nngu007
JF-Expert Member
- Aug 2, 2010
- 15,862
- 5,797
[h=2][/h]JUMAPILI, NOVEMBA 25, 2012 07:31 NA MWANDISHI WETU, BUKOMBE
*
*Polisi wampiga risasi kijana
*Wananchi watishia kuchoma kituo
MJI wa Bukombe jana uligeuka uwanja wa vita baada ya polisi kutumia risasi za moto na mabomu ya kutoa machozi kutawanya mamia ya wananchi waliotaka kuvamia na kukichoma moto kituo kikuu cha polisi.
Kitendo hicho kilitokana na polisi kumuua kwa kumpiga risasi mwananchi mmoja. Tukio hilo linadaiwa kufanywa na polisi aliyejulikana kwa jina moja la Manase.
Unyama huo unadaiwa kufanywa katika Kituo cha Polisi cha Ushirimbo Wilaya ya Bukombe mkoani Geita ambako askari huyo anadaiwa kumuua Rashid Juma (23).
Kuuawa kwa Juma kulisababisha fujo kubwa kati ya polisi na wananchi ambao walitaka kulipiza kisasi kwa kuvamia kituo na kutaka kukichoma moto.
Wananchi hao pia walitaka kumkamata askari aliyehusika na mauaji hayo ili wampige.
Kutokana na hali hiyo, askari walilazimika kurusha mabomu ya machozi, risasi za moto na risasi baridi kuwatawanya wananchi hao.
Licha ya kutumia nguvu kubwa, polisi walijikuta katika wakati mgumu baada ya kurushiwa mawe kila kona na kusababisha askari kadhaa kujeruhiwa vibaya na kuharibiwa mali za kituo hicho.
Inaelezwa kuwa tukio hilo lilitokana na polisi waliokwenda kumkamata mtu aliyedaiwa kuwa jambazi ambaye inasadikiwa alikuwa amejificha katika nyumba moja mtaa wa Kilimahewa.
Katika msako huo, polisi waliweza kumkamata mtuhumiwa huyo na kumweka ndani ya gari lao.
Baada ya kumkamata mtuhumiwa huyo, wananchi walilizingira gari la polisi wakitaka kumuona aliyekamatwa.
Ili kukabiliana na hali hiyo,polisi walilazimika kufyatua risasi hewani kuwatawanya na ndipo askari mmoja alipomlenga kijana Juma kiunoni na kumpiga risasi. Juma alifariki dunia papo hapo.
Baada ya kuibuka fujo hizo, Mbunge wa Bukombe, Profesa Kulikoyela Kahigi(CHADEMA), akiwa amefuatana na Diwani wa Kata ya Igulwa, Soud Ntanyagalla (CHADEMA), walifika eneo la tukio na kufanya kazi ya ziada kuwatuliza wananchi.
Miongoni mwa kazi kubwa walizofanya ni kuwatuliza ndugu wa marehemu akiwamo mama yake, Justina Francis ambaye alidai mwanae hajawahi kushiriki vitendo vya ujambazi.
Baada ya kuona hali imekuwa tete, Profesa Kulikoyela alimtaka Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Bukombe wafuatane hadi hospitalini kuona kama kweli Juma alikuwa amefariki dunia.
Hatua hiyo, ilitokana na madai ya polisi kwamba Juma alikuwa hajafa na alikuwa anaendelea kupatiwa matibabu.
Hata hivyo, baada ya kufika hospitalini, Mganga Mkuu wa Wilaya ya Bukombe, Dk.Archard Rwezahura aliwaeleza kuwa Juma alikuwa amekwisha kufariki dunia.
Alisema Juma alifariki dunia akiwa mikononi mwa polisi na hakufia hospitalini kama ilivyokuwa ikidaiwa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita,Lenard Paul alisema jeshi la polisi limeanza kufanya uchunguzi wa kina kubaini kama askari wake alijichukulia sheria mkononi.
Aliahidi ikibainika askari huyo atachukuliwa hatua zinazostahili.