Polisi wavamia wodi, wapiga mtuhumiwa

Mtu wa Pwani

JF-Expert Member
Dec 26, 2006
4,187
670
Polisi wavamia wodi, wapiga mtuhumiwa
2008-06-16 09:17:03
Na Patrick Chambo, PST Moshi


Watu watatu wanaosadikiwa kuwa ni askari wa upelelezi wa Kituo Kikuu cha Polisi mjini Moshi, wanadaiwa kuvamia wodi namba tatu ya hospitali ya mkoa ya Mawenzi na kumshambulia mtuhumiwa wa ujambazi, Joeli Makundi aliyekuwa amelazwa hospitalini hapo.

Makundi ambaye ni mkazi wa Marangu, alipata kipigo hicho kwa madai ya kukaidi amri ya askari hao ya kumtaka aondoke hospitalini hapo ili akajibu tuhuma dhidi yake akiwa nyumbani kwake.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana hospitalini hapo, askari hao walimshawishi daktari anayemtibu kumuandikia mgonjwa huyo kuwa amepona ili azma yao ya kuondoka naye itimie.

Kutokana na kitendo hicho cha askari kumpiga mgonjwa akiwa chini ya uangalizi wa madaktari, Maofisa waandamizi wa Jeshi la Polisi na wa serikali wamekuwa wakienda hospitalini hapo mara kwa mara, ikiwa ni hatua ya kujisafisha kwa kuowaomba radhi wagonjwa na uongozi wa hospitali kwa kufanya kitendo kinyume na maadili ya jeshi na ya haki za mgonjwa.

Akizungumza kwa shida katika wodi namba tatu huku akiwa na pingu miguuni, Makundi alisema kuwa kipigo alichopata kutoka kwa polisi wiki iliyopita hospitalini hapo ni muendelezo wa vipigo alivyokuwa anavipata kwenye chumba maalumu cha mateso cha polisi mjini Moshi, akishinikizwa akiri kosa lake.

Kwa mujibu wa mtuhumiwa huyo, alipigiwa simu na polisi kuwa mke wake yuko polisi na ataachiwa endapo yeye atafika kituoni hapo kwakuwa wanamtafuta yeye.

Alisema alipofika alipokelewa kwa kipigo na mateso hadi alipozinduka akiwa hosipitalini hapo akiwa na majeraha na bendeji mguuni na alipopatiwa kipigo tena mbele ya wagonjwa na kuzinduka aliambiwa ameshasomewa kesi na hakimu kitandani hapo inayohusu ujambazi wa kutumia silaha, ingawa alidai hajui chochote.

Mkuu wa wilaya ya Moshi, Bw. Musa Samizi, Mganga Mkuu wa hosiptali ya Mawenzi, Dk. Kapalala Saganda na Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Bw. Ramadhani Baruti, wamethibitisha jana kutokea kwa tukio hilo.

Akizungumzia suala hilo, Dk. Saganda alisema kuwa anaandaa taarifa maalumu ya tukio hilo na kuiwasilisha kwa Mganga Mkuu wa Hospitali ya mkoa wa Kilimanjaro, ili amkabidhi Mkuu wa Mkoa huo, sababu za daktari wake kutoa ruhusa kwa mgonjwa ambaye alikuwa akiendelea na matibabu.

``Kwa kweli tukio hili lipo na mimi kama Mganga Mkuu naandaa taarifa kwa mkuu wa mkoa kama alivyotuagiza, halafu nitampatia mganga mkuu aitoe. Ninyi kama waandishi siwezi kuwapatia taarifa kwa kuwa mimi sio msemaji wa hosptitali, mfuateni Kamanda wa Polisi au subirini RMO aje,`` alisema.

Mkuu wa wilaya ya Moshi, Bw. Samizi, alisema anakusudia kutoa taarifa kamili ya tukio hilo leo kwa kuwa alikuwa katika ziara ya Waziri Mkuu.

Naye Kaimu Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Kilimanjaro, Bw. Baruti, alisema na yeye alikuwa katika ziara hiyo hivyo hakuwa katika mazingira mazuri ya kuelezea suala hilo kwa undani.

``Samahani nitakatufuta mwenyewe bado niko hapa Mbuyuni nikifika nitakupa taarifa`` alisema.

Baadhi ya madaktari waliozungumza na Nipashe walisema kuwa matukio ya wahalifu kupigwa wodini hapo na polisi ni mambo ya kawaida na kuwa hivi karibuni mfungwa mmoja alitolewa \'dripu\' na askari Magereza akidai ameagizwa na mkuu wake kuwa hakuna askari wa kumlinda.

Walimuomba mkuu wa mkoa na kamanda wa polisi kuendesha upelelezi mzuri katika tukio hilo ili kuondoa dhana ya kuwadhalilisha wagonjwa na madaktari kila wakati, na kwamba daktari aliyetoa ruhusa ya kumtoa mgonjwa wodini akigundulika achukuliwe hatua za kisheria.

SOURCE: Nipashe
 
Uonevu uliopitiliza.Sasa hapo wahusika pamoja na madaktari inabidi wawe responsible.

Btw: Mtu wa Pwani bado unasubiriwa kuomba msamaha
 
Huu ndiyo shy , Kada na genge lao wanaita ni utawala bora .Huku ndiyo serkali ya JK inaitwa kuheshimu haki aza binadamu .Ndiyo hawa wanao ilinda CCM maana hata ikiwa vipi hawawezi kuwakamata na kuwapata adhabu .Unamkamata mke wa mtu kwa kosa la mumewe sheria inasemaje wana sheria wa JF ?
 
Askari wa Tanzania wanatumia glucose(nguvu) nyingi kuliko akili.
Hospitali ni taasisi nyingine ya serikali kwa nini wasifuate taratibu?Kuwa askari si kwamba wao hawana makosa na wana haki ya kuwapiga raia(wanaiona kesi ya Zombe???).B.S
 
Haya matatizo yapo sana kule Pemba lakini masikini za mngu hawana wa kuwasemea wala kuwatetea.
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom