Polisi waua tena; Risasi, mabomu vyarindima Bukombe; Polisi wampiga risasi kijana


nngu007

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Messages
15,871
Likes
77
Points
145
nngu007

nngu007

JF-Expert Member
Joined Aug 2, 2010
15,871 77 145

[h=2][/h]JUMAPILI, NOVEMBA 25, 2012 07:31 NA MWANDISHI WETU, BUKOMBE

*
*Polisi wampiga risasi kijana
*Wananchi watishia kuchoma kituo
MJI wa Bukombe jana uligeuka uwanja wa vita baada ya polisi kutumia risasi za moto na mabomu ya kutoa machozi kutawanya mamia ya wananchi waliotaka kuvamia na kukichoma moto kituo kikuu cha polisi.


Kitendo hicho kilitokana na polisi kumuua kwa kumpiga risasi mwananchi mmoja. Tukio hilo linadaiwa kufanywa na polisi aliyejulikana kwa jina moja la Manase.


“Unyama’ huo unadaiwa kufanywa katika Kituo cha Polisi cha Ushirimbo Wilaya ya Bukombe mkoani Geita ambako askari huyo anadaiwa kumuua Rashid Juma (23).


Kuuawa kwa Juma kulisababisha fujo kubwa kati ya polisi na wananchi ambao walitaka kulipiza kisasi kwa kuvamia kituo na kutaka kukichoma moto.


Wananchi hao pia walitaka kumkamata askari aliyehusika na mauaji hayo ili wampige.


Kutokana na hali hiyo, askari walilazimika kurusha mabomu ya machozi, risasi za moto na risasi baridi kuwatawanya wananchi hao.


Licha ya kutumia nguvu kubwa, polisi walijikuta katika wakati mgumu baada ya kurushiwa mawe kila kona na kusababisha askari kadhaa kujeruhiwa vibaya na kuharibiwa mali za kituo hicho.


Inaelezwa kuwa tukio hilo lilitokana na polisi waliokwenda kumkamata mtu aliyedaiwa kuwa jambazi ambaye inasadikiwa alikuwa amejificha katika nyumba moja mtaa wa Kilimahewa.


Katika msako huo, polisi waliweza kumkamata mtuhumiwa huyo na kumweka ndani ya gari lao.


Baada ya kumkamata mtuhumiwa huyo, wananchi walilizingira gari la polisi wakitaka kumuona aliyekamatwa.


Ili kukabiliana na hali hiyo,polisi walilazimika kufyatua risasi hewani kuwatawanya na ndipo askari mmoja alipomlenga kijana Juma kiunoni na kumpiga risasi. Juma alifariki dunia papo hapo.


Baada ya kuibuka fujo hizo, Mbunge wa Bukombe, Profesa Kulikoyela Kahigi(CHADEMA), akiwa amefuatana na Diwani wa Kata ya Igulwa, Soud Ntanyagalla (CHADEMA), walifika eneo la tukio na kufanya kazi ya ziada kuwatuliza wananchi.


Miongoni mwa kazi kubwa walizofanya ni kuwatuliza ndugu wa marehemu akiwamo mama yake, Justina Francis ambaye alidai mwanae hajawahi kushiriki vitendo vya ujambazi.


Baada ya kuona hali imekuwa tete, Profesa Kulikoyela alimtaka Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Bukombe wafuatane hadi hospitalini kuona kama kweli Juma alikuwa amefariki dunia.


Hatua hiyo, ilitokana na madai ya polisi kwamba Juma alikuwa hajafa na alikuwa anaendelea kupatiwa matibabu.


Hata hivyo, baada ya kufika hospitalini, Mganga Mkuu wa Wilaya ya Bukombe, Dk.Archard Rwezahura aliwaeleza kuwa Juma alikuwa amekwisha kufariki dunia.


Alisema Juma alifariki dunia akiwa mikononi mwa polisi na hakufia hospitalini kama ilivyokuwa ikidaiwa.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita,Lenard Paul alisema jeshi la polisi limeanza kufanya uchunguzi wa kina kubaini kama askari wake alijichukulia sheria mkononi.


Aliahidi ikibainika askari huyo atachukuliwa hatua zinazostahili.

 
K

Kagalala

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2010
Messages
2,373
Likes
90
Points
145
K

Kagalala

JF-Expert Member
Joined Oct 31, 2010
2,373 90 145
Kwa Tanzania hilo halina shida. Polisi kuua imekuwa kitu cha kawaida na IGP Mwema anazidi kula nchi tu. Only in Tanzania
 
S

Salary Slip

JF-Expert Member
Joined
Apr 3, 2012
Messages
30,416
Likes
58,171
Points
280
S

Salary Slip

JF-Expert Member
Joined Apr 3, 2012
30,416 58,171 280
Habari ya polisi kuua raia kwa hapa bongo umekuwa kama wimbo usiochuja.

Nahisi IGP anaupenda sana wimbo huu na kila siku anawatuma vijana wake wau-rewind.
 
Shomari

Shomari

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2008
Messages
1,106
Likes
7
Points
135
Shomari

Shomari

JF-Expert Member
Joined Mar 8, 2008
1,106 7 135
Mh! habari ya lini hii?
 
Katavi

Katavi

Platinum Member
Joined
Aug 31, 2009
Messages
40,274
Likes
4,736
Points
280
Katavi

Katavi

Platinum Member
Joined Aug 31, 2009
40,274 4,736 280
Hawa askari wakiendelea hivi sijui wataashi wapi...!!
 
Myakubanga

Myakubanga

JF-Expert Member
Joined
Oct 3, 2011
Messages
5,813
Likes
388
Points
180
Myakubanga

Myakubanga

JF-Expert Member
Joined Oct 3, 2011
5,813 388 180
Serikali ya kidhalimu na mauaji ya Kikwete!!
 
Konya

Konya

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2011
Messages
920
Likes
11
Points
35
Konya

Konya

JF-Expert Member
Joined Jun 4, 2011
920 11 35
wakati mjomba ndo hata hayamgusi wala kukemea haya maovu juu ya askari wake kuwa na utaratibu wa kuua raia wasio na hatia
 
CRN

CRN

Member
Joined
Oct 24, 2012
Messages
60
Likes
0
Points
0
CRN

CRN

Member
Joined Oct 24, 2012
60 0 0
hii mada kuichangia inahitaji uwe na moyo kama wa mwenda wazimu,mana pande zote mbili zinamapungufu katika hili,si polisi wala raia wote hapo wamebugi step.
 
Mjuni Lwambo

Mjuni Lwambo

JF-Expert Member
Joined
Apr 25, 2012
Messages
6,082
Likes
1,443
Points
280
Mjuni Lwambo

Mjuni Lwambo

JF-Expert Member
Joined Apr 25, 2012
6,082 1,443 280
Ririkuwa rinapambana na porisi tukarishinda.
 
N

ngonani

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2012
Messages
1,371
Likes
199
Points
160
N

