Polisi waumbuka kwa kifo cha Mwangosi ushahidi ni huu. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Polisi waumbuka kwa kifo cha Mwangosi ushahidi ni huu.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mchonga, Sep 9, 2012.

 1. mchonga

  mchonga JF-Expert Member

  #1
  Sep 9, 2012
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,250
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 2. Return Of Undertaker

  Return Of Undertaker JF-Expert Member

  #2
  Sep 9, 2012
  Joined: Jun 12, 2012
  Messages: 2,376
  Likes Received: 8,520
  Trophy Points: 280
  Mi unyama mkubwa sana
   
 3. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #3
  Sep 9, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  ... bwana ametoa, bwana ametwaa ... jina la Mungu lihimidiwe sawa sawa na mapenzi yake; pumzika kwa amani na starehe ya milele Kamanda Mwangosi!!!!!!!!!!!!

   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 4. mwaJ

  mwaJ Tanzanite Member

  #4
  Sep 9, 2012
  Joined: Sep 27, 2007
  Messages: 4,076
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Ni bora niache kuangalia picha za mwili wa marehemu Daudi Mwangosi maana akili imeshindwa kuzoea. Kila nikiziona naumwa ghafla. Eeh Mwenyezi Mungu umrehemu umpe pumziko la amani na wale waliomtendea hivyo ukawalipe kwa stahili yao.
   
 5. Jodoki Kalimilo

  Jodoki Kalimilo JF-Expert Member

  #5
  Sep 9, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 8,631
  Likes Received: 2,055
  Trophy Points: 280
  Aisee inahuzunisha ukiangalia huo mwili wa Mwangosi
   
 6. Jodoki Kalimilo

  Jodoki Kalimilo JF-Expert Member

  #6
  Sep 9, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 8,631
  Likes Received: 2,055
  Trophy Points: 280
  Nahisi police wengi wakistaafu huwa wanaishi katika majuto sana na ndio maana wanakufa mapema
   
 7. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #7
  Sep 9, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,950
  Likes Received: 1,275
  Trophy Points: 280
  eeh Mungu! Hali hii Mwigulu na Nape wanafurahi kazi yao imefanyika
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 8. Bishop Hiluka

  Bishop Hiluka Verified User

  #8
  Sep 9, 2012
  Joined: Aug 12, 2011
  Messages: 4,100
  Likes Received: 1,424
  Trophy Points: 280
  OMG! Ni wapi nchi hii inaelekea?...
   
 9. N

  Ninaweza JF-Expert Member

  #9
  Sep 9, 2012
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 7,170
  Likes Received: 1,173
  Trophy Points: 280
  Vifo hivi vinaletwa kwetu na polisi kwa hisani ya wana ccm!
   
 10. RGforever

  RGforever JF-Expert Member

  #10
  Sep 9, 2012
  Joined: Apr 3, 2011
  Messages: 6,165
  Likes Received: 1,890
  Trophy Points: 280
  Unaweza kuiweka Vizur Hiyo Link Mkuu! Mi naona Acces inakuwa Ngumu! Niwekee Hata TITLE YAKE
   
 11. U

  Udaa JF-Expert Member

  #11
  Sep 9, 2012
  Joined: Jun 8, 2012
  Messages: 727
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nape nape,hivi unana picha hizi,kama umeona unapataje ujasiri wa kutetea policeccm au unaushetani ndani mwako,mwandos na mwanadam hakustahiri kuuwawa kinyama vile.
   
 12. Watu8

  Watu8 JF-Expert Member

  #12
  Sep 9, 2012
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 47,334
  Likes Received: 2,645
  Trophy Points: 280
  yaani ndhani tuite masalia ya mwili
   
 13. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #13
  Sep 9, 2012
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,823
  Likes Received: 10,120
  Trophy Points: 280
  kwanini huyu mbwa hajijiuzuliu hadi leo
   
