nakumbuka nilipokuwa kule miaka ya tisini serikali ilikuwa inawakataza polisi wasitumie nguvu kupita kiasi lakini ilikuwa haifanyiki ndipo wananchi wakaanzisha mkakati. Mkakati wenyewe ni kumtambua polisi ambaye anakiuka agizo hilo la serikal, wakishamtambua polisi huyo basi huchukua jukumu la kumfuata nyumbani kwake au sehemu za starehe na kumpa kipigo na hata kummaliza kabisa, hii iliwafanya polisi wawe na hofu ya kukiuka kanuni ya kazi zao na kuzingatia haki za binadamu. Haya mabavu ya polisi yanatokana na uwezo wao mdogo wa kum-interrogate mhalifu wakiwa kwenye investigation.
 
mimi nadhani sheria wanaijua maana ni moja ya mafunzo yao ila
wanatumika sana kama sabuni hali wanaokwenda kuumia ni wao

Hawajui sheria mkuu usiwatetee. Wanachojifunza ni CPA CRIMINAL PROCEDURE ACT, Penal code, na PGO, sheria zenyewe ni kwa kingereza, askari wenyewe majority ni failures yani 0. Usifanye mchezo na sheria, miaka minne pale Ud na hapo sup kibao. Kama huamini tafuta bush lawyer umpambanishe na polisi kuhusu mambo ya sheria.
 
Bado wanahitaji elimu endelevu, Nafikiri mpaka sasa wanaamini mtu anayefanya kazi kwa "nguvu" hata kama kichwani hamna kitu atapanda cheo kama huyo kamanda wao Masawe!!!

nakubaliana na ww kiongozi kikubwa ni elimu pili najiuliza huyo kamanda masawe elimu yake ikoje ama alifika kiwango gani maana mambo aliosema inaonyesha kuwa elimu yake ya kukimbia umande maana kama ana elimi ya kutosha asingeongea upu**** ule! hawa makamanda wetu naanza kupata wasiwasi wao wa kielimu,

Wakumbuke kila lenye mwanzo lina mwisho iko siku WATANZANIA WATASEMA SASA TUMECHOKA KUONEWA WATAKIONA CHA MTEMAKUNI
 
nipe data za waliomaliza kidato cha 4 mwaka jana then niambie 70% yao wamefaidika vp na sera nzur ya CCM. Sera ya aliepata div 4 ya 31pts nae unamuita kafaulu?.
Regardless of what they got, being given opportuinity ya kufikia level ya form four ni achievent kubwa sana kwa vijana wetu
 
View attachment 30749
Kuna sheria moja imefunga watu sana hapa nchini, kujichukulia sheria mkononi au kupiga mtu hata kama amekuibia hivi polisi haiwahusu?
Kumdhalilisha hivi waziri kivuli wa sheria je sisi wengine itakuwaje?
Hiyo ni nguo ngumu lakini wameweza kumpa purukushani mpaka ikachanika, je mbavu zake ziko salama?

Mimi nadhani wananchi kuweke msimamo kama tukiona polisi anapiga mtu au kutumia nguvu kupitiliza tufanye nini?
Wenzetu uingereza juzi wamefanikiwa kuipasua sheria ya kuwawekea kinga kwa njia za mahakama watu wenye majina pale wanapofanya uovu kwa kutumia TWITTER.

Na tubuni mbinu ya kukomesha ukatili wa polisi, hata kama ni kuanzisha mfuko wa kuteteta watu wasio na kipato wanaonyanyaswa na polisi na mahakama tufanye, haki haiji kwa kuremba remba.
Hii ni aibu kwa jeshi letu la Polisi!
 
<br />
<br />


Acha hizo wewe,Ccm inaipeleka nchi kaburini,eti wangeifikisha nchi hapa,wapi? Hapa kwenye bei kubwa ya Umeme na Mgao usioisha? Ccm vilaza tu wakiongozwa na Mwenye anayechekacheka kama hamnazo!!!
Tatizo siyo CCM! Tatizo ni sisi wenyewe! Asilimia kubwa ya wananchi ni CCM, sasa iweje tujilaumu wenyewe? We hav to work hard!
 
