Polisi wawakamata watetezi wa kura ya maoni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Polisi wawakamata watetezi wa kura ya maoni

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by abdulahsaf, Apr 20, 2012.

 1. a

  abdulahsaf JF-Expert Member

  #1
  Apr 20, 2012
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  [h=1][/h]Posted on April 20, 2012 by zanzibaryetu
  [​IMG]Hashim na wenzake wakiwa katika gari la Jeshi la Polisi likiwachukua na kuwapeleka Madema, baada ya kukusanyika katika viwanja vya baraza la wawakilishi wakidai kuwepo kwa kura ya maoni itakayoamua kuwepo au kutokuwepo Muungano

  JESHI la Polisi Zanzibar limewatia mbaroni zaidi ya watu 12 wakiwemo viongozi wa kundi la wanaotaka kuitishwe kura ya maoni kuhusu Muungano, baada ya kukataa kutii amri ya jeshi hilo iliyowataka kuondoka katika viwanja vya baraza la wawakilishi jana.[​IMG][​IMG]Kundi la watu zaidi ya 40 lilifika katika viwanja vya baraza la wawakilishi huko Chukwani wakitaka kuonana na Spika wa baraza hilo, Pandu Ameir Kificho ambapo kabla ya kukutana Spika alimuagiza Katibu wake Yahya Khamis Hamad kuongea na wananchi hao.
  Wakizungumza nje ya viwanja hivyo wananchi hao walisema lengo lao ni kuonana na Spika Kificho ili kuwasilisha ombi lao la kutaka kupelekwa hoja binafsi ya kuitishwa kura ya maoni ya kutaka au kukataa Muungano.
  Katibu wa baraza hilo alisema sio vibaya wananchi hao kuwasilisha mapendekezo hayo kwa Spika, lakini aliwataka wananchi hao kufuata utaratibu unaokubalika wa majadiliano na sio kurufika katika viwanja hivyo jambo ambalo linatishia usalama wa chombo hicho muhimu ambacho kinaendelea kujadili masuala mbali mbali nchi.
  “Waheshimiwa pengine mmekuja hapa kwa nia njema kabisa lakini kwa utaratibu huu nimelazimika kuja hapa nje na kukuombeni muondoke ili muache shughuli za baraza ziendelee kwa sababu sipendi kuona mkipambana na jeshi la polisi katika viwanja hivi” alisema Katibu huyo. Na kuongeza.
  “Hata Spika alisema kwa utaratibu kama huu hataweza kuwaruhusu kuonana naye lakini kama mtafuata utaratibu mzuri ambao umewekwa na tumeuainisha ndani ya barua zenu basi mnaweza kukutana na kuongea naye, lakini kwa hali kama hii haitawezekana kwa sababu shughuli za baraza zinaendelea lakini pia wananchi wanashindwa kupita hapa na kufanya shughuli zao kwa kuwa mmefunga njia, waheshimiwa wanataka kuja hapa lakini wanashindwa kutokana na hali hii” alisema Katibu Hamad.
  Mapema wananchi hao wakiongozwa na Rashid Salum Adiy walifika katika viwanja hivyo kwa wingi wakiwa na mabango yao yenye ujumbe wa kutaka kuitishwa kwa kura ya maoni kuamua mustakabali wa Zanzibar ambapo walitaka kuingia ndani na kuonana na uongozi wa baraza hilo.
  Hata hivyo jeshi la polisi lilitoa tahadhari na kuwataka waondoke katika viwanja hivyo na kuelekea nyumbani ili kupisha viongozi wa wajumbe wa baraza la wawakilishi kuwasili katika baraza hilo ili waendelee na shughuli za baraza hilo ambalo jana limeakhirishwa.
  Rashid Sulum Adiy ni kiongozi wa kundi hilo la wazanzibari wenye kudai kuitishwa kura ya maoni juu ya mustakabali wa Zanzibar ndani ya Muungano na anataka baraza la wawakilishi liitishe kura ya maoni ya kuwauliza wazanzibari iwapo wanautaka Muungano au hawautaki.
  Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Aziz Juma Mohammed amesema jeshi lake limejipanga vyema na halitavumilia watu ambao wanakwenda kinyume na sheria. Kamanda alisema watu waliokwenda katika viwanja vya baraza hilo hawakufuata taratibu na hivyo jeshi halitavumilia tena vitendo ambavyo vinakwenda kinyume na sheria na litawashughulikia wale wenye kutoa lugha za matusi katika matamshi yao ambao wanaoendesha mikutano katika maeneo mbali mbali ndani ya jamii.
  Katika barua yao walioiwasilisha kwa Spika Kificho ya Aprili 18 mwaka huu inasema “ Sisi ni wananchi 1825 miongoni mwa watu 300,000 sote wazanzibari na ni watu wazima wenye akili timamu kutoka majimbo 50 ya Unguja na Pemba tunakutaka utuwasilishie mbele ya baraza la wawakilishi ombi la hoja yetu binafsi ya kuwepo kwa kura ya maoni juu ya suala la Muungano wa Tanzania” ilisema barua hiyo.
  Wakitilia mkazo hoja hiyo katika barua yao walisema baada ya kipindi cha miaka 48 ya Muungano hoja yao hiyo ya kuitisha kura ya maoni ni muhimu sana kwa wazanzibari na vizazi vya baadae.
  “Hatukubali kama tutapigwa mabomu, marungu au kukamatwa kwa sababu ya hatari inayotukabili mbele yetu. Kwa hivyo kwa heshima na tunaliomba baraza nalo lishirikiane na sisi kwa kutumiza wajibu wake na kulikubali ombi letu la kuwa na kura ya maoni juu ya Muungano” ilisema barua hiyo ambayo MWANANCHI inayo kopi yake.
  Barua hiyo imesema Muungano huo umekosa misingi ya kisheria ya kitaifa na kimataifa, na ndio sababu ya kuongezeka kero na kasoro kadhaa, lawama na matatizo mbali mbali yanayoshindikana kutatuliwa kwa pande mbili hizo.
  Walisema kwa kuwa Muungano huo unahusu nchi mbili tofauti, za Zanzibar na Tanganyika ni vizuri wananchi wakapewa nafasi ya kuhojiwa iwapo wanautaka uendelee au uvunjike kwani maamuzi ya wananchi ndio yanayotegemea kuendeleza usalama na utulivu uliopo.
  Hivi karibuni Rais Kikwete aliteuwa tume ya kukusanya maoni juu ya katiba mpya na tayari wajumbe wa tume hiyo wameshaapishwa na wataanza kazi rasmi mwanzoni mwa mwezi ujao lakini malalamiko juu ya suala hilo yamekuwa yakijichomoza kila siku hapa Zanzibar.
  Makundi mbali mbali yamekuwa yakifanya mikutano ya wazi kuelezea suala hilo huku idadi kuwa ya wazanzibari wakiunga mkono hoja ya kuwepo kura ya maoni kwanza kabla ya tume kuanza kufanya kazi zake.
   
Loading...