Polisi wawalazimisha vijana kufanya kufanya mapenzi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Polisi wawalazimisha vijana kufanya kufanya mapenzi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mungi, Dec 22, 2010.

 1. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #1
  Dec 22, 2010
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Mwandishi wetu,
  Arusha

  JESHI la polisi mkoani Arusha, limekumbwa na kashfa nyingine, baada ya polisi wake wawili kutuhumiwa kuwateka vijana watatu waliokuwa wakifanyabiashara na kuwapora fedha na kuwalazimisha kujamiiana huku wakiwapiga picha katika eneo la Ikulu ndogo ya Arusha.

  Tukio la aina yake, ambalo tayari limeripotiwa polisi, lilitokea juzi kuanzia saa 5:00 asubuhi hadi saa 8:00 mchana na polisi kuwaachia huru. Vijana hao, walikuwa wakifanya biashara ya kuuza virutubisho vya mwili aina ya Arovela.

  Wakizungumza katika ofisi za Mwananchi jana,wafanyabiashara hao, Victoria Agustine(22),Evance Fank(24) Godbless Shirima(18), walisema walikamatwa na polisi hao, wakiwa wanapita nje ya jengo la Ikulu ndogo ambalo lipo jirani na Mahakama Kuu Kanda ya Arusha.

  Frank alisema wakiwa wanatembeza bidhaa hizo ambazo zinatolewa nakampuni ya Mwema General Supply ya Arusha, walipita mbele ya Ikulu, na polisi wawili walikuwa lindo waliwaita nawalipoingia ndani na Ikulu walianza kuwahoji maswali kuhusu biashara hiyo.

  Alisema ghafla waliambiwa kupiga magoti na kuweka mikono juu, na kuanza kupewa mazoezi ya kupiga pushapu, kuruka kichurachura na baadaye waliwataka kuwakabidhi fedha zote walizonazo.

  "Tulisema hatuna fedha, lakini mmoja alianza kutupekuwa na kuchukua Sh 200,000 za mauzo kwa kiongoziwetu Shirima,” alisema Frank.

  Frank alisema pamoja na kuchukua fedha hizo, pia waliwataka kutoa sadaka na walichukua kwa nguvu Sh 2,500 kutoka kwa kila mmoja.

  "Mimi nilikuwa nawaambia kama tumefanya makosa watupeleke polisi waligoma kabisa na walikuwa wakisisitiza tumefanya makosa kupita mbele ya Ikulu,"alisema Frank.

  Alisema baaday waliwavua nguo na kuwataka kufanya mapenzi na Fank na Victoria waliambiwa kukubatiana nakunyonyana ulimi.

  "Mimi nilikataa kufanya mapenzi wakanilazimisha huku, wakinipiga, lakini nilikataa na kulala ndipo walilazimisha tunyonyane ulimi na Victoria huku wakitupiga picha kwa simu ya mkononi,"alisema Frank.

  Naye Shirima ambaye alikuwa kiongozi, alisema wakati wanapigwa alimtambua polisi mmoja na akamuita kwa jina huku akiomba wasiendelee kuwatesa, lakini aligoma na kuendelea kuwapiga.

  "Tuliwakuta wamelewa na mimi namjua mmoja kabisa kwa jina(jina linahifadhiwa) nikamwambia mimi namjua na kaka yangu alikuwa polisi na pia kuna ndugu yangu ni ofisa wa Magereza Manyara, aliposikia hivyo alianza kunihoji ni wapi nilimuona nikamwambia ndipo alisema anatupeleka polisi, lakini tulipofikanjiani alituacha na kuondoka,"alisema Shirima.

  Mwandishi wa habari hizi, juzi aliwakuta wafanyabiashara hao, wakiwa wanatoa maelezo katika ofisi ya Mkuu wa upelelezi wilaya ya Arusha na baadaye kwa kamanda wa polisi mkoani Arusha, lakini hadi jana hakuna hatua ambazo zilikuwa zimechukuliwa.

