Polisi wavamia Ofisi za jimbo ACT Mbagala Kuu na kukamata Viongozi na Mawakala

Shujaa Mwendazake

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
3,735
6,291
Ofisi ya Jimbo la Mbagala Kuu ya ACT Wazalendo imevamiwa na Polisi Mida ya jioni jana jumamosi na wakalazimisha kuwakamata watu wote waliopo ambao ni pamoja na viongozi na Mawakala kwa hoja kuwa wameweka mkusanyiko usio halali.

Kwa hiyo Sasa RASMI mikusanyiko kote nchini HAIRUHUSIWI? Mkusanyiko halali ukoje? Vipi haki ya kikatiba ya kukusanyika?
Mama Samia haya mambo Yana baraka zako? Unahisi yatakusaidia "kusimamisha" uchumi?

Huoni kuwa haya matendo yataharibu taswira yako kimataifa?

Umeshasahu mara hii madhara ya chuki za kisiasa zilizopitiliza nyakati za ugonjwa mpaka msiba?
===
1626593697125.png

1626593528664.png
 
Endeleeni na chuki zenu maana hizo chuki hata zisipo kuwapo bado hakuna kiwango cha kodi kitaongezeka.

Kazi yenu ninkuwazia matumbo yenu tu na kutaka kumkwamisha huyu mama.

Fanyeni mikutano yabkuleta maendeleo na sio hiyo yenu ya kupinga mambo na kutaka mambo ya kushibisha matumbo yenu
 
Nawashukuru sana Polisi wanatusaidia kuisagia kunguni CCM na Serikali yake. Polisi endeleeni hivyo hivyo mkikuta wapinzani pigeni tu hata kuua ueni tu, Serikali iatawalinda kwa niaba ya CCM
 
Rais alishatoa msimamo wake alipojibu waandishi wa habari. Unataka aseme vipi zaidi uelewe?
Kwa hiyo katiba kaamua kuivunja halafu na sisi tukae kimya katiba inavunjwa. Nchi za afrika zina matatizo ndo mana trump alituita shithole
 
Alisema anaponya majeraha, LAKINI NAONA AMEAMUA KUTENGENEZA MAJERAHA YAKE...
Nakumbuka wakati fulani JK alikuwa anampa ushauri mkuu wa UDSM aliyechukua nafasi ya Profesa Mukandara alisema hivi: usirithi maadui wa mtangulizi wako,naona ushauri huu amempa pia Samia hivyo naye anatengeneza wahanga wake,hakika CCM ni ile ile.
 
Back
Top Bottom