 14. Jodoki Kalimilo

  Jodoki Kalimilo JF-Expert Member

  #14
  Sep 9, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 8,631
  Likes Received: 2,055
  Trophy Points: 280
  Mie huwa najiuliza hivi kwanini police huwa wanajawa na hasira binafsi mwananchi either anapofanya kosa au wanapotoa amri zao ambazo wananchi wanazigomea? huwa najiuliza kwa mantinki kwamba aliekosewa ni serikali na si police kama police hivyo anachotakiwa police ni kumkamata kwa amani na kumpeleka sehemu inapohusika labda kama anaekamatwa ametumia nguvu hapo anadhibitiwa kidogo akitii amri wanamwacha lakini police wetu unakuta kakunja uso utasema umemtukana yeye wakati kilichovunjwa ni sheria iliyotungwa na bunge (tena si kuvunjwa bali niite mtu anatuhumiwa kuvunja sheria) na anatakiwa ampleke mahakamani ili haki itendeke. Nikiangalia mahakimu wanavyofanya kazi pamoja na mapungufu yaliyoko huko nadhani kama police ndio wangekuwa wanahukumu watu wangeweza kufungwa hata miaka 30 kwa kosa la miezi 6 au mwaka na ndio maana kesi zao nyingi zenye maslahi ya taifa huwa wanashindwa mahakamani kwa kushindwa kuelewa vifungu vya sheria vya kumtia hatiani mtuhumiwa kwa kuwa wao wapo mannually zaidi
   
 15. tatanyengo

  tatanyengo JF-Expert Member

  #15
  Sep 9, 2012
  Joined: Mar 30, 2011
  Messages: 1,140
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Anayewatetea polisi kwa tukio hili atakuwa na matatizo.
   
 16. f

  fukunyungu JF-Expert Member

  #16
  Sep 9, 2012
  Joined: May 16, 2011
  Messages: 726
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 45
  polisi wetu wengi wao ni failures masomoni nndo tatizo lao
   
 17. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #17
  Sep 9, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  KOVU LA UKATILI WA JESHI LA POLISI DHIDI YA RAIA NCHINI:
  WATANZANIA TUNAJIBU GANI KWA 'MACHOZI YA LAANA NA KILIO CHA HAKI YA MWANAMAMA WINFRIDA JOHN' WA KIJIJI CHA NYOLOLO MKOANI IRINGA ???


  Kamanda Winfrida John, kada wa CHADEMA kijiji cha Nyololo, bila shaka wewe ni mwana mama mtu mdogo tu hapo kijijini Nyololo ambaye pengine hata mbunge wa eneo hilo huenda asikufahamu kitu achilia mbali wakuu wa wilaya na mkoa huko Mufindi na Iringa kwa mpangilio huo, ila kwa wachache sana tena wenye jicho la mwewe angani huenda lako hili la kipekee mno likawa limewagusa nao pia.

  Naam, kabla sijaandika mengi juu yako na kile kilichonigusa mno kwako kwanza niombe kwamba tafadhali Mama Winfrida futa machozi yako, yale ya akinamama wengine wengi zaidi hapo Nyololo na kwamba katu usiendelee kutuhuzunisha zaidi sisi WaTanzania wenzako kwa uchungu wote huo; machozi yako hadharani ya KULILIA HAKI na kutuhoji sote kama taifa tukupe jibu UHURU WAKO WA MAONI, NA KUJUMUIKA ulikopotelea;

  Ni kweli kwamba siku hiyo 'SIMBA MLA WANYONGE WANAAOLILIA HAAKI' alipomnyakua makuchani Mtanzania wa 22 (Daudi Mwangosi) afiaye mikononi mwa dola kwa visingizio mbalimbali za kisiasa tangu mwaka huu, bila shaka watu wengi tu hapo Nyololo, Itete na hata vijiji vingine vya mbali sana nao walilia ila wewe hapo chozi laako linageuka kuwa chozi la dhahabu si kwa kuwa tu ulikua kwenye eneo la tukio baali zaidi ni kwamba ni mmoja kati ya wenyeji waliotembelewa naa CHAADEMA kwa shughuli ya ufunguzi wa ofisi mahali haapo.

  Hakika ni kutokana na udhahabu huo wa chozi lako tena ukiwaa ni mwanamama tu mnaohitajika kuimarishwa zaidi kushiriki katika siasa na uongozi wa taifa, inanifanya nisiamini tu kwamba hivi karibuni huenda ukawa ni mtu wa kutafutwa sana japo sauti na vyombo vingi vya nyumbani hapa na vile vya kimataifa kama vile BBC, VoA, Deuche Welle ...

  ... bali zaidi najikutaa pia nikiwa sina wasi wasi kwamba Mama Hellen Kijo Bisimba naye amekusikia popote alipo, naamini kwamba msururu wako wa maswali ya msingi sana uliyoyauliza siku hii hata Jaji Mkuu Mstaafu Augustino Ramadhani umemuacha hana amani moyoni;

  Ndio, kwa mtaji w kilio chako kikiwakilicha KILIO CHA HAKI kwetu sisi WaTanzania kwa ujumla wetu bila shaka ni wazi kwamba tayari umetuma ujumbe mzito kiasi cha kuwalazimisha hata magwiji wa habari nchiki akina Mzee Jenerali Ulimwengu, Fred Masako, Mzee Mwanakijiji, pamoja na Pasco wa JF.

  Nasema kwa kilio cha mwanamama 'kiumbe dhaifu' katika jamii yetu hii inayoendekeza ufalme wa akina-baba tu kwamba vile vile utakua umewakuna akina Mama Nkya, Ayub Ryoba, Muhingo Rweyemamu pamoja na wengine kibao, waondoke kwenye viyoyozi maofisini na kuanza kupiga kiguu na njia wao wenyewe bila kumuagiza mwandishi yeyote wa chini, kwenda kukutafutia majibu sahihi na murua zaidi kiasi cha kuweza kukufuta machozi wewe na vizazi vijavyo;

  Mama Winifrida, kwa kilio hiki hapo kijijini Nyololo ni wazi kwamba tayari umewakilisha sauti dhaifu za akina mama wote na watoto Tanzania ambao kweli
  siku Daudi Mwangosi alipogeuka RUNDO LA NYAMA hapo kijijini kwenu(kwa hisani ya maagizo ya serikali ya CCM) - wenzetu mmeonekana kuteseka mno kukimbia ovyo na vichanga kuokoa maisha huku mkidhalilishwa na mgeni wenu CHADEMA ambaye ndiye kwanza mlikua mnamkaribisha rasmi hapo kijijini kwenu kwa kumpa eneo akafungulie ofisi yake (kwa mujibu wa sheria na katiba ya nchi) lakini ukarimu wenu wote ukahitimishwa na kilio cha historia yote Nyololo kugeuka ghafla kuwa uwanja wa mauji kama Syria.

  Naam, nielewavyo mimi ni kwamba mama yetu Winfrida, hadi hapo ni kwamba tayari umewaamrisha wanaharakati kama Kijana mwenzetu Kibodya, Tundu Lissu, Deus Mallya, Prof Shivji, John Tendwa, pamoja na Mhe Augustino Mrema.

  Wengine zaidi ambao wapende wasipende machozi yako ya haki bila shaka yako mabegani mwao ni pamoja na Prof Palamagamba Kabudi, Madam Spika wa Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania, Mama Makinda, Prof Safari, Prof Maina, Prof Baregu, Dr Kitila Mkumbo, Dr Azaveli.

  Ndio, nasema hawa waheshimiwa wote wanao wajibu kwako usiokwepeka kutoa jawabu kamili tena lisilocha maswali, kila mmoja kwa wakati wake, wakwambie kwamba kwenye katiba mpya wao wanategemea kuona Jeshi la Polisi la aina gani ili Winfrida John wa miaka hiyo ijayo wao wasije wakajikuta wakilia kilio kile kile kilichokumuaga machozi hapo Nyololo.

  WaTanznia wote bila kujali itikadi za kidini na kisiasa, je tunalo jibu gani kwa mama huyu Winfrida John wa kijiji cha Nyololo ikiwa ni kielelezo cha kilio cha akina mama wengine wengi zaidi wasiokua na majina katika jamii yetu hii wangali nao wanao wachozi yasiokauka kulilia haki kama vile kule Igunga, Arumeru Mashariki, mauji ya Pemba, Arusha, Tarime, Mbeya ...?
   
 18. K

  Kindimbajuu JF-Expert Member

  #18
  Sep 9, 2012
  Joined: Jul 8, 2009
  Messages: 711
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35

  napingana na wewe , ubinadamu hautegemei elimu yako. kwani kuna watanzania wangapi hawajasoma kabisa na hawana matendo maovu kama ya polisi hawa?. tatizo si la askari wanaopigana mbele, si elimu yao au ubora wa vyeti vyao ni tatizo la dola nzima, ni tatizo la kisheria, nitatizo la maadili ya kazi, ni tatizo la mfumo. ni tatizo lako, ni tatizo langu. amka sasa, niamke sasa, tukeshe tukitafuta iliyo haki kwetu na
  kwa vizazi vijavyo
   
 19. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #19
  Sep 9, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,744
  Likes Received: 1,454
  Trophy Points: 280
  Very well said analytically.
   
 20. a

  afwe JF-Expert Member

  #20
  Sep 9, 2012
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 4,087
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  Pamoja na uhodari tulionao wa kudadavua hoja katika threads mbalimbali hapa JF, hii imetuliza machozi na bila shaka kuhitimisha kwa Kuapa na kuahidi KUTOIPENDA CCM NA SERIKALI YAKE KAMWE katika muda itakaokuwa hai.
   
Loading...