  "Yule mkuu wa upelelezi badala ya kufungua kesi ya malalamiko yetu alianza kuzungumza na kiongozi wa walinzi wa Ikulu na kuomba tukutanishwe ili waombe msahama na akatuomba tuache namba za simu lakini hadi leo(jana) hajatupigia,"alisema Shirima.

  Vijana hao, wamelishauri jeshi la polisi kuchukua hatua kali dhidi ya polisi na kuwalazimisha kufuta picha walizowapiga ili zisisambaa mitaani.

  Alifafanua kuwa baada ya kufika kwa kamanda wa polisi mkoani Arusha, Thobias Andengenye alitusikiliza na kutueleza kuwa atatupigia simu, lakini pia hadi leo (jana) bado hajatupigia.

  Kamanda wa polisi mkoani Arusha, Thobias Andengenye hakupatikana jana kuelezea tuhuma hizo, baada ya simu yake ya mkononi kupokelewa na msaidizi wake aliyedai kuwa yupo katika kikao ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha. Pia saa 8:52 Mwananchi lilimpigia tena lakini simu yake haikupokelewa na ilikuwa ikita tu muda wote bila kujibiwa.

  Tukio hili ni mfululizo wa matukio ya unyanyasaji wa polisi kwa raia na hivi karibuni walituhumiwa kumpiga mbunge wa Jimbo la Arusha, Godbless Lema na pia waliwahi kutuhumiwa kuwauwa kwa risasi vijana wawili eneo la Kijenge, lakini hata hivyo hakuna hatua zilizochukuliwa.

  My take: Kama Andengenye ameshindwa kuwashughulikia polisi waliofanya unyanyasaji ule, Basi hatua kali zichukuliwe na IGP, Vinginevyo hata imani ndogo tuliyonayo dhidi ya polisi zitakuwa zimetoweka, tutaingia mtaani tukiwa tayari hata kufa kupambana na hili jeshi dhalimu la polisi.
   
 2. JOYCE PAUL

  JOYCE PAUL JF-Expert Member

  #2
  Dec 22, 2010
  Joined: Jan 8, 2010
  Messages: 1,007
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Poleni vijana mliokubwa na tukio hilo.
   
 3. c

  cesc Senior Member

  #3
  Dec 22, 2010
  Joined: Nov 25, 2008
  Messages: 156
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mmmhhh...ni kasha..ila inabidi uchunguzi ufanywe ili kulisafisha jeshi la polisi
  kwani sio polisi wote wako hivi..hatuwezi kusema samaki mmjoa akioza wote wameoza..sio kweli..uchunguzi wa kina kwanza
   
 4. Mwadui

  Mwadui Senior Member

  #4
  Dec 22, 2010
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 102
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  daah tunaelekea kubaya, na jeshi la polisi la Arusha lao moja ndo maana hawataki kuwachukulia hatua, kesi inatakiwa apelekewe Nahodha huenda atafanya jambo.
   
 5. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #5
  Dec 22, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Hawa ndiyo JK anawaamini walinde raia namali zao!!!

  Kazi ipo!! Poleni vijana wetu...
   
 6. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #6
  Dec 22, 2010
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Aibu tupu!
   
 7. semango

  semango JF-Expert Member

  #7
  Dec 22, 2010
  Joined: Aug 24, 2010
  Messages: 532
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  tatizo kubwa nadhani ni uongozi ndio maana hawa mabwana wadogo wanafanya wanavyotaka.fikiria mlinzi wa ikulu kalewa saa 5 asubuhi, kuna kitu hapo?hapo dawa huyo andengenye apigwe chini labda mambo yataenda.lakini kwa ninavyoona, wakuu wa nchi wanafurahia anavyowasumbua
  wana chadema so sioni uwezekano wa kupigwa chini.kilichobaki ni kuomba Mungu tu na kuvumilia huku tukingoja 2015 tujitoe kimasomaso kabla makame hajamuweka mbayuwai mwingine.
   
 8. Ndallo

  Ndallo JF-Expert Member

  #8
  Dec 22, 2010
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 7,127
  Likes Received: 1,083
  Trophy Points: 280
  Natumaini Andengenye unakibarua kigumu sana kwa mkoa wa Arusha!
   
