Polisi wazuia mkutano wa ‘CUF Lipumba’

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,604
2,000
Dar es Salaam. Mkutano uliotakiwa kuanza leo Jumanne Machi 12, 2019 wa Chama cha Wananchi (CUF) upande wa mwenyekiti anayetambuliwa na ofisi ya msajili wa vyama vya siasa Profesa Ibrahim Lipumba umezuiwa.

Taarifa ya kuzuiwa huko imeletwa katika eneo la mkutano huo Hoteli ya Lekam Buguruni na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala jijini Dar es Salaam. "Tumekuja kuwaeleza kuhusu zuio hili kwa sababu wameshalipeleka makao makuu ya Polisi," amesema Chembera.

Hata hivyo, Mkurugenzi wa Fedha wa CUF, Thomas Malima na Naibu Katibu mkuu (Bara) Magdalena Sakaya wamesema hawajapata katazo hilo kwa hiyo wataendelea na mkutano. "Sisi hatujapata hilo katazo, tunaendelea na mkutano," amesema Malima.

Awali, akizungumzia na waandishi wa habari, mkurugenzi wa uhusiano wa chama hicho, Abdul Kambaya amesema katazo la Mahakama limewataja watu watatu akiwemo Profesa Lipumba na Magdalena Sakaya.

"Katazo limewataja watu watatu, mkutano mkuu unaitishwa na Baraza Kuu, wao watakuja kama waalikwa tu," amesema Kambaya.

Muda mfupi, baada ya RPC wa Ilala kuondoka, mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Lipumba aliingia katika eneo la mkutano na kupokelewa kwa shangwe huku akiingizwa kwenye ukumbi ambao waandishi wa habari wamezuiwa kuingia.

Awali, Kambaya amesema mkutano rasmi unatarajiwa kufunguliwa Machi 14, 2019 akisema leo na kesho kutakuwa na mambo ya kiutawala.

-Mwananchi
 

imhotep

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
30,377
2,000
Maprofessa wetu bhana!..Huyu mzee anajiaibisha Mbele ya Umma.
Yeye na Msajili ni Matapeli tu.
 

CHA The GREAT

JF-Expert Member
Nov 11, 2010
652
1,000
"leo na kesho kutakuwa na mambo ya kiutawala" mwisho wa kunukuu. Itchukua tena karne ili angalau tuifikie Kenya.
 

kifinga

JF-Expert Member
Dec 5, 2011
4,931
2,000
Da nimecheka sana ha ha ha ha ha lipumba haamini kinachotokea kazoea kuwaletea figisu figisu wenzie leo wamemuwai
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom