Polisi wazuia mkutano wa CHADEMA Rujewa, Mbarali; sasa utafanyika Mei 28,2014

Chadema Diaspora

JF-Expert Member
Oct 25, 2010
481
1,000
Polisi wazuia mkutano wa CHADEMA Mbarali, Rujewa; sasa utafanyika Mei 28,2014

Mkutano wa CHADEMA wilayani Mbarali ulio kuwa ufanyike Rujewa Jumapili Mei 25, 2014;
Rujewa Gest, saa nane mchana (2pm) ukiwa na agenda zifuatazo ulizuiliwa na polis kwa madai kuwa kutakuwa fujo na intelejensia sio nzuri

Agenda za mkutano ni

-Ushuru ulio pitishwa na madiwani wa CCM
-Katiba na UKAWA
-Taarifa ya CAG juu ya ubadhirifu wa Billion mbili na million mia nne (2 billion na million 400) fedha za halimashauri

Hata hivyo kwa sababu mkutano ulikuwa ni halali na una vibari stahiki; polis wameshindwa kuzui huo mkutano moja kwa moja na kusema ufanyike Mei 28,2014 Jumatano. Habari kutoka kwa watu wa Mbarali wanasema kuwa polis wamekuwa wakizuia mikutano ya CHADEMA na kuwatia kizuizini viongozi wa CHADEMA mara kwa mara kitu ambacho kilipelekea mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Mbarali kumlima barua OCD. Pia inasemekana hujuma za kuzuia mkutano huo siku ya jumpili ni kwa sababu watu wengi walikuwa wamehamasiki kuhudhuria na kusikia hatma ya ubadhirifu wa billion 2 na ushuru wa gunia la mpunga Tsh 2000/=. Imani ya polis na watu ambao wapo nyuma ya zuio la mkutano huu ni kuwa wana Mbarali wengi huwa mashambani siku za wiki ndio maana walikataa huo mkutano usifanyike Jumapili

NB: Madiwani wote wa CHADEMA Mbarali watakuwepo na viongozi wa wilaya


Info na Maswali kuhusu mkutano piga;
767 362230 Nicko
753 786792 Pater Mwashiti

Mnaombwa kuhudhuria na kuwajurisha wengine
 

samaki2011

JF-Expert Member
Dec 17, 2013
1,776
0
wakulima kwa hasira ili kuwakomesha hawa sisiminzi interahamwe siku ya mkutano wa ukawa jitokezeni kwa wingi ck 1 haitapunguza kitu shambani ila mtapata ufahamu zaidi juu ya haki zenu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom