Polisi wazuia mikutano ya Chadema nchi nzima; Chadema wamekubali? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Polisi wazuia mikutano ya Chadema nchi nzima; Chadema wamekubali?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ngisibara, Nov 27, 2010.

 1. Ngisibara

  Ngisibara JF-Expert Member

  #1
  Nov 27, 2010
  Joined: Jan 2, 2009
  Messages: 2,083
  Likes Received: 431
  Trophy Points: 180
  Poliosi wazuia mikutano ya Chadema nchi nzima Saturday, 27 November 2010 06:41


  [​IMG] IGP Said Mwema

  Waandishi Wetu
  HALI bado si shwari baina ya Jeshi la Polisi na Chadema baada ya chombo hicho cha dola kukizuia chama hicho kufanya mikutano ya hadhara nchi nzima "hadi hapo hali itakapotengemaa".
  Lakini hakuna ofisa wa jeshi hilo aliyekuwa tayari kutoa maelezo bayana kuhusu amri ya kuzuia maandamano ya Chadema kwa kisingizio hicho, huku kila mmoja akirumshia mpira mwenzake na mwishoni kutaka aulizwe Waziri Mkuu au mkuu wa Jeshi la Polisi, Inspekta Jenerali Said Mwema, ambaye hata hivyo hakupatikana.
  Chadema iliweka rekodi ya kutwaa majimbo mengi ya Tanzania Bara kwenye uchaguzi mkuu na katika baadhi ya majimbo ilishindwa kwa tofauti ya kura chache na kusababisha kuibuka kwa vurugu zilizotokana na wananchi kudai matokeo yatangazwe mapema.
  Baada ya kufanya uchunguzi kwenye majimbo kadhaa, Mwananchi imebaini kuwa wabunge na wagombea ubunge wa Chadema wamekuwa wakitaka kufanya mikutano ya hadhara kwa malengo tofauti, lakini wamejikuta wakizuiwa na jeshi hilo ambalo jukumu lake ni kutoa ulinzi kwenye mikutano ya hadhara.
  Kamanda Clodwig Mtweve, ambaye hukaimu shughuli za IGP Mwema, alikiri kuwepo kwa agizo la kukizuia chama hicho kuendesha mikutano ya hadhara.
  Kamishna Mtweve, ambaye anahusika na utawala na rasilimali, alisema:
  "Maombi ya Chadema ambayo tumeyapokea yanaambatana na maandamano na wanasema ni maandamano ya kuhitimishwa kwa sherehe za mikutano ya hadhara ya kupongezana kwa ushindi.
  "Sasa sisi tumeyakataa na kama ni sherehe za kupongezana tunasema zifanyike ukumbini. Na hii si kwa Chadema tu, bali hata kwa chama tawala."
  Kamishna Mtweve alisema Chadema wanaruhusiwa kufanya mikutano ya hadhara isiyoambatana na maandamano na kwamba amri ya kutoruhusiwa kwa maandamano haina muda maalum na inaendelea kuwepo hadi polisi watakapoamua vinginevyo.
  Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, John Tendwa alikitaka chama hicho kuwasilisha malalamiko hayo kwake kama kweli kimezuiwa kuendesha mikutano ya hadhara.
  Awali kabla ya kuwasiliana na Kamishna Tweve, kamanda wa Kanda ya Dar es salaam, Suleiman Kova alisema: “Malalamiko ya Chadema ni ya nchi nzima. Mimi siwezi kuropoka chochote; kama unataka, ongea na Waziri Mkuu au Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Said Mwema.”

  IGP Mwema ndiye aliyemuelekeza mwandishi afuatilie suala hilo kwa Kamishna Tweve.
  Mapema katika hatua za kutaka kuthibitisha taarifa hizo, Mwananchi iliwasiliana na msemaji wa Jeshi la Polisi, Advera Senso lakini akampa kazi nyingine mwandishi wetu.
  “Wasiliana na makamanda wa majimbo yote yaliyotoa taarifa hizo kwa sababu wao ndio wahusika na wasemaji wakuu," alisema Senso.
  Baadhi ya mikoa iliyoripotiwa kuwepo na matukio ya kuzuiwa kwa mikutano ya Chadema ni pamoja na Jimbo la Segerea mkoani Dar es Salaam, Mpanda (Katavi), Babati (Manyara), Arusha, Mbeya na Musoma mkoani Mara.
  Makamu mwenyekiti wa Chadema ambaye pia ni mbunge wa Mpanda Mjini, Said Arfi amelalamikia kitendo cha jeshi hilo wilayani Mpanda kuzuia mkutano wa hadhara na maandamano yaliyopangwa kufanyika kesho jimboni humo.
  Arfi, ambaye alishinda katika uchaguzi uliofanyika Novemba 14 baada ya kuahirishwa kutokana na kasoro kadhaa zilizojitokeza kwenye majimbo saba wakati wa uchaguzi mkuu wa Oktoba 31, alisema kuwa wananchi wake waliandaa mkutano wa hadhara na kupeleka taarifa polisi, lakini walinyimwa ruhusa ya kufanya hivyo.
  “Nikiwa najiandaa kwenda kwenye mkutano jimboni kwangu, nimepata faksi inayoonyesha barua ya Jeshi la Polisi inayokataza kuwepo kwa maandamano na mkutano huo,” alisema Arfi.
  Barua hiyo yenye kumbukumbu namba MPA/S04/ Vol 2/93 imeleeza sababu ya kukatazwa kwa mkutano huo ni kuwepo kwa taarifa za baadhi ya vyama visivyo na mapenzi mema na Chadema kuashiria kuvunja amani.
  “Pamoja na barua hii nakujulisha kuwa kutokana na taarifa tulizonazo, baadhi ya vyama vya siasa havina nia njema na zoezi hilo. Kwa sababu hiyo si ruksa kuandamana wala kufanya mikutano ya hadhara kwa sasa,” inasema barua hiyo ya polisi.
  Arfi alisema kuwa amejaribu kuwasiliana bila ya mafanikio na kamanda wa polisi mkoa wa Rukwa anayesimamia pia mkoa wa Rukwa.
  Kwa upande mwingine, Arfi alisema wamebaini kuwa hali hiyo imetokea pia katika maeneo yote ambayo chama hicho kilipanga kufanya mikutano.
  Aliyataja maeneo hayo kuwa ni pamoja na Jimbo la Tarime, Arusha, Segerea na Mbeya.
  “Huu ni mkakati umewekwa ili kutukwamisha Chadema. Kama kuna hali ya hatari, mbona rais hajatangaza kuwepo kwa hali hiyo,” alihoji Arfi akirejea sheria inayomruhusu amiri jeshi mkuu tu kuwa ndiye mwenye uwezo wa kutangaza hali ya hatari ambayo huzuia mikusanyiko ya aina yoyote ile.
  Alisema kwa hali hiyo serikali haiwatendei haki kwa kuwa imewazuia kufanya shughuli za siasa na kwamba watakutana kama chama ili kutoa tamko.
  Kamanda polisi wa Ilala, Faustine Shilogile alikiri kuwepo na maelekezo ya kuzuia mikutano hiyo, akiweka bayana kuwa agizo hilo limetoka Kanda Maalumu ya Dar es Salaam.
  “Agizo hilo tumelipokea kutoka ofisi zetu za Kanda Maalumu ya Dar es Salaam," alisema Shilogile na kuongeza: "Sababu za agizo hilo mimi sizijui ila nimeagizwa kufanya hivyo.”
  Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Rukwa, Isunto Mantage alisema hajapata taarifa zozote kuhusu hali mbaya ya usalama kwenye Wilaya ya Mpanda ambako mbunge Arfi alizuiwa kufanya mkutano wa hadhara.
  "Hiyo barua kwenda kwa mbunge sijaiona, pengine ningeiona ningeweza kusema chochote... nipe muda niwasiliane na huko Mpanda ili niweze kufahamu kinachoendelea halafu nitakujulisha," alisema Kamanda Mantage.
  Hata hivyo, alisema jana asingeweza kufanya mawasiliano na polisi wa Mpanda kutokana na kuwa kwenye ziara vijijini ambako kuna matatizo ya mawasiliano.
  Kutoka mkoani Mwanza taarifa zinasema kuwa polisi imezuia maandamamo ya uzinduzi wa maadhimisho ya "Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Wanawake Majumbani" ikidaiwa ni kutokana na waandaaji wake kumualika mbunge mpya wa Jimbo la Nyamagana kwa tiketi ya Chadema, Ezekiel Wenje kuwa mgeni rasmi.
  Mratibu wa maadhimisho hayo kutoka Shirika la Kutetea Haki za Wanawake (Kivulini), Yusta Ntibashima aliliambia gazeti hili jana kuwa polisi imezuia maandamano hayo kutokana na kuhofia watu kuwa wengi kwa sababu ya mgeni huyo rasmi.
  Alisema kufanyika kwa maandamano hayo kungeweza kuwa na athari kubwa kwa uchaguzi mdogo wa udiwani ambao umepangwa kufanyika kesho katika kata mbili za Mkuyuni na Mirongo, hivyo kuwaomba waandaaji kufanya maandamano yao baada ya uchaguzi.
  “Tukiwa katika kikao cha pamoja, Kamanda Sirro alisema jeshi lake haliwezi kutoa kibali cha maandamano kwa kuhofia watu watakuwa wengi na hivyo kusababisha kuzuka kwa vurugu kama zile za uchaguzi mkuu wakati watu walipochoma ofisi za CCM,” alieleza Ntibashima akimkariri kamanda wa polisi mkoa.
  Kamanda huyo alisema jeshi lake lilipaswa kupewa taarifa wiki moja kabla ili liandae askari wa kutuliza wengi wa kutosha kila aneo ili kuhakikisha maandamano hayo yanakuwa ya amani na kuepuka maafa.
  Hata hivyo, habari kutoka ndani ya jeshi hilo zimeeleza kuwa, sababu za kuzuia maandamano ni kuhofia lawama ambazo zingeibuka kutokana na mgeni rasmi wa shughuli hiyo kuwa mbunge wa Chadema.
  “Kama mgeni rasmi angekuwa kiongozi mwingine na siyo mbunge wa Chadema, basi maandamano hayo yangeruhusiwa, lakini CCM walitushutumu sana baada ya uchaguzi kuwa tulishindwa kulikomboa Jimbo la Nyamagana na tulikuwa tukiwaacha vijana kutamba na kufanya wanavyotaka... naona ameogopa kulaumiwa tena kamanda,” alieleza mmoja wa maofisa wa polisi ambaye hakutaka kutaja jina lake gazetini.
  Alipoulizwa kuhusu suala hilo, Kamanda Sirro alisema amezuia maandamano hayo kutokana na kutokuwa na muda wa kutosha baada ya waandaaji kuchelewa kutoa taarifa.
  Kuhusu taarifa kuwa agizo hilo linahusiana na uchaguzi, Sirro alisema: “Kwa sasa nipo nje ya Mwanza; nitarejea Jumatatu, naomba unitafute... nitafafanua ni kwa nini tumezuia.”
  Mkurugenzi wa Kivulini, Maimuna Kanyamala alisema uamuzi wao wa kumualika Wenje kuwa mgeni rasmi ni utaratibu wa kawaida na kwamba kila mara wanapokuwa na maadhimisho hayo hualika viongozi mbalimbali.
  Alisema wakati majimbo ya Nyamagana na Ilemela yakiwa chini ya wabunge wa CCM, walikuwa wakiwaalika wabunge hao wa chama tawala na hawakukutana na vikwazo.
  “Mgeni rasmi huchaguliwa katika kikao cha maandalizi ya maadhimisho. Lengo la kuwa na mgeni rasmi ni kupata kiongozi ambaye kwa uwezo wake anahusika na utungaji sera ama mabadiliko," alisema.
  Akizungumza na gazeti hili, Wenje alisema polisi wanaingilia mambo bila ya kujua kwa kuwa maandamano hayo si ya kisiasa na hayana uhusiano na Kata ya Nyamagana kwa kuwa uchaguzi unafanyika kwenye Kata ya Mkuyuni na Mirongo.
  “Nadhani Jeshi la Polisi linaitafsiri vibaya sheria. Mimi ni mbunge kama wale wa CCM, sasa siwezi kuzuiwa kuendelea na shughuli zangu kama mbunge kwa sababu ya kisingizio cha uchaguzi. Haya ni maandamano ya wanaharakati na siyo maandamano ya Chadema, polisi wanapaswa kuelewa hilo,” alisema Wenje.
  Mkurugenzi wa mambo ya katiba na Bunge wa Chadema, John Mrema alisema chama chake kimeshtushwa na hatua ya polisi kuzuia mikutano ya chama hicho na kwamba kesho watatoa tamko.
  "Wametuzuia nchi nzima; tayari tumekusanya ushahidi mwingi kutoka maeneo mbalimbali," alisema Mrema.
  "Tunashangaa kwani vyama vya siasa vinakosa kazi baada ya uchaguzi? inakuwaje wametuzuia kufanya mikutano yetu, uchaguzi umekwisha, nchi ina amani na utulivu wa kutosha, hakuna vurugu, lakini wao wanasema wametuzuia kwa sababu ya taarifa za kipelelezi wakidai eti hali ni tete. Hii ni hofu isiyo na msingi."

  Nafikiri ingefaa Chadema wapate uthibitisho halisi na kuutangazia umma wa watanzania wote kuwa wamepigwa pin bila sababu ya msingi, then itasaidia kuongeza kura nyingi tu lakini zitakuwa za huruma
   
 2. Supa.engineer

  Supa.engineer Member

  #2
  Nov 27, 2010
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 47
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nadhani serikali isisingizie vurugu katika nchi inayo taka demokrasia kama Tanzania. Hapa ndoo huwa naanza kuona kichefuchefu na kuichukia TZ hata kama is my country.
   
 3. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #3
  Nov 27, 2010
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Hii ni mzuri sana, lazima nchi izibe nyufa, tusipoziba nyufa tutajenga ukuta.

  Maandamno yakupongezana? Hawa watu wa ajabu sana! Sijasikia watu wakipongezana kwa maandamano. Si waende kumbi za sherehe wakapongezane.
   
 4. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #4
  Nov 27, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  wanataka kurusha tena helikopta hewani nchi nzima?............. hizo hela zinatoka wapi?.......... ama kweli bongo kazi ipo.............
   
 5. Mimibaba

  Mimibaba JF-Expert Member

  #5
  Nov 27, 2010
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 4,566
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Huna wakukupongeza wala wakumpongeza inaeleweka. Wana haki ya kikatiba kufanya hivyo
   
 6. Mimibaba

  Mimibaba JF-Expert Member

  #6
  Nov 27, 2010
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 4,566
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Kutoka kwa wananchi wenye chama
   
 7. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #7
  Nov 27, 2010
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Nilijua hili litatokea soon or later, I suggest wananchi wenyewe tujiorganise "kudai katiba na tume ya uchaguzi kubadilika" wenyewe... I suggest kutumia njia mbadala kama kuorganise namba ya sms kwa wananchi kutuma na kudai katiba mpya tunaweza kutumia hii kama ammunition kwa kuwapa wabunge wetu kujadili hili suala bungeni. "Non violence non violence, We shall overcome"
   
 8. F

  Froida JF-Expert Member

  #8
  Nov 27, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Kwani Polisi wamepata wapi uwezo wa kuzuia maaandamano ya amani hawa wanatumiwa na serikali na CCM Polisi kumbukeni hii nchi ni yetu wote bwana sio ya kikundi fulani cha wahuni
   
 9. MchunguZI

  MchunguZI JF-Expert Member

  #9
  Nov 27, 2010
  Joined: Jun 14, 2008
  Messages: 3,623
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280

  Energize your cerebral before engaging gear.
   
 10. MchunguZI

  MchunguZI JF-Expert Member

  #10
  Nov 27, 2010
  Joined: Jun 14, 2008
  Messages: 3,623
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  Wanahangaika na mambo trivial wanaacha kazi zao na shida zao. Ndo maana imefikia hatua OCD mzima kutwangwa makofi na 'CCM'.
   
 11. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #11
  Nov 27, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  CCM at WORK
   
 12. YeshuaHaMelech

  YeshuaHaMelech JF-Expert Member

  #12
  Nov 27, 2010
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 2,624
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  didn't I say I hear a sound of hoofs a far? May God help us!
   
 13. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #13
  Nov 27, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,182
  Trophy Points: 280
  Hali gani itakapotengemaa ? Hivi Tanzania kumetangazwa hali ya hatari ?

  Huu ni uvunjaji wa katiba ya nchi, kuwazuia watu kufanya mikutano ya kisiasa ya amani chini ya wigo wa haki ya kukusanyika pamoja inayotolewa na katiba.

  CHADEMA wanatakiwa kuishitaki polisi, au kudai uwezekano wa kuishitaki polisi kama kuishitaki haiwezekani, ili kupata haki yao ya kikatiba.

  Kama wakishindwa hili mambo makubwa kama kubadili katiba yatakuwa ndoto ndani ya miaka 5-10 ijayo.

  http://www.tanzania.go.tz/images/katibamuungano.pdf


  Benjamin Franklin alisema "Those who sacrifice freedom for security deserve neither". Hatuwezi kuwa na polisi wanaotaka kuzuia watu wasikutane eti na sababu tu wanahofia kutakuwa na fujo.

  What's next? Watataka kutufungia ndani ili tu tusije kuwa wahalifu ? Waache watu wakutane, wakifanya fujo fanya kazi yako kama polisi na FFU, sasa unataka kuwa polisi jina usiye na kazi?

  Hatuwezi kuwa na polisi wanaofanya kazi kwa kutumia mtego wa panya unaowanasa waliokusudiwa na wsiokusudiwa.
   
 14. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #14
  Nov 27, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,821
  Likes Received: 10,117
  Trophy Points: 280
  Wanazidi kuwasha moto unaofuka chinichini haya yetu macho sie
   
 15. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #15
  Nov 27, 2010
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280

  Nategemea Lisu na Marando watalifanyia kazi mara moja.
   
 16. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #16
  Nov 27, 2010
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  well said
   
 17. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #17
  Nov 27, 2010
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  90% ya hawa wapiga soga wa JF wanao shabikia maandamano hawapo Tanzania.
   
 18. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #18
  Nov 27, 2010
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,638
  Likes Received: 1,427
  Trophy Points: 280

  Hii nchi ya kipimbi sana... kwa style hii hatutaendelea kamwe!

  kama vip tujikusanye na tuingie barabarani tu kwani kibali kitu gani bana?:disapointed:
   
 19. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #19
  Nov 27, 2010
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Kwahiyo hao 10% hawana haki
   
 20. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #20
  Nov 27, 2010
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Hawana haki ya kaandamana mpaka wapate kibali, na Serikali ikishaona kuwa kuna uvunjaji wa amani unaoweza kutokea, hawatoi kibali mpaka watapohakikisha kuwa wanaweza kumudu kuwadhibiti wavunja amani, wachache, ambao wanaweza kujitokeza kwenye maandamano.

  Halafu si wangoje basi Mawaziri wachukuwe ofisi zao, wajipange, na hapo watapewa vibali vya kuandamana hata wakitaka usiku na mchana, kuwadhibiti, wavunja amani wachache itakuwa ni rahisi.

  Kwa sasa hawana haki kwa kuwa hawajapata ruksa!
   
Loading...