ngonani

JF-Expert Member
Joined Aug 27, 2012
1,371 199 160
Askari walienda kumuokoa mtu aliyedaiwa kuwa mwizi na ambaye alikuwa amezingirwa na wananchi wakitaka kuchukua sheria mikononi,hata hivyo wananchi walichachamaa kuzuia mtu huyo asichukuliwe na polisi,kwa kutumia silaha za jadi waliwavamia polisi na kufanya uharibifu mkubwa kwenye gari lao,polisi kujinusuru waliruka kwenye gari na kujaribu kukimbia toka eneo ilo,wananchi walifanikiwa kumzuia askari Manase asirukie kwenye gari na bila wenzake kutambua gari liliondoka na kumuacha Manase nyuma huku amezingirwa na wananchi waliotaka kumtoa roho wakichukizwa na kitendo cha wenzake kumuokoa mtuhumiwa wa wizi,wakiwa katika harakati za kutaka kumuua ilibidi apige risasi hewanikuzuia wananchi wenye hasira wasimfikie,wananchi hawakutii na kuendele kumfuata wakiwa na lengo la kumuua,kujinusuru alipiga risasi zaid na moja kati ya hizo ikampata marehemu,wenzake walipigiwa simu na kurudi eneo la tukio na kumnusuru Mananse,baada ya polisi kuondoka wananchi walimbeba majeruhi na badala ya kufanya jitihada za kumkimbiza hospitali walimbeba na kuondoka naye huku wakiandamana umbali mrefu tu kuelekea kituo cha polisi na walipofika kituo cha polisi walianzisha vurugu za kutaka kuchoma kituo,na walipozidiwa walimtelekeza majeruhi na alifia nje ya kituo kwa kukosa huduma za haraka.Kwa maoni yangu sio kila wakati askari wanapouwa wanakuwa wamefanya makosa,hata wenzangu wanajamvi katika mazingira hayo mngekuwa nyie ndio askari Manase mngechukua hatua gani,inabidi busara itumike,otherwise mashinikizo ya wanasiasa mfano ya DC na mbunge wa Bukombe ambaye ni CHADEMA yanaweza kusababisha askari awe victimized bure kitu amabacho kinaweza kuathiri morari ya askari wengine.Raia waelimishiwe kuwa bunduki wanazotembea nazo askari sio toy,unapotaka ku mu attack askari mwenye silaha unategemea aitupe chini aokote fimbo kujitetea,na kama ni watu zaidi ya mia wenye silaha mbalimbali wanakujongelea wakitaka kukuua,wewe ukae tu wakati bunduki unayo,inabidi ujitetee kunususru maisha yako.Mimi kuna wakati uwa siko upande wa askari wanapofanya mauaji mfano ya Mwangosi,lakini kwa ili la Bukombe mimi namtetea sana huyu askari.Magazeti yasiwe biased yaandike ukweli kama ulivyo.
 
Pancras Suday

Pancras Suday

Verified User
Joined
Jun 24, 2011
Messages
7,463
Likes
1,504
Points
280
Pancras Suday

Pancras Suday

Verified User
Joined Jun 24, 2011
7,463 1,504 280
Dah! Naona kwa mbali sana somalia ya bongo ikaribu
 
Pancras Suday

Pancras Suday

Verified User
Joined
Jun 24, 2011
Messages
7,463
Likes
1,504
Points
280
Pancras Suday

Pancras Suday

Verified User
Joined Jun 24, 2011
7,463 1,504 280
ngonani Aghaaah! Nawe usituchanganye, wakati wote ulikuwa wapi kuripoti hii habari yako au unapima upepo?
 
Last edited by a moderator:
Rapherl

Rapherl

JF-Expert Member
Joined
Jun 20, 2012
Messages
3,310
Likes
1,493
Points
280
Rapherl

Rapherl

JF-Expert Member
Joined Jun 20, 2012
3,310 1,493 280
ngonani Kama ni hvyo unavyosema basi huyo askar hana makosa,Raia tuache kujichukulia sheria mikononi.
 
Last edited by a moderator:
Inno laka

Inno laka

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2012
Messages
1,591
Likes
449
Points
180
Age
26
Inno laka

Inno laka

JF-Expert Member
Joined Mar 24, 2012
1,591 449 180
Kazi nzuri kamanda....dat iz good job umeokoa uhai wako kamanda pamoja na hyo silaha yetu.....unajua hawa Raia wanaboa sana.,wanakera mda mwingne unaweza ukaua hata bila kukusudia jaman hzo bunduki sio kwa ajili ya wanyama nikwaajil ya binadamu kama hao kina mwa...

Huyu askar ni shujaa watu wote wale kaua tu mmoja.
 
amkawewe

amkawewe

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2011
Messages
2,028
Likes
12
Points
135
Age
28
amkawewe

amkawewe

JF-Expert Member
Joined Dec 9, 2011
2,028 12 135
ngonani Ulikuwa eneo la tukio? Je, wewe ni askari au raia wa kawaida? Je, tutakuaminije?
 
Last edited by a moderator:

Forum statistics

Threads 1,214,714
Members 462,830
Posts 28,520,719