Polisi wazuia maandamano ya wazee wastaafu kuandamana Dar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Polisi wazuia maandamano ya wazee wastaafu kuandamana Dar

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Aug 7, 2008.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Aug 7, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,609
  Likes Received: 82,187
  Trophy Points: 280
  Date::8/6/2008
  Polisi wazuia maandamano ya wazee wastaafu kuandamana Dar

  Kagashe Beatus na Florence Mugarula
  Mwananchi

  JESHI la Polisi, Mkoa wa Kinondoni, Kanda Maalumu, wamezima maandamano ya wastaafu wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) hadi Ofisi za Ubalozi wa Marekani kuelezea matatizo ya mafao yao.

  Magari ya polisi pamoja na Polisi wa Kuzuia Ghasia walionekana wakivinjari katika viwanja vya ubalozi wa Marekani jijini Dar es Salaam kuanzia saa 2.30 asubuhi ili kudhibiti maandamano.

  Wazee hao waliiomba serikali kutoa tamko kama haiko tayari kuwalipa mafao yao ili waweze kuchukua hatua nyingine au wasamehe haki zao za msingi.

  "Sisi tunataka tamko la serikali kama hawako tayari kutulipa tujue tufanye nini sio kutuzungusha kama wakimbizi ndani ya nchi yetu," alisema mmoja wa wazee hao.

  Mwenyekiti wa wastaafu hao, Nathaniel Mlaki, alifika katika eneo la ubalozi kuangalia kama uwezekano wa wao kufanya maandamano hayo, lakini alielezwa na maafisa wa polisi yalikuwa batili na kwamba, Balozi wa Marekani, Mark Green, hakuwa tayari kukutana nao.

  Wazee hao wamemwomba Rais kuongea nao na sio kuwakimbia na kwamba, watapiga kambi Ikulu mpaka madai yao yatakaposikilizwa na kutatuliwa.

  Akizungumza na waandishi wa gazeti hili katika eneo la tukio, Mlaki alidai kuwa, serikali inatumia vyombo vya dola kuwakandamiza na kuwanyima haki zao licha ya wao kufuata taratibu zote za kufanya maandamano.

  "Sisi tumefuata taratibu zote za kufanya maandamano, tumeandika barua kwa Kamanda Kova na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchi (IGP), Said Mwema, pamoja na ubalozini, lakini serikali inaamua kutunyanyasa," alidai Mlaki.

  Aliongeza kuwa serikali inashindwa kutambua mchango wa wazee hao ambao nguvu na mishahara yao ilichangia viongozi wengi wa sasa kusoma bure na kujengewa uwezo wa kushika nyadhifa mbalimbali serikalini, badala yake polisi wanatumwa kutukandamiza.

  Hata hivyo, Mwenyekiti huyo wa alishindwa kuthibitisha iwapo walipokea barua ya ombi lao la kuandamana kukubaliwa.
   
 2. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #2
  Aug 7, 2008
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Hmmm!!! iko siku haki itapatikana wazee. Yaani iko siku.....
   
 3. BabaH

  BabaH JF-Expert Member

  #3
  Aug 7, 2008
  Joined: Jan 25, 2008
  Messages: 703
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  si mnaipigia CCM kura bila kujali, na cha ajabu hata serikali haitambui mchango wenu enzi za ujana wenu mlioitendea nchii hii wanayofaidi wachache
  Haya ndio matunda, maana nyie wazee mmekuwa mkiitetea sana serikali hii pindi mnapopelekwa pale ukumbini karimjee na kuutubiwa na Kikwete na kuwadanganya danganya mnakubali tu

  sasa mnaonja moto ya jiwe, mlipanda na mnaendelea kupalilia mibono, mnadhani mtavuna mpunga??
   
 4. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #4
  Aug 7, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  warudishe kadi zao kwa CCM utaona watakavyochangamkiwa kushughulikia...
   
 5. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #5
  Aug 7, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,609
  Likes Received: 82,187
  Trophy Points: 280
  Mkjj, sijui kama wana hii idea. Ka inzi kako kama kangeruka hadi walipoweka maskani yao na kuwatonya kuhusu hili basi wangepewa nafasi ya kukutana na LAIS (Rais alikuwa Mwalimu tu) haraka sana.
   
 6. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #6
  Aug 7, 2008
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Angalia sasa, crummy press, gazeti linachemsha mpaka kwenye heading. Kiswahili kidogo tu. Jirani zetu wakisoma illiteracy kama hiyo si nchi nzima tunaonekana illiterate !
   
 7. M

  Mutu JF-Expert Member

  #7
  Aug 7, 2008
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Kwa sasa itabidi wasahau tu maana hata kama kuna fungu walitengewa litakuwa limetafutiwa utaratibu mwingine ,serikali yenyewe hii budget wafadhili wamesusia ..sijui.

  Ndio wajue madaraka kumpa msanii.
   
 8. M

  Malila JF-Expert Member

  #8
  Aug 7, 2008
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280
  Makundi mbalimbali ktk jamii yanapoanza kupata joto ya jiwe toka serikali huwa ni mwanzo mzuri wa kuelekea ktk ukombozi?
   
Loading...