Polisi wazuia mikutano ya mbunge wa CUF Tanga

Kifoi

JF-Expert Member
May 12, 2007
1,226
531
pic+mbunge.gif

Mbunge wa Tanga Mussa Mbarouk kupitia chama cha wananchi CUF

Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Tanga, Leonard Paulo amesema hayo leo alipokuwa akizungumza na Mwananchi.Tanga.

Jeshi la Polisi wilayani hapa limemzuia Mbunge wa Tanga, Mussa Mbarouk kupitia CUF kufanya mikutano ya hadhara kwa muda usiojulikana kutokana na kile ilichoeleza kwamba inaweza kuhatarisha amani.

Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Tanga, Leonard Paulo amesema hayo leo alipokuwa akizungumza na Mwananchi.

“Mkuu wa jeshi la Polisi Wilaya ya Tanga (OCD) amesitisha mikutano ya hadhara ya mbunge huyo kwa muda usiojulikana kwa sababu ameonyesha kwamba mikutano yake haina malengo na nia njema,” alisema Paulo.

Alisema mbunge huyo alimakatwa juzi jumapili baada ya kufanya mkutano wa hadhara Agosti 13 mwaka huu katika mtaa wa Madina kata ya Msambweni ambako alitoa matamshi yenye kuchochea chuki baina ya wananchi na Rais pamoja na vyombo vya dola.

Chanzo: Mwananchi
 
CUF wameamua kukaa kimya kwenye suala la uvunjifu wa demokrasia unaofanywa na mkuu wa kaya akishirikiana na chama chake. CHADEMA na ACT pekee ndo wamekuwa mstari wa mbele kupambana na udhalimu huu huku Chama cha Wananchi kikionekana kupuuzia suala hili la usiginaji wa demokrasia. Binafsi nimeona ni bora huyo mbunge alivyozuiwa ili kama watakuwa wameumizwa, nao watajiunga na wenzao katika mapambano dhidi ya udhalimu huu unaofanywa na mkuu wa kaya na chama chake kwa ushirikiano na vyombo vya dola.
 
Back
Top Bottom