 9. N

  NAHUJA JF-Expert Member

  #9
  Dec 22, 2010
  Joined: Aug 1, 2007
  Messages: 15,004
  Likes Received: 15,563
  Trophy Points: 280
  Mungu wangu hivi ni kweli au naota!!! ina maana hao polisi wako juu ya sheria au? jamani jamani jamani inatisha kusema kweli.
   
 10. P

  Prover Member

  #10
  Dec 22, 2010
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 23
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  washitakiwe kwa kosa la kulewa masaa ya kazi .kwa kosa la uporaji .kosa la uzalishaji .kosa la kusababisha hatari ya maambukizi. Kosa la kutmia madaraka vibaya pia nashauri wapeleke shauri hilo kwa HUMAN RIGHT ADVOCATES
   
 11. C

  Chief JF-Expert Member

  #11
  Dec 22, 2010
  Joined: Jun 5, 2006
  Messages: 1,488
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  I would just too happy to be proved wrong, lakini kwa hili, sisi watanzania hatuwezi. Nakumbuka mdada fulani miaka ile ya nyuma alituita sisi watanzania ni makondoo, na mpaka sasa ni kweli
   
 12. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #12
  Dec 22, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Hivi mawakili wa tanzania wa nini hawajitolei kesi kama hizi.

  Au kwa nini mawakili wasinunue hizi kesi za watu kunyanyaswa kuidabisha serikali na watendaji wake wabovu.

  I wish ningekuwa lawyer hawa vijana ningewatafuta na kuinunua kesi yao
   
 13. O

  Oldarasu Member

  #13
  Dec 22, 2010
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 45
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Nawashukuru wote mliotangulia kutoa mawazo. Jambo hili ni la aibu kubwa mno. Bill Clinton alipokuja Arusha aliuita mji wetu "Geneva of Africa" kwa maana kwamba ni mji salama. Je huu ndio usalama? Jambo hili linawahusu wote waliotajwa na waliochangia akiwemo JK, IGP, RPC Andengenye. Wasipowaadhibu hao polisi wanyang'anyi hatutawaelewa
   
 14. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #14
  Dec 22, 2010
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Inauma sana na kusikitisha!
   
 15. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #15
  Dec 22, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,253
  Likes Received: 19,383
  Trophy Points: 280
  haki za binadamu wako wapi jamani? hii kitu sio ya kuachwa hivi hivi
   
 16. n

  nkosiyamakosini Member

  #16
  Dec 22, 2010
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 83
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Aah! Tumechoka na uchochezi na uchakachuaji wa habari! sio kweli hii mada. thanks
   
 17. O

  Oldarasu Member

  #17
  Dec 22, 2010
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 45
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Kuwa na polisi wa aina hii ni sawa na kutokuwa na polisi kabisa. Kama polisi wanapora, wanalewa, wanawalazimisha watu kufanya vitendo vichafu vinavyoweza kuhatarisha maisha ya watu kwa maambukizi ya UKIMWI, hawa ni wabaya kuliko UKIMWI wenyewe. Nitawashangaa sana wakubwa wakiwaacha waendelee na kazi. Au ni watoto wa ndugu nini? Mheshimiwa JK na Mheshimiwa Mwema na Mheshimiwa Nahodha uliye na dhamana ya ulinzi wa raia ina maana hamjasikia hili na mengine mengi mabaya yanayofanywa na polisi? Chonde chonde tuondoleeni uhayawani huu
   
 18. semango

  semango JF-Expert Member

  #18
  Dec 22, 2010
  Joined: Aug 24, 2010
  Messages: 532
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  tunaomba ukweli unaoufahamu aisee.
   
 19. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #19
  Dec 22, 2010
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Soma Mwananchi ya leo
   
 20. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #20
  Dec 22, 2010
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Polisi hawa ndiyo walioandaliwa kukabiliana na vurugu za Uchaguzi hapa Arusha lakini ashukuriwe Mungu hakuna vurugu zilizotokea kwa busara za RPC waliyemuondoa Basilio Matei! Sijui kama ingekuwaje kama Matei angakuwa na akili kama za Mahita!
   
Loading...