Polisi wawili mbaroni kwa kuomba rushwa milioni 7.2

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,879
6,356
Polisi mkoani Rukwa inawashikilia askari wake wawili wa Kituo Kikuu cha Polisi wilayani Nkasi, wakituhumiwa kuomba na kupokea rushwa ya zaidi ya Sh milioni 7.2 wamsaidie mtuhumiwa.

Kaimu Kamanda wa Polisi wa Rukwa, Leonce Rwegasira alitaja askari hao kuwa ni Konstebo Filbert Ruhemeja na Konstebo Bahati Sengerema, ambao walikuwa wakifanya kazi katika Kituo cha Polisi mjini Namanyere wilayani Nkasi.

Alisema polisi inawafanyia uchunguzi wa kina askari wake wawili, wanaotuhumiwa kwa kashfa ya kuomba rushwa ya Sh milioni 7.2 na iwapo watabainika halitasita kuwatimua na kuwafikisha mahakamani.

Alisema askari hao wawili wa polisi, wanatuhumiwa kuomba na kupokea rushwa ya fedha kutoka kwa mtu mmoja ili wamsaidie katika shitaka linalomkabili.

Chanzo: HiviSasa
 
Rushwa ilikuwa sahani ya wali, lakini karne hii MTU anataka ajenge kwa rushwa, tutafika kombwa nyumba kabisaaa
 
Rushwa ipigwe vita kuanzia ngazi ya mtaa hadi Ikulu. Hivyo anayekamatwa bila kujali wadhifa au unyonge wake lazima achukuliwe hatua. Achunguzwe na ikithibitishwa adhabu stahiki juu yake zichukuliwe.
 
Polisi mkoani Rukwa inawashikilia askari wake wawili wa Kituo Kikuu cha Polisi wilayani Nkasi, wakituhumiwa kuomba na kupokea rushwa ya zaidi ya Sh milioni 7.2 wamsaidie mtuhumiwa.

Kaimu Kamanda wa Polisi wa Rukwa, Leonce Rwegasira alitaja askari hao kuwa ni Konstebo Filbert Ruhemeja na Konstebo Bahati Sengerema, ambao walikuwa wakifanya kazi katika Kituo cha Polisi mjini Namanyere wilayani Nkasi.

Alisema polisi inawafanyia uchunguzi wa kina askari wake wawili, wanaotuhumiwa kwa kashfa ya kuomba rushwa ya Sh milioni 7.2 na iwapo watabainika halitasita kuwatimua na kuwafikisha mahakamani.

Alisema askari hao wawili wa polisi, wanatuhumiwa kuomba na kupokea rushwa ya fedha kutoka kwa mtu mmoja ili wamsaidie katika shitaka linalomkabili.

Chanzo: HiviSasa
Sijawahi kusikia tangu nije dunia hii RPC amekamatwa akipokea rushwa.Wao wana utaalam wa kukwepa kukamatwa jambo ambalo hawa polisi wadogo hawana! Ni maajabu haya!
 
Back
Top Bottom