Polisi wazuia Mkutano Mkuu wa Lipumba uliokuwa unafanyika leo

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,271
47,271
  • Aibu kwa Msajili wa vyama vya siasa aliyebariki mkutano na kutoa ruzuku kwa ajili ya mkutano huku akijua kuna zuio la Mahakama.
  • Aibu kwa prof. Lipumba na genge lake kwa kutoheshimu mahakama.
  • Aibu kwa demokrasia nchini.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Ilala limezuia mkutano wa CUF upande wa Mwenyekiti Profesa Ibrahim Lipumba likisema kuna zuio la mahakama.

cufpic.jpg

Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama Cha wananchi CUF wakiwa katika Ukumbi wa Lekama Social Hall Buguruni jijini Dar es Salaam leo. Picha na Anthony Siame.

Mwananchi: Polisi wazuia mkutano wa ‘CUF Lipumba’
 
Si ajabu ukakuta ni macccm haya ! Inawezekanaje kuna zuio la Mahakama and still Lipumba anapata ujasili wa kuendelea na mkutano. Hawa wajumbe wametoka kipande gani ya nchi?
 
Yaani kuna mambo yanatokea Tanzania tu huwezi kuyakuta kwenye nchi nyingine.Lipumba huyo huyo anapewa pesa za ruzuku isivyostahili mpaka anawasafirisha hao wanaoitwa wajumbe wa mkutano mkuu kutoka sehemu mbalimbali ikiwemo kwao Uyui,halafu mnasubiri waje mpaka kwenye ukumbi ndo mnajifanya kuwazuia?mnatudanganya sana watanzania
 
Hata wangewaacha tu hawana madhara yoyote kwa cuf yetu ya maalim seif, labda kwa ccm ndiyo imeathirika
 
Si ajabu ukakuta ni macccm haya ! Inawezekanaje kuna zuio la Mahakama and still Lipumba anapata ujasili wa kuendelea na mkutano. Hawa wajumbe wametoka kipande gani ya nchi?

Walisafirishwa kwa treni kutoka Kaliua kwa Sakaya na Lulanguru kwa Lipumba.
 
Yaani kuna mambo yanatokea Tanzania tu huwezi kuyakuta kwenye nchi nyingine.Lipumba huyo huyo anapewa pesa za ruzuku isivyostahili mpaka anawasafirisha hao wanaoitwa wajumbe wa mkutano mkuu kutoka sehemu mbalimbali ikiwemo kwao Uyui,halafu mnasubiri waje mpaka kwenye ukumbi ndo mnajifanya kuwazuia?mnatudanganya sana watanzania
Anayechangia yote haya ni Masajili wa vyama, wiki kama moja hivi kulikuwa na taarifa ya kikao chake na Magdalena Sakaya wakipanga mkutano na kesho yake tukasikia RITA wameisajili Bodi ya Lipumba.

Hii yote ni kuchezea pesa ya walipakodi, ifike mahala watu kama hawa wawe wanafidia hasara kama hizi kwa gharama zao.
 
Hapana unaendelea. Ofisi ya msajili imebariki. Wamekaidi na sasa polisi waliotumwa kuuzuia ndio wanatoa ulinzi. Tayari shisty nyahoza kutoka ofisisi ya msajili amehutubia na kupongeza. Hio ndio polisi na hii ndio SMZ na JMT
 
Mkutano unaendelea. Wamekaidi .wamepewa baraka zote na ofisi ya msajili. Shisty Nyahoza wa msajili amehutubia na kupongeza . Wake polisi waliotumwa kuzuiya sasa ndio wanatoa ulinzi mkutano uendelee. Hao ndio polisi, hio ndio SMZ na JMT
 
Back
Top Bottom