Polisi waua tena

oba

JF-Expert Member
Oct 31, 2010
310
65
Kama kawaida, vyombo vya dola vikiongozwa na polisi huko Geita vimeripotiwa kumuua mtu mmoja na kuwajarehi wengine kwa risasi za moto wakati raia hao wa kata moja ya Geita kuandamana kwa amani wakishinikiza diwani wao ajiuzuru baada ya diwani wao huyo kushiriki katika baraza la madiwani kumwondoa kiongozi aliyesadikiwa kutetea maslahi ya wananchi. Wananchi wanauliza, sisi ndio tuliomchagua diwani wetu na tuna haki ya kumwondoa tumepigwa na polisi kwa nini?
Source; ITV saa 8 usiku

wananchi wa geita,wamefanya maandamano ya kumtaka diwani wao atoke madarakanii kwa kile kinachodaiwa alisababisha mkuu wa halmashauri kujiuzulu hapo juzi.Lakini mapolisi wametokea na kuwapiga wananchi,huku wakivunja nyumba za watu na kutumia risasi kunyamazisha maandamano hayo jamani tanzania tunaelekea wapi?
source itv habari saa 2 usiku

Kwa hali hii uvumilivu kwa kisingizio cha kudumisha amani na utulivu sasa basi. Inabidi tuanze kujibu mapigo kwa wahusika mmoja baada ya mwingine. Niliumia sana nilipoona hata kikongwe kapigwa na polisi kwa kufuatwa ndani ya nyumba yake.

....... Niliumia sana nilipoona hata kikongwe kapigwa na polisi kwa kufuatwa ndani ya nyumba yake.

Polisi wa nchi hii wanatakiwa wapelekwe the hegue.....!? Hapo walikuwa wanasitisha maandamano au walikuwa wanavamia wananchi!!?
Hasira itaniletea kiharusi, ngoja nilale mie!

Polisi wauaji inabidi washitakiwe au wananchi wachukue sheria mkononi walipe kisasi

sasa yule bibi wa miaka 90 wamempigia nini?inakuaje polisi wanabomoa mirango?nimeskititika sana.harafu polisi mjue nmewamind sana!.kwanini mnatuonea lakini?

jamani tumechoka kuona mauaji ya kila siku na hawa wanaotakiwa kuwa wanausalama,bibi wa watu kanifanya nitoe machozi alivyopigwa

Kama kawaida, vyombo vya dola vikiongozwa na polisi huko Geita vimeripotiwa kumuua mtu mmoja na kuwajarehi wengine kwa risasi za moto wakati raia hao wa kata moja ya Geita kuandamana kwa amani wakishinikiza diwani wao ajiuzuru baada ya diwani wao huyo kushiriki katika baraza la madiwani kumwondoa kiongozi aliyesadikiwa kutetea maslahi ya wananchi. Wananchi wanauliza, sisi ndio tuliomchagua diwani wetu na tuna haki ya kumwondoa tumepigwa na polisi kwa nini?

Source; ITV saa 8 usiku

Hii hali sasa inatisha!

Ndio Tatizo la kutokuwa na mamlaka ya kwa Viogozi wakuu ... Polisi wanajua ..Hatafanywa chochote ...na unajua nini..? watarudia tena na tena ..yuko wapi mwenye mamlaka ya kuongoza nchi kwa dhati na kuisimamia? ... Wachukuliwe hatua basi ..Leo arusha..kesho ..geita... kkutwa..mara... msururu ... Ahh just CraPp!!

poleni sana wafiwa ila ipo siku Mungu atatulipia tu
haiji akini kutumia risasi za moto kwa watu wasio na silaha au ndiyo wanajaribishia silaha wanazo nunua kila wakati kwa kodi zetu
POLISI WA NCHI HII MWOGOPENI MUNGU WENU

How long with this extra judicial killings, police state, police brutality, killings in cold blood? Haiwezekani, this cruelty of torturing and taking people's life should come to an end. Wale watu walikuwa wanaandamana peacefully wakimtaka diwani wao aondoke/ajiuzulu kwa kushiriki kwake katika kikao ambacho kilimwondoa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita. Namfahamu jamaa yule ni mpambanaji kweli. Recently alikuwa akipambana na GGM wale jamaa wa mgodi pale Geita kwa ukiukaji wa haki za binadamu hasa katika uchafuzi wa mazingira. Wananchi wamesema kuwa alikuwa mtetezi wao (wanyonge).

Polisi wamekwenda pale na mabomu ya machozi na wakapiga risasi za moto. Mtu mmoja wamemwua hivi hivi jamani. Wengine wanafuatwa majumbani na kupigwa. Kikongwe wa miaka 90 kapigwa pia. Watoto! How can one justify the continuity of killing unarmed people, demonstrating peacefully? No plz.

Ninaomba wenye data tuondelee kuzitunza na kama ninavyofahamu tume ya haki za binadamu inayo na Mh Lema alishawasilisha haya kule Bungeni sasa tutayapeleka UN na ICC tutawafungulia kesi hawa watawala na Police zao. Ninaamini binadamu wa mataifa wanaona na hawatakuwa tayari kutuangalia tunakwisha hivi hivi.

They will go, bush shit. CCM na akili zao za kijinga na ni huko huko Geita polisi wanamzuia Mbunge asiingie kwenye kikao cha halmashauri wajinga sana. Hao madiwani yawezekana wamehongwa na Mkurungenzi maana niliona akiwatetea sana hawa jamaa zake.

Mfumo wa mafunzo wa jeshi la polisi sharti iangaliwe upya. Yanayofanywa na polisi ni uzembe na kutojua majukumu yake. Kiwango cha ufaulu ni muhimu izingatiwe na kuacha kuchukua watu wasio na uwezo wa kufikiri. Kama shule kafeli polisi ndo ataweza?

watanzania tuunganishe nguvu lakini tukiendelea kutengana ooh, arusha ni wahuni haya leo geita, juzi ili kuwa tabora na nyamongo tukawaita majambazi lakini tulikuwa tayalikutoa zaidi ya mil 3 kwa kila jambazi iliziwasaidi kwenye mazishi sijui huruma hii imeanza lini..je kesho wataua wapi wasingizia nini..?

Polisi wanachotakiwa wkifahamu kuwa kuna baadhi yao wapo kwenye makazi mchanganyiko na hao raia wanaowapotezea maisha jamaa zao.
Ipo siku nao uvumilivu utawashinda na kuanza kuviziana vichochoroni kulipa kisasi.

wapumbavu kweli,kisa cha kuvunja mlango ni nini?walidhani kuna watu wanaandamana mpaka vyumbani?ipo siku tutawageuzia kibao ndo wakome.p**bu zao

Ndio Tatizo la kutokuwa na mamlaka ya kwa Viogozi wakuu ... Polisi wanajua ..Hatafanywa chochote ...na unajua nini..? watarudia tena na tena ..yuko wapi mwenye mamlaka ya kuongoza nchi kwa dhati na kuisimamia? ... Wachukuliwe hatua basi ..Leo arusha..kesho ..geita... kkutwa..mara... msururu ... Ahh just CraPp!!

Hah ha ha ha ha aaaaaaaa. Umenichekesha kweli!? Huyo ndo baba Riz bwana aka mzee wa suti. Utamwambia nini?

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom