napingana na wewe , ubinadamu hautegemei elimu yako. kwani kuna watanzania wangapi hawajasoma kabisa na hawana matendo maovu kama ya polisi hawa?. tatizo si la askari wanaopigana mbele, si elimu yao au ubora wa vyeti vyao ni tatizo la dola nzima, ni tatizo la kisheria, nitatizo la maadili ya kazi, ni tatizo la mfumo. ni tatizo lako, ni tatizo langu. amka sasa, niamke sasa, tukeshe tukitafuta iliyo haki kwetu na
kwa vizazi vijavyo
polisi wetu wengi wao ni failures masomoni nndo tatizo lao
KOVU LA UKATILI WA JESHI LA POLISI DHIDI YA RAIA NCHINI:
WATANZANIA TUNAJIBU GANI KWA 'MACHOZI YA LAANA NA KILIO CHA HAKI YA MWANAMAMA WINFRIDA JOHN' WA KIJIJI CHA NYOLOLO MKOANI IRINGA ???
Kamanda Winfrida John, kada wa CHADEMA kijiji cha Nyololo, bila shaka wewe ni mwana mama mtu mdogo tu hapo kijijini Nyololo ambaye pengine hata mbunge wa eneo hilo huenda asikufahamu kitu achilia mbali wakuu wa wilaya na mkoa huko Mufindi na Iringa kwa mpangilio huo, ila kwa wachache sana tena wenye jicho la mwewe angani huenda lako hili la kipekee mno likawa limewagusa nao pia.
Naam, kabla sijaandika mengi juu yako na kile kilichonigusa mno kwako kwanza niombe kwamba tafadhali Mama Winfrida futa machozi yako, yale ya akinamama wengine wengi zaidi hapo Nyololo na kwamba katu usiendelee kutuhuzunisha zaidi sisi WaTanzania wenzako kwa uchungu wote huo; machozi yako hadharani ya KULILIA HAKI na kutuhoji sote kama taifa tukupe jibu UHURU WAKO WA MAONI, NA KUJUMUIKA ulikopotelea;
Ni kweli kwamba siku hiyo 'SIMBA MLA WANYONGE WANAAOLILIA HAAKI' alipomnyakua makuchani Mtanzania wa 22 (Daudi Mwangosi) afiaye mikononi mwa dola kwa visingizio mbalimbali za kisiasa tangu mwaka huu, bila shaka watu wengi tu hapo Nyololo, Itete na hata vijiji vingine vya mbali sana nao walilia ila wewe hapo chozi laako linageuka kuwa chozi la dhahabu si kwa kuwa tu ulikua kwenye eneo la tukio baali zaidi ni kwamba ni mmoja kati ya wenyeji waliotembelewa naa CHAADEMA kwa shughuli ya ufunguzi wa ofisi mahali haapo.
Hakika ni kutokana na udhahabu huo wa chozi lako tena ukiwaa ni mwanamama tu mnaohitajika kuimarishwa zaidi kushiriki katika siasa na uongozi wa taifa, inanifanya nisiamini tu kwamba hivi karibuni huenda ukawa ni mtu wa kutafutwa sana japo sauti na vyombo vingi vya nyumbani hapa na vile vya kimataifa kama vile BBC, VoA, Deuche Welle ...
... bali zaidi najikutaa pia nikiwa sina wasi wasi kwamba Mama Hellen Kijo Bisimba naye amekusikia popote alipo, naamini kwamba msururu wako wa maswali ya msingi sana uliyoyauliza siku hii hata Jaji Mkuu Mstaafu Augustino Ramadhani umemuacha hana amani moyoni;
Ndio, kwa mtaji w kilio chako kikiwakilicha KILIO CHA HAKI kwetu sisi WaTanzania kwa ujumla wetu bila shaka ni wazi kwamba tayari umetuma ujumbe mzito kiasi cha kuwalazimisha hata magwiji wa habari nchiki akina Mzee Jenerali Ulimwengu, Fred Masako, Mzee Mwanakijiji, pamoja na Pasco wa JF.
Nasema kwa kilio cha mwanamama 'kiumbe dhaifu' katika jamii yetu hii inayoendekeza ufalme wa akina-baba tu kwamba vile vile utakua umewakuna akina Mama Nkya, Ayub Ryoba, Muhingo Rweyemamu pamoja na wengine kibao, waondoke kwenye viyoyozi maofisini na kuanza kupiga kiguu na njia wao wenyewe bila kumuagiza mwandishi yeyote wa chini, kwenda kukutafutia majibu sahihi na murua zaidi kiasi cha kuweza kukufuta machozi wewe na vizazi vijavyo;
Mama Winifrida, kwa kilio hiki hapo kijijini Nyololo ni wazi kwamba tayari umewakilisha sauti dhaifu za akina mama wote na watoto Tanzania ambao kweli siku Daudi Mwangosi alipogeuka RUNDO LA NYAMA hapo kijijini kwenu(kwa hisani ya maagizo ya serikali ya CCM) - wenzetu mmeonekana kuteseka mno kukimbia ovyo na vichanga kuokoa maisha huku mkidhalilishwa na mgeni wenu CHADEMA ambaye ndiye kwanza mlikua mnamkaribisha rasmi hapo kijijini kwenu kwa kumpa eneo akafungulie ofisi yake (kwa mujibu wa sheria na katiba ya nchi) lakini ukarimu wenu wote ukahitimishwa na kilio cha historia yote Nyololo kugeuka ghafla kuwa uwanja wa mauji kama Syria.
Naam, nielewavyo mimi ni kwamba mama yetu Winfrida, hadi hapo ni kwamba tayari umewaamrisha wanaharakati kama Kijana mwenzetu Kibodya, Tundu Lissu, Deus Mallya, Prof Shivji, John Tendwa, pamoja na Mhe Augustino Mrema.
Wengine zaidi ambao wapende wasipende machozi yako ya haki bila shaka yako mabegani mwao ni pamoja na Prof Palamagamba Kabudi, Madam Spika wa Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania, Mama Makinda, Prof Safari, Prof Maina, Prof Baregu, Dr Kitila Mkumbo, Dr Azaveli.
Ndio, nasema hawa waheshimiwa wote wanao wajibu kwako usiokwepeka kutoa jawabu kamili tena lisilocha maswali, kila mmoja kwa wakati wake, wakwambie kwamba kwenye katiba mpya wao wanategemea kuona Jeshi la Polisi la aina gani ili Winfrida John wa miaka hiyo ijayo wao wasije wakajikuta wakilia kilio kile kile kilichokumuaga machozi hapo Nyololo.
WaTanznia wote bila kujali itikadi za kidini na kisiasa, je tunalo jibu gani kwa mama huyu Winfrida John wa kijiji cha Nyololo ikiwa ni kielelezo cha kilio cha akina mama wengine wengi zaidi wasiokua na majina katika jamii yetu hii wangali nao wanao wachozi yasiokauka kulilia haki kama vile kule Igunga, Arumeru Mashariki, mauji ya Pemba, Arusha, Tarime, Mbeya ...?
Hakika kuna nafsi inaongea ndani yao na iko siku tutaamka na kusikia Police wameandamana dhidi ya amri ya kuua bila hatia wala njama mbaya.