Polisi wazuia maandamano ya wazee wastaafu kuandamana Dar

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,007
Date::8/6/2008
Polisi wazuia maandamano ya wazee wastaafu kuandamana Dar

Kagashe Beatus na Florence Mugarula
Mwananchi

JESHI la Polisi, Mkoa wa Kinondoni, Kanda Maalumu, wamezima maandamano ya wastaafu wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) hadi Ofisi za Ubalozi wa Marekani kuelezea matatizo ya mafao yao.

Magari ya polisi pamoja na Polisi wa Kuzuia Ghasia walionekana wakivinjari katika viwanja vya ubalozi wa Marekani jijini Dar es Salaam kuanzia saa 2.30 asubuhi ili kudhibiti maandamano.

Wazee hao waliiomba serikali kutoa tamko kama haiko tayari kuwalipa mafao yao ili waweze kuchukua hatua nyingine au wasamehe haki zao za msingi.

"Sisi tunataka tamko la serikali kama hawako tayari kutulipa tujue tufanye nini sio kutuzungusha kama wakimbizi ndani ya nchi yetu," alisema mmoja wa wazee hao.

Mwenyekiti wa wastaafu hao, Nathaniel Mlaki, alifika katika eneo la ubalozi kuangalia kama uwezekano wa wao kufanya maandamano hayo, lakini alielezwa na maafisa wa polisi yalikuwa batili na kwamba, Balozi wa Marekani, Mark Green, hakuwa tayari kukutana nao.

Wazee hao wamemwomba Rais kuongea nao na sio kuwakimbia na kwamba, watapiga kambi Ikulu mpaka madai yao yatakaposikilizwa na kutatuliwa.

Akizungumza na waandishi wa gazeti hili katika eneo la tukio, Mlaki alidai kuwa, serikali inatumia vyombo vya dola kuwakandamiza na kuwanyima haki zao licha ya wao kufuata taratibu zote za kufanya maandamano.

"Sisi tumefuata taratibu zote za kufanya maandamano, tumeandika barua kwa Kamanda Kova na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchi (IGP), Said Mwema, pamoja na ubalozini, lakini serikali inaamua kutunyanyasa," alidai Mlaki.

Aliongeza kuwa serikali inashindwa kutambua mchango wa wazee hao ambao nguvu na mishahara yao ilichangia viongozi wengi wa sasa kusoma bure na kujengewa uwezo wa kushika nyadhifa mbalimbali serikalini, badala yake polisi wanatumwa kutukandamiza.

Hata hivyo, Mwenyekiti huyo wa alishindwa kuthibitisha iwapo walipokea barua ya ombi lao la kuandamana kukubaliwa.
 
Hmmm!!! iko siku haki itapatikana wazee. Yaani iko siku.....
 
warudishe kadi zao kwa CCM utaona watakavyochangamkiwa kushughulikia...

Mkjj, sijui kama wana hii idea. Ka inzi kako kama kangeruka hadi walipoweka maskani yao na kuwatonya kuhusu hili basi wangepewa nafasi ya kukutana na LAIS (Rais alikuwa Mwalimu tu) haraka sana.
 

Polisi wazuia maandamano ya wazee wastaafu kuandamana Dar

Kagashe Beatus na Florence Mugarula
Mwananchi

Angalia sasa, crummy press, gazeti linachemsha mpaka kwenye heading. Kiswahili kidogo tu. Jirani zetu wakisoma illiteracy kama hiyo si nchi nzima tunaonekana illiterate !
 
Kwa sasa itabidi wasahau tu maana hata kama kuna fungu walitengewa litakuwa limetafutiwa utaratibu mwingine ,serikali yenyewe hii budget wafadhili wamesusia ..sijui.

Ndio wajue madaraka kumpa msanii.
 
Makundi mbalimbali ktk jamii yanapoanza kupata joto ya jiwe toka serikali huwa ni mwanzo mzuri wa kuelekea ktk ukombozi?
 
Back
Top Bottom