Kwa suala la elimu hapo umekosea sana! CCM imejitahidi sana kutengeneza sera nzuri ya elimu kiasi kwamba kila mtoto miaka hii ana uhakika wa kumaliza kidato cha nne! Huon haya ni maendeleo makubwa?
Kuhusu suala la madawati, nchi nyingi za africa bado hazijaweza kufanikisha kuendeleza miundominu ya shule zao, especially in rural remote areas where accessbility inakuwa ngumu! Kwa hilo la madawati CCM has nothing to do with it!

Acha pumba wewe, una udhi, una kera, yaani kifupi unaongea upupu tupu. Yaani vijijini ndo hawana haki ya kukalia madawati eti kisingizio "ni rural remote area" acha upupu. Hiyo miundo mbinu mlikatazwa kuitengeneza toka uhuru? Wamishenari waliweza vipi kuweka miundo mbinu bora katika shule zao za vijijini miaka ile? Aisee unatia kichefuchefu kama mjamzito
 
Wangekuwa vilaza wangeweza kuifikisha nchi ilipo? Acha kuropoka tu, shirikisha na ubongo!
Kwani wewe unanona nchi ilipofika pazuri! POLE SANA NAPE! ( MAGAMBA MMEVUA YA NINI SASA?)
 
Acha pumba wewe, una udhi, una kera, yaani kifupi unaongea upupu tupu. Yaani vijijini ndo hawana haki ya kukalia madawati eti kisingizio "ni rural remote area" acha upupu. Hiyo miundo mbinu mlikatazwa kuitengeneza toka uhuru? Wamishenari waliweza vipi kuweka miundo mbinu bora katika shule zao za vijijini miaka ile? Aisee unatia kichefuchefu kama mjamzito
Mkuu kwenye nyekundu ni udhalilishaji wa mwanamke!
kwingine koote nakuunga mkono na kwa taarifa yako mkuu SHULE KIBAO HAPA JIJINI WATOTO WANAKAA CHINI TEMBELEA UTAONA MENGI, JUZI WAMEONYESHA ITV WANAFUNZI DODOMA MJINI WANAFANYIA MTIHANI CHINI!
 
Regardless of what they got, being given opportuinity ya kufikia level ya form four ni achievent kubwa sana kwa vijana wetu
toka madrasa mpaka form 4 inatosha! eeti tena 98% failure duu! MAGAMBA YANAENDELEA!
 
kwako mwanfunzi kumaliza kidato cha nne ni ndio maendeleo?mawazo yako mafupi kama ya raisi wako jk aliposema uchumi wa tanzania umekuwa sababu ya foleni za magari kuwa kubwa so mnafanana kwa akili.kwa mawazo yako mafupi unanitolea mifano mifupi kwa migongo ya nchi za afrika.vigogo wa ccm siril chami na william likuvi wana vibali vya kuvuna magogo serikali yako ya ccm imeshindwa vipi na yenyewe kuvuna magogo na kuwapa kazi jkt watutengenezee madawati sbb misitu tunayo?
mkuu si hapo tuu usisahau na thamani za kichina wanazotumia ofisa za serikali, wakati magereza na jkt wanatengeneza thamani nzuri sana poor tanzanian, tunapoteza pesa za kigeni kwa ujinga wetu, kweli ccm itoke tuu!
 
Hivi askari akimkimbiza mhalifu ambaye hataki kutiwa nguvuni akaendesha spidi kuliko ya mhalifu hapo atakuwa kavunja sheria au inatosha kusema sheria haimhusu?! What do you know abt the term "corrective measure"
Guys open your eyes and see things from their original colors, see things beyond politics!!
Its a police FORCE you are talkin about and thats just a REASONABLE FORCE.
Askari akitumwa kwa amri halali akazuie uhalifu, resistance ni kitu cha kutegemewa obviously. Lakini itafaa kwa askari kurudi na kusema "tumeongea nao wamesema watakuja kituoni baadaye"
If thats ok then tutakuwa tumeongeza govt expenditure bure kwa mishahara na gharama nyingine za polisi wakati hata hatuwahitaji ama hatuna jeshi lenyewe.
Tafakari.
 
inasikisha sana kwa kweli, hii nchi ni yetu sote, madini yalisha shindwa kutunufaisha tuwafukuze hawa Barricks, mbona zamani tulikuwa tunaishi tu.
 
hivi mbunge hana immunity? anaweza kudhalilishwa kiasi hiki akiwa mahabusu?
 
Back
Top Bottom